Zijue tabia za Kanisani

Zijue tabia za Kanisani

Macho hayana mpaka mkuu, ndio maana tanawashauri dada zetu wavae mavazi ya kijisitiri vyema.

Wasipovaa vyema watasababisha wengine watende dhambi.
mida yaasubuhi nimeona mdada anaenda chach na Bible yake kava kimini mapaja yote wazi na ana wowowo sijui waumini wakiume watakua nahali gani huko
 
Kiuhalisia hiyo haiwezi kuwa na tija
"Mpingeni shetani naye atawakimbia"

Huwezi subiri mtu mmoja tu miongoni mwa watu zaidi ya mia awe mpigaji pekee.

Mapepo ni jeshi lazima yapingwe na Jeshi la waimbaji.
 
Kwa akina dada vaa nguo yenye kusitiri mwili wako, ficha matiti yako na usionyeshe mapaja na matako yako ukiwa kanisani - haswa ikiwa umeketi mbele au unaongoza nyimbo za sifa na ibada. Kwa nini umkengeushe nabii na waabudu wengine?

Ukiwa kanisani, zima simu yako. Epuka kutafuna big G. Na usitupe takataka kanisani.

Ukiwa na changamoto ya kusikia usingizi wakati wa ibada, kaa safu ya katikati nyuma kabisa. Unaweza pia kupiga miayo huko.

Acha kuwatazama watu wanapoomba na kusifu - wewe pia umeenda kanisani kuabudu na kusifu hivyo sifu na uombe kama wao.

Acha kuchezea kurasa za biblia hovyo hovyo maana kufanya hivyo ni kukosa adabu - unaweza kufanya hivyo kibinafsi ukiwa nyumbani kwako.

Tafadhali jali watoto wanaolia. Usiondoke kabla ibada haijamaliza, isipokuwa kama utapata dharura.

Kama lilivyo shirika lingine lolote, kanisa pia lina bili - usiende kanisani mikono mtupu nenda na sadaka.

Ikiwa hujui kuimba ama huwa unaimba off-tune kama mimi, tafadhali punguza sauti yako[emoji1787]

Wengine wakimaliza kuomba tafadhali nyamaza. Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko (1Kor 14:33).

Kwa wanandoa, peaneni mabusu mkiwa nyumbani au kwenye gari na sio ibadani.

Nakutakia ibada njema.

Ubarikiwe.
kwa wasabato na waloma sawa lakini haya makanisa ya walanguzi hilo aliwezekani
 
Hairuhusiwi bible kwenye simu ni kwenye private area na sio kanisani.
Ukiwa kanisani nani anacontrol attention YAKO.
private area kivipi? Na huku kuna wachungaji wanatumia na ibada zinaendeshwa vizuri sana.
 
Ikiwa hujui kuimba ama huwa unaimba off-tune kama mimi, tafadhali punguza sauti yako
emoji1787.png
Sasa hawa ndiyo wengi tena wanatoka kwenye viti wanaingia kwenye isle na kuimba kwa kuzungukazunguka, watafitiwe gavana
 
Waimbaji ni jambo jingine na maombi ya sauti ni jambo jingine
Sikia ndugu nyimbo za ibada sio burudani bali ni jumbe zenye nguvu ya Mungu, huweza hata kuangusha ngome na mamlaka ya shetani

Kumbuka Paul na Sila walifanya kitu kama hicho gerezani walipokuwa wamefungwa kwa hila, mwisho wa siku walishinda.
 
Hilo ulijualo wewe ndio upuuzi huo huo wa ku switch on simu yako ukiwa katika Ibada.

Nakutakia ibada njema.
perception yako ya hovyo kweli,,,basi unaamini una-amini kila anayeswitch on simu yake,,,anakuwa na mambo ya hovyo kama yaliyo kwenye simu yako,,,i feel you sorry!
 
Sikia ndugu nyimbo za ibada sio burudani bali ni jumbe zenye nguvu ya Mungu, huweza hata kuangusha ngome na mamlaka ya shetani

Kumbuka Paul na Sila walifanya kitu kama hicho gerezani walipokuwa wamefungwa kwa hila, mwisho wa siku walishinda.
Hatukatai, hoja yangu kwanini watu wote kwa pamoja wasali kila mtu kivyake tena kwasauti kubwa na kupoteza kusikilizana?
 
private area kivipi? Na huku kuna wachungaji wanatumia na ibada zinaendeshwa vizuri sana.
Wao ni sahihi Ili kurahisisha ufundishaji.
Wengine amchelewi kutazama ngono ibada ikiendelea
 
Hatukatai, hoja yangu kwanini watu wote kwa pamoja wasali kila mtu kivyake tena kwasauti kubwa na kupoteza kusikilizana?
Katika maombi huwa kuna kiongozi wa maombi, huyo husimamia zoezi zima la maombi, ndio maana kuna ushauri kama huu "ukisikia wengine wamenyamaza nawe nyamaza"

Hapo kiongozi atakuwa ktk nafasi yake kusimamia maombi hatua kwa hatua.
 
Back
Top Bottom