Zijue taratibu za kufuata ili kufungiwa umeme na TANESCO

Mungu wangu mm nimelipia nguzi moja mwezi jmepita sasa na niko mita 200 kutoka Tanesco yaani barabarani kabisa na niombi la kwenye nyumba za taasisi lkn hata dalili sioni!
 
Tanesco kuna hitaji kubwa la kufanyiwa overhaul kuanzia wakubwa wenu mpaka ngazi za chini, jana nimejionea ndugu yangu wa Kibaha karudisha form pale mailimoja ambapo nyumba husika ina miundo mbinu yote ipo na yeye anahitaji extension meter tu kwani ni mpangaji na amechoka kugombana na wapangaji wenzake ambao ni wakorofi, nashangaa eti kaambiwa arudi nyumbani akamsubiri Suveyor ambaye atamtembelea after two weeks (not within 7 days), kweli kama ningekuwa DG wenu ningeanza na huyo zonal meneja wenu hapo Kibaha, acheni kufanya kazi kwa mazoea jamani
 
Mimi nilifwatiria taratbu zote za kufungiwa umeme kosa nililokosea nilianza kutafuta pesa kabla Umeme
Wakati nafatiria taratibu za Umeme nilikuwa na 450,000 mpaka jibu la ghalama 320,7720 zinazotakiwa tanesko natumiwa kwenye cm ni dhaid ya miezi 2 pesa kwisha mpango wa pesa kama ile kwisha sasa ninachotaka kujua upo uwezekano wa mteja kulipa kidogo kidogo ?
 
Heshima kwenu Tanesco.
Naomba kujuzwa taratibu za kuhamisha nguzo ya Umeme iliyowekwa kimakosa Njia ya kwenda kwangu .

Hongereni sana kwa kazi nzuri mnazofanya
 

Mkuu! Kuunganishiwa umeme kwenye nyumba ama kimradi sh ngapi?
 
tanesco urasimu bado haijaishaa... Rushwa kama haki yao... Takukuru wakiwa Serious kabisa kabisa upande ea Tanesco, watu wengi wataacha kazi
 
Tanesco hizo mita zishafika na kuanza kuzigawa au bado,maana muda ss ni sound ya mita azijafika!
 
Nipo wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera, nimelipia umeme baada ya kukamilisha taratibu zote, nyumba ipo ndani ya umbali wa mita 30 (i.e. 19 meter) kutoka kwenye nguzo leo ni siku ya 36 sijafungiwa mita. Kila nikiuliza naambiwa mita hazijaja kutoka Bukoba mara hakuna nyaya. Naomba unisaidie kufuatilia ili nifungiwe umeme kama ulivyoainisha kuwa ni ndani ya siku 30 za kazi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na ile naona wanaandika volt 380 ina maana ni below au na resistsnce Mohms kwa single na three phase huwa ni nagapi?
 
hapo kwa kuangalia mita za aina gani ?
 
saaaaaafiiiiiiiiiiiiiiii nimeelewa
naomba katika hiyo mikataba jaribuni pia kuandika lugha ya kiswahili maaana mmeandika kiingereza jambo ambalo ni shida si wote watumiaj wa lugha hii sasa we udhadhani ntafanya nini zaid ndo hivyo kukumbushana kusign bogus treat mwisho wa siku ndo mambo kama haya wengi wetu tunaambiwa sign hupo chini nasign kumbe kuna mambo mengine kama hayo ss ni watanzania lazma lugha yetu ipewe kipaombele kama watakuja wazungu bas wawe na fomu zao au kama ni shida wekeni lugha mbili pale ya kiingeza na tafsiri yake pale maana % kubwa mnaotuhudumia ni cc watanzania tena watumia kiswahili kuliko hiyooo
 
Thanks
 
Tanesco ifutwe haina faida inajiendesha KIBWANYENYE sana! Dar kuna sehemu umeme haujafika vipi kuhusu NAMINYWIRI? Vipi Kuhusu NAMTUMBO? Vipi Kuhusu NYAMISATI,vp kuhusu NAMANYERE,NKASI? Vipi Kuhusu KAZURAMIMBA?




 
Ndugu mpendwa mteja wetu kwa heshima kubwa kabisa tunaomba uambue kuwa TANESCO kupitia usimamizi mzuri wa serikali yetu imefanya kazi kubwa sana haswa kwenye uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme.utakuwa shahidi kuwa leo vijiji vingi na maeneo mengi ya mijini yafurahia umeme. Shirika linaendelea kusambaza umeme kwa awamu mbalimbali hivyo uvumilivu wako na taarifa sahihi za eneo lako na namba yako ya simu itatusaidia kukupatia ufafanuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maeneo yote hayo uliyotaja umeme upo ni baadhi ya maeneo machacha haujafika hivyo ni vema kutuunga mkono badala ya kuona hatujafanya chochote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliomba umeme mwaka 2016 mpaka sasa haujafika,nilijaribu kufatilia nikaambiwa baadhi ya wafanyakazi wasio waaminifu wa TANESCO wamekula fedha ya mradi karibia milioni mia 5,kwasasa nimefunga solar tu,nguzo zipo tu zimeachwa kama mapambo ila kwenye vikao vya kwenu huko huwa wanasema TAYARI TUSHAPATA Umeme wakati Fedha 500m watu wamekula!! Tushaandika Barua kwenda kwa Waziri kuelezea huo WIZI tunasubiri majibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…