Zijue taratibu za kufuata ili kufungiwa umeme na TANESCO

Zijue taratibu za kufuata ili kufungiwa umeme na TANESCO

Niliomba umeme mwaka 2016 mpaka sasa haujafika,nilijaribu kufatilia nikaambiwa baadhi ya wafanyakazi wasio waaminifu wa TANESCO wamekula fedha ya mradi karibia milioni mia 5,kwasasa nimefunga solar tu,nguzo zipo tu zimeachwa kama mapambo ila kwenye vikao vya kwenu huko huwa wanasema TAYARI TUSHAPATA Umeme wakati Fedha 500m watu wamekula!! Tushaandika Barua kwenda kwa Waziri kuelezea huo WIZI tunasubiri majibu.
Nani alikuambia maneno hayo? Jr mradi wa REA unatakelezwa na TANESCO? Turudi kwenye kukusikiliza upo wilaya gani? Namba ya simu tafadhali na eneo husika unalozungumzia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maeneo yote hayo uliyotaja umeme upo ni baadhi ya maeneo machacha haujafika hivyo ni vema kutuunga mkono badala ya kuona hatujafanya chochote

Sent using Jamii Forums mobile app
Uwepo wa Umeme kwa hayo maeneo ni kitu kimoja na kupeleka kwa wananchi/wakazi wa hapo ni kitu kingine,Tumeshuhudia umeme mkubwa unapita kwenye vijiji na wananchi wanauangalia tu lakini hawana unaenda kuwekwa kwenye ofisi za wilaya nyingine za serikali/nyumba ya rc/dc huku ukiwapita wanakijiji.

Tatizo la TANESCO ni Rushwa na Ubwanyenye,mpo peke yenu mmemonopoly soko ,mngekuwa na mshindani kama kampuni za simu mngetia akili,Bunge waruhusu kampuni binafsi za kusambaza umeme mfe kifo kama cha ttcl/atcl,mtu anaomba umeme miaka mi3 hakuna kitu mnamjibu kwa umbali huo hapo ni mradi unatakiwa tunasubiri mradi uje kumbe fedha za mradi na zenyewe zimeliwa na wajanja,hivi hakuna TOP management wanaofatilia maendeleo ya miradi?
 
Nani alikuambia maneno hayo? Jr mradi wa REA unatakelezwa na TANESCO? Turudi kwenye kukusikiliza upo wilaya gani? Namba ya simu tafadhali na eneo husika unalozungumzia

Sent using Jamii Forums mobile app
Subiri tu FEEDBACK ya WAZIRI kuhusu huo wizi ndio utaamini,Hauwezi Kutenganisha REA na TANESCO,wote ni watoto wa BABA na MAMA Mmoja ndio maana tukinunua umeme TANESCO tnakatwa fedha ya REA.
 
Mimi naomba kuuliza hivi nyumba ambayo haiitaji nguzo kuingiza umeme yaani iko mita chache kutoka kwenye nguzo ya umeme gharama ni kiasi gani?Maana yangu ni kwamba zinahitajika waya tu ili kuingiza umeme kwenye nyumba
 
Uwepo wa Umeme kwa hayo maeneo ni kitu kimoja na kupeleka kwa wananchi/wakazi wa hapo ni kitu kingine,Tumeshuhudia umeme mkubwa unapita kwenye vijiji na wananchi wanauangalia tu lakini hawana unaenda kuwekwa kwenye ofisi za wilaya nyingine za serikali/nyumba ya rc/dc huku ukiwapita wanakijiji.

Tatizo la TANESCO ni Rushwa na Ubwanyenye,mpo peke yenu mmemonopoly soko ,mngekuwa na mshindani kama kampuni za simu mngetia akili,Bunge waruhusu kampuni binafsi za kusambaza umeme mfe kifo kama cha ttcl/atcl,mtu anaomba umeme miaka mi3 hakuna kitu mnamjibu kwa umbali huo hapo ni mradi unatakiwa tunasubiri mradi uje kumbe fedha za mradi na zenyewe zimeliwa na wajanja,hivi hakuna TOP management wanaofatilia maendeleo ya miradi?
Unapotoa tuhuma bila ushahidi au ushirikiano kwetu unapenda tukuhudumiaje mpendwa mteja? Unaposema maeneo hayo hayana umeme wakati vijiji vingi vinaumeme unakuwa unamaanisha Namtumbo yote haina umeme? Tunaomba tukusikuliza maana huu ni ukurasa wa huduma kwa wateja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi naomba kuuliza hivi nyumba ambayo haiitaji nguzo kuingiza umeme yaani iko mita chache kutoka kwenye nguzo ya umeme gharama ni kiasi gani?Maana yangu ni kwamba zinahitajika waya tu ili kuingiza umeme kwenye nyumba
Tafadhali pitia maelezo yetu
IMG-20190224-WA0047.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unapotoa tuhuma bila ushahidi au ushirikiano kwetu unapenda tukuhudumiaje mpendwa mteja? Unaposema maeneo hayo hayana umeme wakati vijiji vingi vinaumeme unakuwa unamaanisha Namtumbo yote haina umeme? Tunaomba tukusikuliza maana huu ni ukurasa wa huduma kwa wateja

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama DAR kuna Sehemu Kibao Umeme hakuna sina Shaka kabisa huko namtumbo wananchi wengi hawana UMEME.
 
Naomba mfanye marekebisho na muandike kuwa kugungiwa umeme baada ya kufanya malipo itategemea na upatikanaji wa nguzo. Nimelipia na siku 60 zimepita lakini naambiwa nisubiri mpaka wateja wa mwezi wa 9 wamalizike kwanza. So sioni logic ya kusema ndani ya siku kadhaa kwa kweli
HATUA YA KWANZA

MAOMBI YA MWANZO


Je mteja anaweza kuchukua fomu ofisi yeyote ya tanesco?

Mteja anaweza kuchukua fomu ya maombi ya umeme katika ofisi yeyote ya shirika bila kujali kuwa eneo hilo linahudumiwa na ofisi husika. Ila atapaswa kurudisha ofisi ya maeneo ambayo makazi yake yapo ili kurahisisha kufanyiwa vipimo (service line survey)

JE KUNA GHARAMA ZOZOTE KATIKA UCHUKUAJI WA FOMU?

Fomu za maombi ya umeme zinatolewa bure kabisa kwa wateja wote.

VITU MUHIMU VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUCHUKUA FOMU

1. Hakikisha umeme umefika maeneo yako na kama ni mradi uwe umekamilika.

2. Hakikisha mtandao wa nyaya ndani ya nyumba yako (wiring) umefanyika kupitia mkandarasi aliyesajiliwa.

3. Kitambulisho kinachomtambulisha muombaji wa umeme mfano leseni ya udereva, hati ya kusafiria, kitambulisho cha kazi (hii inasaidia shirika kumtambua mteja husika)

4. Kwa mwombaji wa mita ya ziada (meter separation) jina litakalotumika ni la mwenye nyumba kama linavyosomeka katika mita ya awali. Vinginevyo mteja atapaswa kutumia uthibitisho wa ruhusa ya mwenyenyumba kama atakuwa ni mpangaji. Lazima mteja aje na namba ya mita (kama zipo zaidi ya moja aje nazo zote) ili kuhakiki kama kuna yenye deni.


5. Kwa waombaji wanaomba kwa ajili ya ofisi, makapuni au taasisi za serikali au binafsi anapaswa kuja na leseni ya biashara, tin namba, udhibitisho wa usajili wa kampuni. Au udhibitisho wa ofisi ya serikali husika.

6. Kwa wapangaji wa nyumba za taasisi au makampuni waje na barua za waliopangisha zinazoonyesha kuwe wenye nyumba hizo wameridhia mita husika iwe na jina la mpangaji husika.

7. Shirika linapenda kuwaomba wamiliki wa nyumba kupenda kufika ofisi zetu wenyewe ili kuzuia udanganyifu ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu

HATUA YA PILI KUWEKA MCHORO, PICHA NA KUINGIA MAKUBALIANO YA KUFUNGIWA UMEME NAKUREJESHA FOMU

Endapo mteja atakidhi vigezo na masharti ya hatua ya mwanzo na kupatiwa fomu ya maombi ya mwanzo anatakiwa afanye yafuatayo

1. Kuisoma fomu kwa umakini mkubwa na kukubailiana na vigezo namba moja mpaka kumi na mbili. Mteja akijiridhisha kuwa amekubaliana na masharti yote ataweka sahihi sehemu husika (ukurasa wa pili wa fomu ya maombi ya umeme)

2. Kumpatia mkandarasi aliyesajiliwa ili achore mchoro wa mtandao wa nyaya (wiring diagram) wa nyumba husika pamoja na kugonga muhuri. (gharama ni makubaliano baina ya mteja na mkandarasi husika), wakandarasi wanapatikana kwenye ofisi zao maeneo mbalimbali, orodha ya waliosajiliwa pia inapatikana kwenye ofisi za tanesco. Mteja anapaswa kupewa orodha na kuchagua mkandarasi anayemtaka yeye.

3. Mteja atapaswa kuweka picha moja ya mwombaji wa umeme

4. Kisha mteja atarudisha fomu hiyo iliyokamilika ofisi ya eneo ambalo makazi yake yako (inayomudumia)

HATUA YA TATU- KUFANYIWA VIPIMO (SURVEY)

Mara baada ya mteja kurejesha fomu iliyojazwa kikamilifu, mteja atapangiwa tarehe ya kufanyiwa vipimo (survey). Mafundi watafika kwenye nyumba au sehemu inayoombewa umeme ili kutathimini gharama atakazolipia mteja kwa kuzingatia umbali wa eneo ilipo miundombinu ya umeme kama nguzo na transfoma na uwezo wa umeme huo kuunganisha kwa wateja wapya.

HATUA YA NNE: - KUPATIWA MAKADIRIO YA GHARAMA KIASI GANI ALIPE ILI AFUNGIWA UMEME

Mara baada ya kufanyiwa tathimini mteja anaweza kupatiwa makadirio ya gharama ya kiasi gani alipe ili kufungiwa umeme. Makadirio haya huweza kutumwa kwa njia ya nukushi, ujumbe mfupi wa meneno, barua pepe au mteja kufika ofisini na kuchukua barua. Viwango vya muda wa kutoa makadirio kama inavyoonekana kwenye jedwali hapo chini:

MAELEZO

Muda wa makadirio

Kama miundombinu iliyopo itatumika (ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo iliyokaribu)

Ndani ya siku 7 za kazi

Ujenzi wa njia ya nyongeza unahitajika (mita 30- 100)

Ndani ya siku 10 za kazi

Kama mfumo mpya wa usambazaji unahitajika kujegwa au mfumo wa umeme mkubwa unahitajika kuongezwa kwa ajili ya kiwanda au biashara kubwa (kama hakuna mfumo wa kumuunganishia mwombaji) (zaidi ya mita 100)

Ndani ya siku 14 za kazi

HATUA YA TANO: - KUFANYA MALIPO

Mteja atafika ofisi ya tanesco ili kupatiwa namba ya kumbukumbu (reference number) itakayomuwezesha kufanya malipo bank, mteja atafanya malipo na atapatiwa stakabadhi ya malipo bank (risiti kwa njia ya ujumbe mfupi- sms) (kwa sasa ni bank ya nmb tu), wateja wanahimizwa kufanya malipo yote bank na si kwa mtu mwingine yeyote. Malipo yote yatakayofanyika nje ya mfumo uliwekwa hayatambulika na tanesco. Mteja akishafanya malipo bank husika hatatakiwa kurudi tena tanesco bali tanesco watakuwa na taarifa zake zote na kinachofuata ni kumfungia umeme.

HATUA YA SITA:-KUUNGANISHIWA UMEME

Mara baada ya mteja kufanya malipo viwango vya muda wa kumfungia umeme vitakuwa kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali hapo chini.

MAELEZO

Muda wa kufungiwa

Kama miundombinu iliyopo itatumika (ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo iliyokaribu)

Ndani ya siku 30 za kazi

Ujenzi wa njia ya nyongeza itahitajika

(mita 30- 100)

Ndani ya siku 60 za kazi

KAMA MFUMO MPYA WA USAMBAZAJI UNAHITAJIKA KUJEGWA AU MFUMO WA UMEME MKUBWA UNAHITAJIKA KUONGEZWA KWA AJILI YA KIWANDA AU BIASHARA KUBWA (KAMA HAKUNA MFUMO WA KUMUUNGANISHIA MWOMBAJI) (ZAIDI YA MITA 100)

Ndani ya siku 90 za kazi

KWA MAULIZO WASILIANA NASI

Kituo cha huduma kwa wateja: - 0768985100/0222194400

Barua pepe: customer.Service@tanesco.Co.Tz

Facebook: www.Facebook.Com/tanesco yetu

Twitter: - www.Twitter.Com/tanesco yetu

Tovuti; www.Tanesco.Co.Tz

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TANESCO IS A DEAD WORKING ORGANISATION, EVERY DEPARTMENT IS TOTALLY PALSY, Mtu aliyelipia Umeme Mwezi wa Saba hadi leo hajapata umeme bado mnajinadi eti tunatekeleza...
Serikali inatakiwa ifanye overhaul kuanzia Sangara hadi Dagaa, Nadhani ni moja ya corrupt organization kwa Sasa ukiondoa
Police, judiciary, lands and Tanzania Revenue Authority (TRA).... TANESCO
 
Huo utaratibu upo kwenye maandishi si kiuhalisia kabisa....Mngeongezea na suala la kununua nguzo
 
MM NI MHANGA WA TANESCO SENGEREMA NILICHUKUA FOMU 23 03 2018 NIKARUDISHA FOMU YANGU MWEZI WA TATU MWAKA JANA YANI 2018 BAADA YA KUKAA SANA NIKAFATILIA MNAMO MWEZI WA TISA FOMU IKAPATIKANA BAADA YA HAPO SAVERY AKAENDA SITE NIKAFANYIWA HESABU NIKALPA GHARAMA MWAKA JANA MWEZI WA 11 CHA KUSHAGAZA MPAKA LEO HII NAANDIKA HAKUNA HATA DALILI PESA NIMELIPA SIDAIWI LEO MIEZI MITANO TOKA NILIPE NAULIZA FOMU YANGU IMEPOTEA TENA AU TATIZO LIKO WAPI/ MALIPO YALIPOKELEWA KWENYE ANKARA NA 991030600443 TSH 362885 RISITI NA 99009696782 KUPITIA EC 100278236428 HIVI VYOTE NIMEFANYA NIFANYEJE
 
Back
Top Bottom