Zijue taratibu za kufuata ili kufungiwa umeme na TANESCO

Ubarikiwe sn mkuu.

Nitaiweka hii kitu kumbe.
 
Mkuu kuna upungufu wa material hasahasa nguzo hivyo kwakuwa umeshasambaziwa nguzo ujenzi wake basi sio siku nyingi kwakuwa kwa wateja wa nguzo huwa wanasambaza kwanza nguzo wakija wanasimamisha na kuwasha umeme. Kama nguzo wameleta hapo chekelea tu

Kuhusu hiyo ya REA siwezi kukupa jibu la uhakika ila ukishalipia kwenye REA wala Tanesco wanakuwa hawahusiki maana hata hela uliyolipa ni VAT na inaenda TRA wala sio kwa Tanesco.

Ukishalipa Tanesco hukabidhi kazi yako kwa contractor aliyepewa tender na REA kwa sehemu husika na huyo mkandarasi ndie naehusika kuja kufunga umeme wala sio Tanesco.
 
Tunashukuru kuna maeneo kule moshi vijijini ambayo yalibahatika kuwa na umeme tooka enzi za mwalimu na kila uchwao kule nyumba zinajengwa na mahitaji ya umeme kuongezeka sasa mdau kero yake inakuja baadhi ya maeneo ambayo nimeshuhudia kwa macho yangu umeme wake ule mwanga ni bora uwashe chemli au mshumaa yaani ni mdogo tena unaumiza macho tena ikifika majira ya jioni ambapo uhitaji huongezeka ukiwasha taa zingine haziwaki kabisa tembeleeni huko vijijini hasa vunjo mkajionee
 
TANESCO kwanaza nawashukuru kwa kuwa na account yenu humu jamii f. Naomba kuuliza haya maswali. Mosi IPI ni gharama halisi ya kuunganisha Umeme wa REA vijijini? Pili, Mimi nipo katika kijijini cha Itale wilayani Ileje ambapo kwa sasa ndo Umeme umeanza kuunganishwa na tumetozwa sh elfu sabini na saba (77000) kwa kila anayetaka kuunganishwa Umeme na mkandarasi anasema elfu 27 ni ya TANESCO na elfu 50 ni ya mkandarasi. Je, ni halali hiyo? Tatu huwa hatoi list na anaandika jina tu na kwa kuwa inakuwa na uongozi wa kata na kijijini basi watu hukubali tu, je utaratibu unakuwaje? Mwisho napenda niuombe uongozi wa TASESCO ebu mtusaidie sisi wanakijiji cha Itale -Ileje maana wengi naona wataliwa fedha na wahuni kupitia mgongo wa wakandarasi uchwara.
 
Hao watoe taarifa hapo Himo (kama sijakosea) kuna low voltage na Tanesco watafanya Voltage improvement kwa ku upgrade size ya transformer au kuweka TF jingine
 
huko ikonda nililipa kwa tanesco ila nilivyowasumbua sana wakaniambia mradi upo chini ya REA, na REA haina fedha tena mpaka mwaka mpya wa fedha nkachoka.
 
Mkuu kama unatozwa 77k hiyo ni bei ya kuunganishiwa umeme kwa maeneo ya kijijini.

Hiyo 150 inaenda Tanesco kama uko vizuri kihisabati basi uki calculate VAT ya hiyo 150 k ni 27k na sio kwamba inaenda REA bali kodi ya ongezeko la thamani inaenda TRA na sio REA
 
Tanesco nyie no waongo,labda maeneo mengine ya nchi. NIKO NYAMONGO NIMELIPA UMEME TA NGIA JANUARY MWISHONI NADHANI, KUTOKA KWENYE NGUZO NI MITA KAMA 88.KILA NIKIFUATILIA NI KISWAHILI TU.NA SIO MIMI TU HATA JIRANI YANGU NAYE NI LAINI YA SNGLE,MPAKA KESHO. LABDA MSEME LINGINE NIWAELEWE.NIKO NYAMONGO TARIME, 0756847424
 
huko ikonda nililipa kwa tanesco ila nilivyowasumbua sana wakaniambia mradi upo chini ya REA, na REA haina fedha tena mpaka mwaka mpya wa fedha nkachoka.
Basi usiilaumu tanesco. REA ni wakala wa kusambaza umeme vijijini hivyo jaribu kuulizia REA kwanini hawaunganishi umeme
 
Hatumuelewi Meneger wa Tanesco Bagamoyo kuna mitaa ya pale pale Bagamoyo mjini kama Sengerema na Kimara ng'ombe haina umeme almost 10 years now, its too much na imeanza kuwa na nyumba nyingi kwa miaka hyo hyo 10, Cha kushangaza ujenzi wa chuo ulioanza miaka ya hivi karibuni tayari una transfoma lake binafsi. You guys mnafanya kazi kwa masilahi ya walipa kodi au watumia kodi, matukio ya wizi yanazidi kuongezeka maeneo hayo. Na cha kushangaza zaidi maeneo ya mitaa mingine ambayo nyumba ziko more separated ndio yamepata umeme, mjali wananchi jamani huku mikoa mingine tunashuhudia mpaka nyumba za nyasi zina umeme....inakuwaje mitaa ya mjini/wilayani bagamoyo ikose.
 
Kuwa mvumilivu mkuu, utapata umeme soon. Chamuhimu epuka vishoka ambao wanaharibu taswira ya Tanesco kwa kutapeli wateja, usitoe hela yako kwa cash, mpesa au tigo pesa. Malipo yote halali yanafanyika bank na unapata receipt.
 
Mkuu kama mpo wananchi wengi kuanzia 20 basi andikeni barua kuomba mradi maeneo ya kwenyu na surveyor atakuja kupima maradi ili muweze kuletewa umeme huko
 
Unatetea upuuzi?,au wewe Surveyor?..
Ndio na huwa sipendi rushwa, na ndio maana najaribu kuwaelewesha wateja njia sahihi.

Hao wanaopenda rushwa ni vishoka mkuu ila watu tunaojaua kazi zetu na wenye maadili ya kazi hatufanyi hivo
 
Mkuu kama mpo wananchi wengi kuanzia 20 basi andikeni barua kuomba mradi maeneo ya kwenyu na surveyor atakuja kupima maradi ili muweze kuletewa umeme huko
Hapana tunaomba makao makuu wafanye mawasiliano na meneja huyo wa Tanesco Bagamoyo kuhusu kero ya maeneo hayo ya Sengerema na Kimarang'ombe hayo majibu unayotoa mkuu ni majibu rahisi sana kama nilivyotangulia kusema hapo awali maeneo hayo yana nyumba bora zaidi ya 100 ambazo hazina umeme na wenyew walisema barua ya kuomba mradi ni baada ya kufikia watu 50 na sio 20 lakini hivi tunavyoongea kuna nyumba zaidi ya 100 hazina umeme na ni nyumba bora kabisa kama barua nadhani zimeshaandikwa zaidi hata ya 10 labda saizi tuandike tuadress USAID watupe msaada, tunashangaa hata huu umeme wa rea wa vijijini sisi tunakosa.....ni aibu kubwa sana
 
Chamuhimu andikeni barua kwenda kwa meneja wa tanesco pwani ikiwa na list ya wateja wanaotaka umeme mtapata tu
 
huyo anayejibu ni tanesco au kishika.Vishoka ndo wabba mlungula kwa mabs na wanatngnzw na mabs haohao wa tanyesco
 

Asante chaliifrancisco kwa maelezo yako mazuri. Japo sijajua kama unajibu kama miongoni mwa wahusika wa TANESCO au kama mtu mwenye uzoefu na mambo ya Tanesco.

Labda nikuulize swali la ziada, iwapo Mita inarudi Tanesco je nitalazimika kuilipia upya? Au kwa malipo yale ya awali yatatosha kuniwezesha kufungiwa mita hiyo au nyingine mahali pengine baada ya kukamilisha ujazaji wa form unaoonesha eneo langu jipya (mahali ninapotaka ifungwe baada ya kuhama/kuacha eneo/ofisi ya awali).
 
Mimi ni mwananchi wa kawaida tu kama wewe na kweli nina uzoefu na masuala ya Tanesco.

Kuna tabia ya sisi watanzania wengu kutopenda kusoma au kuomba kueleweshwa mambo. Ukifanya application ya maombi ya umeme ile form unayopewa ina maelezo yakutosha na kuna kipengele kinaeleza kuwa "material yote kuanzia kwenye nguzo mpaka kwenyr meter vitabaki kuwa mali ya Tanesco"

Kwanini mali ya Tanesco!?
Jibu: Tanesco wanatoa huduma ya umeme na hawauzi meter wala nguzo wala nyaya, wao wanasambaza huduma ya umeme na wewe unacholipia ni gharama kwaajili ya kupatiwa huduma ya umeme na sio gharama kwaajili yakuuziwa nguzo au meter.

Kwa mantiki hiyo basi kama uli sign ule mkataba ina maana ulisoma na kuridhia yaliyoandikwa na hivyo hupasi kupinga pale utakapoambiwa kuwa huwezi kuhamisha hiyo meter kwakuwa sio mali yako na huko unapoenda kama utahitaji umeme lazima ufanye maombi upya na kulipia gharama kama kawaida.

Kuhusu kupungua kwa gharama ni katika ku upgrade tu kutoka labda single phase kuenda three phase katika nyumba hiyo hiyo. Mfano una meter ya single phase lakini matumizi yako yameongezeka na hiyo haikidhi load uliyonayo basi utafanya maombi ya kuomba umeme na contractor wako atachora mchoro wa wiring na kuonyesha vifaa vilivyopo na total load kisha baada ya taratibu zote ile gharama ya three phase service line itachukuliwa kisha itatolewa ile uliyolipia mwanzo (single phase)

Mfano kama ulilipia 500 kupata single phase na gharama ya three phase ni 2000 basi watafanya 2000-500 na utalipia 1500
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…