Zijue taratibu za kufuata ili kufungiwa umeme na TANESCO

Tanesco mnazingua

Hiku kijichi line imekata umeme Kitaambo toka saa moja kuna line imekata lakini simu za emergency hazipatikani
 
TANESCO inahitaji kuongozwa na mtu aina ya Kimei au Mchechu.

Shirika limekosa visionary leaders wanaenda kwa mazoea tu.
 
embutuambieni kama mgao wa umeme umerudi au la maana hatuwaelewi mlitwambia mgao ni historia
 
Mradi wa usambazaji umeme huku Muliet Arusha unasuasua si kawaida na wananchi wanahitaji umeme Tanesco wanadai hawana vifaa hususani waya.
 
Nasubili kuwekewa umeme Na miezi miwili imeshapita,wanasema kunatatizo la Nguzo,Mimi ni Nguzo moja tu.Nguzo inakuqajw ni tatizo wakati tumelipia.Nipo Tegeta Madale Framingo.
 
Nashukuru kwa maelekezo mazuri, niliyoyasoma humu. Maana nimechukua fomu Mkuranga nikaelekezwa nizikamilishe kisha watapita maeneo yetu.

Lkn imekuwa kimya,na maelekezo humu yananitaka nikabidhi ofisi ya TANESCO ktk eneo langu wao ndiyo watapanga kuja kufanya ukadiriaji Wa malipo.

Kesho narudisha fomu zangu kwa utaratibu huu niliyosoma.
 
Hivi haiwezekani kuwa shirika mbadala na TANESCO maana naona wanajisahau sana
 
Yoooote mliyosema ni uongo. Mbona suala la saveyo kuomba 30000 hamkuliandika ? Mbona Kibaha inachukua siku zaidi ya 120 tangu mtu kulipia hamkulisema ?
Acheni kutuzingua
 
TANESCO inahitaji kuongozwa na mtu aina ya Kimei au Mchechu.

Shirika limekosa visionary leaders wanaenda kwa mazoea tu.
Tanesco ikiendelea kubaki kama ilivyo, hata angekuja rais mkali namna gani, hata ungeweka watendaji wakuu wachapa kazi kiasi gani, bado ufanisi hautapatikana! Tanesco inatakiwa igawanywe na shughuli zingine zibinafisishwe. Mfano Tanesco ya leo inatakiwa kuwa mzalishaji na msafirishaji tu wa umeme. Suala la usambazaji linatakiwa kubinafisishwa kabisa ili kuongeza tija ya kuwapatia watanzania umeme kwa haraka na kwa bei za kiushindani. Naamini kungekuwepo na makampuni binafsi ya kusambaza umeme, malalamiko mengi yasingekuwa ya kuchelewa kufungiwa umeme. Makampuni yangefanya kazi kibiashara zaidi, bei zingekuwa za kiushindani zaidi...huenda zingekuwa chini ya hizi za sasa na huduma ingepatikana kwa haraka sana. Hivyo watanzania wengi sana wangepata huduma ya umeme kwa wakati. Kama kuna wadau wa serikali au wizara husika humu na mambo haya ya umeme, nawashauri waufanyie kazi ushari wangu, utatuletea maendeleo ya haraka sana kwenye sekta ya nishati ya umeme.
 
KWA TANZANIA YA VIWANDA KUSUBIRIA UMEME SIKU 60???????
BADILIKENI
Ndani ya siku 60 za kazi

KAMA MFUMO MPYA WA USAMBAZAJI UNAHITAJIKA KUJEGWA AU MFUMO WA UMEME MKUBWA UNAHITAJIKA KUONGEZWA KWA AJILI YA KIWANDA AU BIASHARA KUBWA (KAMA HAKUNA MFUMO WA KUMUUNGANISHIA MWOMBAJI) (ZAIDI YA MITA 100)

Ndani ya siku 90 za kazi
 
Hahahahaha Mkuranga ni MOTOOOOOO, hatimaye surveyor amepita kwenye himaya yangu na kufanya uchunguzi na kupitisha tayari kwa hatua nyingine.

Nasema MKURANGA MOTOOOOOOOOOOO!
 
Wabunge ebu pelekeni HOJA Bungeni tupate kampuni mbadala ya usambazaji umeme,kitendo cha TANESCO kumonopolise usambazaji inawapa ugumu wa kukidhi matakwa ya wananchi wahitaji kupata umeme,tukipata kampuni kama mbili za ziada hakika wataisoma namba TANESCO.
 
90 % malalamiko...something is really wrong with TANESCO
 
mi tanesco kwakweli mnisamehe, nliomba umeme nikakaa miezi6 naambiwa nguzo hakuna, ikabidi nimpigie kiongozi mmoja wa tanesco hq, asubuhi nikaenda kuulizia naambiwa nguzo hakuna hazijaja, akati natoka geti la tanesco nikapigowa simu na housegirl wangu kuwa mafundi wamekuja kuweka u.eme, kufika pale kwangu wanatukana hovyo tu. kwa simu ilopigwa kutoka juu
 
Tanesco,mimi nahitaji umeme,nguzo zilipoishia ni zaidi ya mita 100 kufika kwangu,nifanyeje ili nipate umeme......nipo Nyamhongoro-Ilemela -Mwanza
 
Mbona mm nimepewa form nirud nazo site watazikaguwa nakurud nazo.
 
Ushauti wako haufuatwi na Tanesco itaendelea kua pasua kichwa. Bora enzi za Filischemi Mramba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…