Tanesco ikiendelea kubaki kama ilivyo, hata angekuja rais mkali namna gani, hata ungeweka watendaji wakuu wachapa kazi kiasi gani, bado ufanisi hautapatikana! Tanesco inatakiwa igawanywe na shughuli zingine zibinafisishwe. Mfano Tanesco ya leo inatakiwa kuwa mzalishaji na msafirishaji tu wa umeme. Suala la usambazaji linatakiwa kubinafisishwa kabisa ili kuongeza tija ya kuwapatia watanzania umeme kwa haraka na kwa bei za kiushindani. Naamini kungekuwepo na makampuni binafsi ya kusambaza umeme, malalamiko mengi yasingekuwa ya kuchelewa kufungiwa umeme. Makampuni yangefanya kazi kibiashara zaidi, bei zingekuwa za kiushindani zaidi...huenda zingekuwa chini ya hizi za sasa na huduma ingepatikana kwa haraka sana. Hivyo watanzania wengi sana wangepata huduma ya umeme kwa wakati. Kama kuna wadau wa serikali au wizara husika humu na mambo haya ya umeme, nawashauri waufanyie kazi ushari wangu, utatuletea maendeleo ya haraka sana kwenye sekta ya nishati ya umeme.