Malyenge
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 6,658
- 3,659
Nakushauri funga ndoa ya dini hata kama una sababu kubwa kiasi gani. Ndoa ya bomani itakusumbua sana muda si mrefu.Ukiona mtu anataka kwenda bomani anasababu zake..na haimaanishi hana dini
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nakushauri funga ndoa ya dini hata kama una sababu kubwa kiasi gani. Ndoa ya bomani itakusumbua sana muda si mrefu.Ukiona mtu anataka kwenda bomani anasababu zake..na haimaanishi hana dini
Itasumbua nn?Nakushauri funga ndoa ya dini hata kama una sababu kubwa kiasi gani. Ndoa ya bomani itakusumbua sana muda si mrefu.
Ndoa ya bomani haina nguvu kama ile ya dini. Zingatia hilo.Itasumbua nn?
Nguvu kwenye nn mkuu?Ndoa ya bomani haina nguvu kama ile ya dini. Zingatia hilo.
Fuata ushauri tu kwa sasa. Ukishaoa tutakwambia kwa undani. Sasa hivi focus yako ielekeze kwenye kufunga ndoa ya kidini. Tafadhali sana zingatia.Nguvu kwenye nn mkuu?
Na kusali muende huko huko bomani Maana hakuna dini watu wanaosali wakiwa dini tofauti. Maana ninavyoelewa ni kuwa watu hufikia kufunga ndoa bomani kwa sababu wanafikia uamuzi wa kila mmoja kuishi na dini yake.Ndugu, kalagabaho kwani Kuna ubaya gani kufunga ndoa bomani? Tatizo nini hasa? Kwani bomani kuna nini? Kwanini uwe na mhemko wa namna hiyo kwa mtu anayehitaji msaada wa kujua jambo analohitaji kujua badala yake unatumia lugha zisizo na staha? Kwani wewe nani hapa duniani usiyehitaji kujuzwa unapokuwa na maswali? Siyo lazima ujibu wewe , kama wewe unakuona bomani kubaya ni wewe, siyo wote wanaokuona bomani ni kubaya! Tuwe na ustaarabu hata Mitandaoni wakati mwingine, msiwakatishe tamaa wanaohitaji misaada humu Mitandaoni.
Hekima inapatikana hata ukikaa kimya. Mjanja unaonekana hata ukikaa kimya, mwenye akili anaonekana hata akikaa kimya!
Siyo kwakuwa umeficha jina lako halisi ndiyo utashindwa kulaanika kwa matendo mabaya hapana! Basi tujibu wenzetu vizuri , tuwasaidie kabla ya sisi kuhitaji huo msaada.
Nakutakia siku njema.
Iko hivi, cheti cha ndoa utakachopata kanisani ni sawa na cheti utakachopata bomani.yakobo11
Niulize pia...vpi ukihitaji kuingia tena kanisani utapata cheti kingine au utafanyaje?
Sawa nmekupata mkuu..so itabd nmwambie faza kwamba tayar nina gamba?Iko hivi, cheti cha ndoa utakachopata kanisani ni sawa na cheti utakachopata bomani.
Maana vile vitabu vyote vinatoka serikalini. Kanisa linakwenda kuomba serikalini kwamba watakuwa wanafungisha ndoa, kwahiyo tofauti ni kwamba wewe utafungia ndoa kanisani na yule mwingine atafungia ndoa yake bomani lakini ndoa zote zinatambulika kiserikali pia.
Jibu , la Kaka Mr.Mtui , ukishafunga ndoa yako bomani unaweza kwenda kuomba kuibariki kanisani na cheti kilekile ulichopewa bomani , maana hicho cheti ni sawa na kile cha kanisani.
Na wakikuombea unabarikiwa vizuri sana tu.
Ha haaaAwamu hii wengi watakimbilia hku
Imani yako inasemaje mkuuMi nadhani humu watu wanatangaza biashara wajameni. Hizo laki na nusu laki tatu simchezo. Fateni imani zenu mfunge ndoa kidini na kuthibitisha tu serikalini. Labda km imani Yako inaruhusu ndoa za bomani.
Taratibu za imani yangu hizifiti kabisa na taratibu za bomani. Tuanzie hapa, kwann ufungie ndoa bomani? Shida ni nini? Kwann usifungie msikitini au kanisani?Imani yako inasemaje mkuu
NdiyoSawa nmekupata mkuu..so itabd nmwambie faza kwamba tayar nina gamba?
Naomba msaada. Mashahidi wanahitajika ile siku ya kupeleka barua za serikali ya mtaa na siku ya kufunga ndoa? Ama watahitajika ile siku ya kufunga ndoa tu? Msaada wa haraka tafadhaliUtaratibu wa kufunga ndoa yenu bomani mnatakiwa muwe na barua ya serikali ya mtaa kwaajili ya kuwatambulisha mnapotoka.
Pia mnatakiwa mlipie ada ya kufungishwa ndoa ya shilingi 50,000/-.
Baada ya kuandikisha, mtasubiria itangazwe kwa muda wa siku 21, na baada ya hapo mtafungishwa ndoa.
Na bomani ndoa inafungwa siku ya jumatatu mpaka ijumaa, mkitaka kufungishwa ndoa siku ya jumamosi au jumapili basi mtalipia shilingi 150,000/-.
Na pia mkitaka kufungishwa ndoa nje na ofisi za serikali yaani pale bomani inawezekana ila mtalipia shilingi 300,000/- , na hayo malipo ni mbali na ile ada ya shilingi 50,000/-.
Kwa kufanya hivyo ndoa yako itakuwa imekamilika na kutambuliwa na jamii na mbinguni pia sasa na neno kwenye kitabu cha Rum 13:1-2 imeandikwa, kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu , kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa MUNGU, na ile iliyopo imeamliwa na MUNGU.
Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la MUNGU, nao washindanao watajipatia hukumu.