Zijue taratibu za ndoa ya bomani

Zijue taratibu za ndoa ya bomani

Wewe tu mkuu maana maisha ni kuchagua na kuchagua ni kupanga. Wengine huwa wanajifungisha wenyewe na wanaita ndoa kwa kuishi pamoja. So hapo we chagua unachopenda kama dini zimewakinahi. ILA swali ni kuwa unapoenda huko bomani je huwakosei viongozi wako wa dini? Iloposemwa kuheshim mamlaka si kufunga ndoa Bali ni kufuata taratibu za kiserekali kama kulipa kodi, kufuata sheria za nchi nk. Hivyo acha kupotosha watu unakosea sana.
 
Ndugu, kalagabaho kwani Kuna ubaya gani kufunga ndoa bomani? Tatizo nini hasa? Kwani bomani kuna nini? Kwanini uwe na mhemko wa namna hiyo kwa mtu anayehitaji msaada wa kujua jambo analohitaji kujua badala yake unatumia lugha zisizo na staha? Kwani wewe nani hapa duniani usiyehitaji kujuzwa unapokuwa na maswali? Siyo lazima ujibu wewe , kama wewe unakuona bomani kubaya ni wewe, siyo wote wanaokuona bomani ni kubaya! Tuwe na ustaarabu hata Mitandaoni wakati mwingine, msiwakatishe tamaa wanaohitaji misaada humu Mitandaoni.
Hekima inapatikana hata ukikaa kimya. Mjanja unaonekana hata ukikaa kimya, mwenye akili anaonekana hata akikaa kimya!
Siyo kwakuwa umeficha jina lako halisi ndiyo utashindwa kulaanika kwa matendo mabaya hapana! Basi tujibu wenzetu vizuri , tuwasaidie kabla ya sisi kuhitaji huo msaada.
Nakutakia siku njema.
Na kusali muende huko huko bomani Maana hakuna dini watu wanaosali wakiwa dini tofauti. Maana ninavyoelewa ni kuwa watu hufikia kufunga ndoa bomani kwa sababu wanafikia uamuzi wa kila mmoja kuishi na dini yake.
 
yakobo11
Niulize pia...vpi ukihitaji kuingia tena kanisani utapata cheti kingine au utafanyaje?
Iko hivi, cheti cha ndoa utakachopata kanisani ni sawa na cheti utakachopata bomani.
Maana vile vitabu vyote vinatoka serikalini. Kanisa linakwenda kuomba serikalini kwamba watakuwa wanafungisha ndoa, kwahiyo tofauti ni kwamba wewe utafungia ndoa kanisani na yule mwingine atafungia ndoa yake bomani lakini ndoa zote zinatambulika kiserikali pia.

Jibu , la Kaka Mr.Mtui , ukishafunga ndoa yako bomani unaweza kwenda kuomba kuibariki kanisani na cheti kilekile ulichopewa bomani , maana hicho cheti ni sawa na kile cha kanisani.
Na wakikuombea unabarikiwa vizuri sana tu.
 
Sawa nmekupata mkuu..so itabd nmwambie faza kwamba tayar nina gamba?
 
Mi nadhani humu watu wanatangaza biashara wajameni. Hizo laki na nusu laki tatu simchezo. Fateni imani zenu mfunge ndoa kidini na kuthibitisha tu serikalini. Labda km imani Yako inaruhusu ndoa za bomani.
 
Imani yako inasemaje mkuu
 
Utaratibu wa kufunga ndoa yenu bomani mnatakiwa muwe na barua ya serikali ya mtaa kwaajili ya kuwatambulisha mnapotoka.

Pia mnatakiwa mlipie ada ya kufungishwa ndoa ya shilingi 50,000/-.
Baada ya kuandikisha, mtasubiria itangazwe kwa muda wa siku 21, na baada ya hapo mtafungishwa ndoa.

Na bomani ndoa inafungwa siku ya jumatatu mpaka ijumaa, mkitaka kufungishwa ndoa siku ya jumamosi au jumapili basi mtalipia shilingi 150,000/-.
Na pia mkitaka kufungishwa ndoa nje na ofisi za serikali yaani pale bomani inawezekana ila mtalipia shilingi 300,000/- , na hayo malipo ni mbali na ile ada ya shilingi 50,000/-.

Kwa kufanya hivyo ndoa yako itakuwa imekamilika na kutambuliwa na jamii na mbinguni pia sasa na neno kwenye kitabu cha Rum 13:1-2 imeandikwa, kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu , kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa MUNGU, na ile iliyopo imeamliwa na MUNGU.

Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la MUNGU, nao washindanao watajipatia hukumu.
Naomba msaada. Mashahidi wanahitajika ile siku ya kupeleka barua za serikali ya mtaa na siku ya kufunga ndoa? Ama watahitajika ile siku ya kufunga ndoa tu? Msaada wa haraka tafadhali
 
Back
Top Bottom