Koo za simba haziwi kubwa sana bali zinaungana kuzifanya kubwa lakini zinazohusiana moja kwa moja ni za watu kidogo sana.
Mfano mimi nipo kwenye koo moja ya simba tuna jamii yetu ambayo haizidi watu 50, hao hamsini ni wa koo tofauti za simba na marafiki wa simba wazilizoungana.
Na wengine kwengine wapo hivyohivyo. Simba mmoja anaweza kua kaungana na koo zaidi ya moja, huyo anakua kiunganishi cha hizo koo, aidha za hapa Tanzania au za Tanzania na za nje.
Koo kuungana kikamilifu ni mpaka wakuu wa koo wajamiiane na wakuu wa koo nyingine.
Idhini ya wengine kujamiiana na koo nyingine kwa wasio na cheo (rank) kwenye koo ni lazima itoke kwa wenye cheo.
Wenye vyeo kwenye koo ni wanawake wawili wakuu, mkuu na ataemchagua kua ni msaidizi wake. Ni lazima mkuu wa koo awe ameolewa na simba mwenye hadhi, hawezi kuolewa kama huyo mume hajaidhinishwa kwake na koo yake na koo yao.
Koo mbili tofauti za simba hazitaungana kama wakubwa wakoo hatajamiiana, zitaheshimiana lakini mambo ya ushirika kimali na kikoo yatakua kila koo kivyake hata kama wanajuana. Sema watasaidiana kwenye tatizo, kulitatua tatizo.
Koo moja ya simba ya Tanzania inaweza kua na uhusiano na koo nyingine ya nje ya Tanzania kwa wakuu wao kujamiian, japo mara moja tu katika maisha yao.