Zile kelele za Chato kuwa mkoa zimekomea wapi?

Umenikumbusha kipindi Cha mwendakuzimu kila ukifungua TBC unakutana na kipindi kinaitwa KISHINDO CHA AWAMU YA TANO. Mtangazaji alikua na mihemko kwa kuufukuzia ukuu wa wilaya.
Yule jamaa sijui hata anaitwa Nani.

Ila hii nchi imepitia upuuzi mwingi sana, kuna muda tulilazimishwa kuangalia TBC kwa lazima, station nyingine zote zikatolewa DSTV ikaachwa TBC, ili wote tuiangalie. TBC yenyewe sasa....
 
Hivi mtaacha lini ujinga nyinyi. baada ya kuongea mambo ya maana kama kubambikiwa matozo mnaleta mada za kimbea. sasa chato iwe mkoa au wilaya itakusaidia nini. hii nchi kuiongoza rahisi sana sababu wajinga ni wengi mno.
Chato kuwa mkoa au la Kuna impact kiuchumi, kijamii na kisasa. Hakuna kosa kkuzungumzia Hilo labda namna ya kulizungumzia tu.
Ukisema tz ni ya wajinga, na X ni m tz pia X atakuwa mjinga..
 
Magufuli mwenyewe alikuwa anawatania tu,halaf alipofariki wakakomalia hili swala la mkoa, nadhani Chato kuwa mkoa bado sana. Mkoa wenyewe wa Geita ni mdogo sana wenye wilaya za Chato, Geita mji, Geita vijijini, Nyang'hwale na Mbogwe. Ni wilaya sita na siyo populated sana. Kama Rais anawapenda sana awapelekee maendeleo na siyo Zawadi ya mkoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…