Zilikuwa nyakati za Chico, Nat King Cole, Dean Martin, Sammy Davis Jr, Sidney Poitier..Ukipenda Sal

Alama, Mohamed Said, uliowataja karibia wote ni kaka zangu wa Kariakoo. Nnalia.

Dah! Ulipomtaja Salum Hiriz, nikamkumbuka na Ali Bobo.

Henin ananikumbusha enzi za Lumumba ilivyokuwa Lumumba haswa.

Mrisho Wanted unanikumbuka siku zake za mwisho akija nyumbani kuchukuwa kanzu zake za KUSWALIA, special kwa ajili yake zilizotoka Dubai kwa Jamil, Dennis Law.

Mohamed Saiwad (Chico) Allah amrehemu aturehemu nasi tulio hai. Amiiiin.
 
Pohamba,
Usitokwe na machozi bali shukuru kuwa Allah katoweka kiasi hiki
kwani wenzetu wengi wameshatangulia.

Tamim ni rafiki yangu wa miaka mingi sana.
Nikipata picha za zamani nitakuwekea hapa.

Ma sha Allah, juzi juzi Anko Tamim alikuwa akinipa kisa chenu na Henin na Black American mmoja aliyekuja 70s na kuponda ponda watu.

Nadhani utakikumbuka.
 
Chico hajatumikia nchi kwa uadilifu mkubwa.
 
Taazia pelekeni nyumbani mkawadanganye ndugu zake. Tulio ishi na Chico hamuwezi kutuletea bandiko hili tukaacha kusema ukweli.


Semeni ukweli kwa kufungulia uzi wake, tutakuja kujibu.

Hapa ni taazia.
 
Taazia pelekeni nyumbani mkawadanganye ndugu zake. Tulio ishi na Chico hamuwezi kutuletea bandiko hili tukaacha kusema ukweli.
Jigsaw,
Huenda kuna baadhi ya ada zetu huzielewi na ndiyo maana umekuja na
maneno haya.

Mtu anapofariki inapendeza watu wakazungumza yale mema yake kwani
wapo nduguze walio hai hawatafurahi kusikia maiti yao inakashfiwa na hili
si jambo linalohitaji fikra sana.

Pili marehemu hayupo kujitetea ukiwa unamsema vibaya inakuwa kama vile
unamuonea.

Hakuna binadamu aliyekamilika kila mtu anazo kasoro na huu ndiyo hakika
ubinadamu wenyewe.

Ikiwa Chico alikuwa na ubaya wake basi na tumsamehe na tumuombe Allah
pia amsamehe kwani mwenzetu keshatangulia mbele ya haki.
 
Maalim Faiza,
Moja katika dua nizipendazo kuomba ni Allah kuniweka mbali na huzuni.

Nami nakuombea kwa Allah asitie moya wako huzuni kiasi ukabubujikwa
na machozi.

Hakika haya mie moyo huingia simanzi nikizikumbuka siku zile.
Haziwezi kuondoka katika fikra zetu maana zinatukumbusha mengi.

Ali Bobo na Abdallah Awadh nani asiyewajua Dar es Salaam.

Watu waungwana waliojishusha kuwa katika kila shughuli wao hujitolea
kuwaandalia watu chakula kwa ustadi mkubwa sana.

Salum Hiriz aka Sammy Davis Jr. ''gifted singer,'' akiimba kati ya nyimbo
nizipendazo, ''Summer Time.''

Jamil Hizam aka Denis Law, ''brilliant striker with Cosmopolitan.''

Sahib yangu tukifanyakazi pamoja East African Cargo Handling Serices
(EACHS).


Mrisho aka Wanted...
Mtu mkakamavu na mpirani ni mlinzi asiyechoka na mpiganaji wa kutumainiwa.

Mrisho alichukua, ''nickname,'' yake kutoka hiyo movie hapo juu 1966.

Wote hawa ni jamaa zetu na kwa pamoja tumeandika historia ya vijana wa
Kariakoo.
 
Ma sha Allah, juzi juzi Anko Tamim
alikuwa akinipa kisa chenu na Henin na Black American mmoja aliyekuja 70s na kuponda ponda watu.

Nadhani utakikumbuka.
Maalim Faiza,
Tamim
ni, ''super intelligent,'' asikuambie mtu.

Hebu soma haya maneno niliyoandika kuhusu Tamim kama, ''dedication,''
katika kitabu cha Sykes:
''Lastly I wish to pay special tribute to my friend Faraj Abdallah Tamim
whose thoughts and ideas are entangled with mine in this work.

I can only distinguish his thoughts from mine in Tamim’s gift of eloquence
and flow of words which appear in the work as well as in those references
attributed to me verbatim.''
 

Hahahaha, ipo hiyo katika ukoo, labda mimi ndiye niliyemrithi ammi yangu.
 
Hahahaha, ipo hiyo katika ukoo, labda mimi ndiye niliyemrithi ammi yangu.
Maalim Faiza,
Hilo nalikubali kabisa.

Tumekaa mimi, Tamim, Hamza Njozi na Prof. Mazrui Kampala Nile Hilton.
Tulikuwa kwenye mkutano na wenyeji wetu wametuweka hapo.

Tamim akawa anavipitia vitabu vya Prof. Mazrui moja baada ya kingine taratibu.
Prof. ''all ears,'' anamsikiza kwa makini.

Tamim akaingia katika kitabu cha Prof. ''The Trial of Christopher Okigbo.''
Prof. akamuuliza, ''Umependa nini katika kitabui kile?''

Bila kupepesa jicho Tamim akamwambia Ali Mazrui, ''They come at midnight...''
Prof. Mazrui alicheka.


Kushoto: Tamim Faraj, Prof. Ali Mazrui na Mwandishi Kampala 2003
 

Hahahaha, ipo hiyo katika ukoo, labda mimi ndiye niliyemrithi ammi yangu.

 
Nilipoona umeandika nikaenda mbio kusoma, pamoja na urefu wa ile taanzia nimeimaliza kuisoma,kaka hongera kwa kuifanyia kazi elimu yako kisawasawa,Mungu akufanyie wepesi uandike zaidi kwani ni wazi unayoyajua si haba. R .I. P Kamanda Chiko
 
Ma sha Allah, juzi juzi Anko Tamim alikuwa akinipa kisa chenu na Henin na Black American mmoja aliyekuja 70s na kuponda ponda watu.

Nadhani utakikumbuka.

Ohhh 1970's Itabidi nimuulize Tamim hiyo
 

Tamim machine nyingine kabisaaa mkuu

Kwanza tazama his prodigious volume of scholarship. Najua haha publish vitabu vine kama akina Njozi et al. Lakini I know he has published hundreds of essay and commentaries kwa bahai mbaya sina hakika kama alifanya film documentaries but he could be a valuable contributor na naamini ana so much secondary and primary resources. Miaka hiyo nilikuwa naenda naye maeneo mbali mbali alipokuwa anaenda kufanya public lectures na and its very difficult not to see the the range, probity as well as impact of his intellectual analyses, interventions, and debates ambazo in my humble opinion were short of nothing but extraordinary. Kwa bahai mbaya hakuna vijana ambao wamefuata nyayo zake kama yeye ninaowafaham zama hizi. Mimi hunikumbusha RK Dau by the way Dr anavyoweza ku move seamlessly between the kwa Klabuni hapo Pan na akina Captain Malik to classroom then to conference circuit, kwenye sports, and corporate boardroom, to the corridors of political power. As for Tamim ni mtu ambaye he often relishes intellectual debate and combat because he believed in the power of ideas na hasa ideas beyond haya mambo yetu ya kawaida. Nakumbuka articles zake Benzi za Africa events alivyokuwa akiwavuruga akina Ahmed Rajab and Co. Binafsi nakumbuka alinipa moja ya first copies za mwanzo za kitabu cha Partnership na vitabu vinginevyo na linguine nilikuwa naazima na soirudishi of course na ninavyo mpaka leo. In my opinion ni mtu aliyeamua ku dedicate his life kuendeleza watu na kwa bahati mbaya sana imekuwa kama case ya Mfalme asiyetambulika kwao. Muhim Allah SW anatambua mchango wake.


The man has a beautiful mind he could have been in the ranks za akina sheikh anta drop, Ivan Van sertima, Molefi Kente Asante, Horace Campbell na wengineo. Itabidi Maalim Mohammed Said tumfungulie Uzi wake
 
Amazing story well narrated.....
 
Sal Davis nilibahatika kumsikia miaka ya 90s hap0 Euro Pub,nafkiri akiwa karejea toka Ulaya,kwakweli alikua na kipaji cha pekee,alifanya ninze kufatilia jazz kwa karibu.kwa akili yangu nikijua ni mmarekani Mweusi anayeishi TZ.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…