Maalim Faiza,
Nilimheshimu Tamim katika mgogoro wa Zanzibar kuingia katika
Organisation of Islamic Conference (OIC) mwaka wa 1993.
Rais Ali Hassan Mwinyi na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje
Hassan
Diria walikuwa katika wakati mgumu sana.
Kanisa lilisimama vikali kupinga, magazeti yote yalikuwa yanashambulia
ili muradi Zanzibar ilikuwa mashakani pamoja na
Rais Mwinyi na
Waziri
Diria.
BAKWATA haikuwa na watu ambao wangeliweza hata kwa mbali kusaidia.
''Enter the Dragon...''
Tamim kila tukikaa kutafakari hali ya nchi yetu anaeleza masikitiko yake
jinsi vyombo vya habari pamoja na magazeti ya CCM na serikali yalivyokosa
adabu kiasi hata cha kumshambulia MwenyeikitI wa CCM
Rais Mwinyi.
Kila tukikaa hatuna mazungumzo ila hayo.
Nikikutananae namkuta mwenzangu kesha soma magazeti yote ya siku hadi
''gutter press,'' ananipa ''briefing.''
Ghafla likatokea jambo limezuka vuuu!
Wakati ukifika In Shaa Allah nitalieleza hili la kuzuka.
Ndipo
Tamim akaja na kitabu kutoka Nigeria, ''The Two Headed Dragon,''
kitabu kilichokuwa kinaelezea fitna yote ya OIC.
Tamim anakonda panapokuwa hakuna kitu cha kuhangaisha bongo lake
na ananenepa katika, ''crisis.''
''Hawa tunawafungulia front mbili za mapambano tupime ubavu wao.
Tunabisha hodi huko huko kwenye kichaka chao...kisha tunawaleta huku
kwetu wapambane na askari wenda kwa miguu chakula chao biskuti za
chumvi na maji.''
Tamim huyo anakuja na ''strategy,'' ya mapambano.
Bunge lilipigwa na mshangao na barua walizokuwa wanapokea kuhusu
tatizo la Zanzibar kujiunga na OIC kiasi iliulizwa hawa ni akina nani wenye
kalamu kama hii?
Ghafla hali ya hewa Dar es Salaam ikabadilika na
Rais Mwinyi akawa kapata
utetezi na watetezi.
Waliokuwa wanamshambulia
Rais Mwinyi wakaingiwa na hofu.
Hawakuwa na uwezo wa kufungua, ''front,'' ya pili kuja kulikabili jeshi la,
''infantry.''
Lugha yao ikaanza kubadilika kulikuwa na maneno ya, ''impeachment.''
Msamiati huu ukatoweka ikawa sasa wanasema,
''Baba wa Taifa asaidie.''
''The eagle has landed...''
Ingia hapo chini usome ilikuwaje:
Mohamed Said: Zanzibar Membership to Organisation of Islamic Conference (OIC) and Islam in Africa Organisation (IAO)