ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Zile ndo zilikuwa nyimbo si hizi za computer kisha tunalazimishwa kusikiliza na kuzibatiza kuwa ni zetu.

Mpaka leo na kesho hizi zitabaki nyimbo bora. Nenda sehemu wanakopiga copy ya hizi nyimbo ndiyo utajua jinsi watu wanavyozizimia.
 
Bitchuka rehani ameimba sana kwenye huu wimbo.
Kisha Maalim Ghurumo anakuja mpokea...dah those days

Bitchuka sauti noma, kuna ule wimbo wa mlimani park km sikosei unaitwa njia ya kwetu, pale anapoimba wengine humwita shemeji ooh, madhara yake ni makubwa ooh! Duh ile stereo yake ni balaa
 
Mpaka leo na kesho hizi zitabaki nyimbo bora. Nenda sehemu wanakopiga copy ya hizi nyimbo ndiyo utajua jinsi watu wanavyozizimia.

Mnoo! Kuna nyimbo zilirekodiwa ziko stereo mpaka leo ukisikiliza kila chombo unakisikia. Kuna nyimbo za makassy orch wakati wa mosesengo Molema na mosese, Matimila na dr remmy mume wangu, RTD walijitahidi sana. Nimeachana mume wangu nimekwendani kwa rehani ooh baada ya muda si mrefu kasema niondoke sina tabia nzuri ooh!
 
Msaada wenu wana jf msaada wa rekodi ya nyimbo hizi za zilipendwa online 1. DALILI-MSONDO NGOMA 2. CHEUSI MAGALA NO.1-OTTU JAZZ 3. MALARIA-MSONDO NGOMA 4. NIPELEKE KWA BABA NO.2-OTTU JAZZ 5. SI WAZURI BINADAMU-MLIMANI PARK ORCHESTRA Kama kuna mdau ataweza kuniaploadia online au anafahamu link ambayo nitaweza kuzipata nyimbo hizi, nitashukuru sana

si wazuri binadamu ni wa Ochestra Safari Sound wakati bichuka na Gurumo walipohamia huko na mtindo wa Ndekule
 
huo naujua unaitwa Noel hata Youtube uko. nnaouzungumzia kuna maneno kabsa yanasea tukacheze kamanyola na marquis ooh christmas oyee

Kuna nyimbo mbili hapa. mmoja ni Christmas Bonane wa Maquis na Noele Bonane wa OSS.
Zote zimetungwa na kuimbwa na king kiki kwa nyakati tofauti.
 
Mnoo! Kuna nyimbo zilirekodiwa ziko stereo mpaka leo ukisikiliza kila chombo unakisikia. Kuna nyimbo za makassy orch wakati wa mosesengo Molema na mosese, Matimila na dr remmy mume wangu, RTD walijitahidi sana. Nimeachana mume wangu nimekwendani kwa rehani ooh baada ya muda si mrefu kasema niondoke sina tabia nzuri ooh!

Hiyo nyimbo ''homa imenizidia mie ooh'' Bitchuka anajiimba mwenyewe baada ya Kuachana na mume wake Sikinde na kwenda kwa Rehani ambaye ni Hugo Kisima aliekuwa mmiliki wa OSS...

Baada ya hapo Sikinde wakamjibu na ''mtoto akililia wembe''
Mtoto akililia wembe wacha umkate, atapopata kidonda ndipo atapouogopa, dada yetu weewe ulikwisha olewa, lakini kwa tamaa yako ulikubali kuacha watoto wako, kwenda kuishi na bwana mwingine eeh hodari sana wa kuoa na kuacha...

Usilie eeeh eeeh unalia nini nawe ulisema, umempata bwana ataekufaa maishani mwaako aloo Dada, aloo sister.
Sisi tulijuwa nyumba hiyo ni chambo tu, sio kwako peke yako Dada eeheee hata hao walioolewa kabla yako wakaachika, tunawaona mitaani kila siku ''akina Kasheba hao'' tunapanda nao uda na daladala eeh hakuna magari wala viwanja walivyoambulia, pole Dada umeyataka mwenyewee eeeeeh
 
Mpaka leo na kesho hizi zitabaki nyimbo bora. Nenda sehemu wanakopiga copy ya hizi nyimbo ndiyo utajua jinsi watu wanavyozizimia.

Miaka mitatu iliyopita nilikuwa London, bahati nzuri kukawa na pati ya watanzania wiki niliyofika kule. Kwenda kwenye pati nyimbo ambazo zilitia fora ni za muziki wetu wa dansi na hizi za taarab za kina Issa Matona na Bi. Shakira pamoja na hizi za sasa. Watu walicheza hakuna mfano, wakiweka bongo fleva ni wachache tu ndo wanabakia kucheza mpaka Dj anatoa na kupiga nyimbo watu wazipendazo na umati unarudi tena ukumbini kucheza. Original ni original tu, hizi za kucopy na kupaste hazina radha hata.
 
Hizi nyimbo na mie Mhhhhh! lakini siku za karibuni nimeanza kusikia chache ambazo zinanigusagusa.

Miaka mitatu iliyopita nilikuwa London, bahati nzuri kukawa na pati ya watanzania wiki niliyofika kule. Kwenda kwenye pati nyimbo ambazo zilitia fora ni za muziki wetu wa dansi na hizi za taarab za kina Issa Matona na Bi. Shakira pamoja na hizi za sasa. Watu walicheza hakuna mfano, wakiweka bongo fleva ni wachache tu ndo wanabakia kucheza mpaka Dj anatoa na kupiga nyimbo watu wazipendazo na umati unarudi tena ukumbini kucheza. Original ni original tu, hizi za kucopy na kupaste hazina radha hata.
 
Last edited by a moderator:
[video=youtube_share;ZyeMisKRpdE]http://youtu.be/ZyeMisKRpdE[/video]

[video=youtube_share;UsfXcyuquhA]http://youtu.be/UsfXcyuquhA[/video]

[video=youtube_share;UsfXcyuquhA]http://youtu.be/UsfXcyuquhA[/video]

Jerry Nashoni, Max Bushoke, Muhidin Gurumo, Hassan Rehani Bichuka, Niko Zingekala- hizi ni sauti chache tu ambazo kwa kweli nikiziskia popote pale iwe leo au kesho roho yangu inafarijika. But I do believe tukiongelea zilipendwa Mbaraka Mwinshehe na Marijani Rajabu wao wako kwenye level tofauti kabisa na mtu mwingine yeyote, these are the gods of zilipendwa.
 
Thanx all for you contribution nimejifunza vingi sana hapa
 
Pouwa sana! ila hii ni cheusi magala no. 2, Nilikua naitafuta ile cheusi magala no.1 ambayo kwenye sauti ya stereo pale ameimba bichuka, ila hii cheusi magala no.2 kwenye sauti ya stereo pale kaimba marehemu othman momba
 
Last edited by a moderator:
Hizo nyimbo zote na nyingine nyiiingi mimi ninazo ila nauza.
Una pakee mfukoni ni PM ili nikuite sehemu na kukuchomea kwenye CD...
Napatikana Dar kwa sasa, lakini mwezi ujao ntakwenda home Baidoa.

Mshenzi mkubwa wee, nyinyi ndio mnaoua wenzenu kwa wizi wenu. Unaziuza umeziimba wewe?

Na wewe unayetafuta nyimbo, nenda dukani. Hizo nyimbo sio ZILIPENDWA, bado zipo madukani.

Zilipendwa ni enzi hizo za kina Muba, Salum Abdallah, Daudi Kabaka na wakongwe wengine.

Quban Marimba, Tabora Jazz, Moro Jazz, Mwenge Jazz n.k

Nakuacha na kipande hii moja ya Muba.....Dr. Kleruu

''Oooh Dr. Kleruuu, ukalale pema kiongozi wetu shujaa.......''
''Mwanamapinduzi, kalale pema kyongozi weetu shujaa...
Kifo chake dokta, kimetusikitisha sisi wakulima wote woye......

Bumpkin nitake radhi...
Umenitusi kwa kuniita mshenzi.
Unanilaumu kwa kuuza nyimbo ambazo sijaziimba, mbona wewe unauza masabuli hayo...je uliyaumba?
 
Bumpkin nitake radhi...
Umenitusi kwa kuniita mshenzi.
Unanilaumu kwa kuuza nyimbo ambazo sijaziimba, mbona wewe unauza masabuli hayo...je uliyaumba?

Te te te te teeh. Ukiwa na stress we log in jf kama zisipoisha basi zitapungua sana. Mnakikumbuka kitu Jackie cha Zengekala? "Sauti yako nyororo inaniua saana na mwendo wako wa maringo unanikondesha mamaa haa aiyolelii mwanamamayee nakuwinda saana Jackie ye ye ye mwana mama iyaee". "Mvumilivu ula mbivu Jack yeye x2 jaribu kuvumilia yee tutaonana mama aah kama sio Kampala yee ni Tanzania mamaa Jack yeye mwana mama iyaee
 
Msaada wenu wana jf msaada wa rekodi ya nyimbo hizi za zilipendwa online 1. DALILI-MSONDO NGOMA 2. CHEUSI MAGALA NO.1-OTTU JAZZ 3. MALARIA-MSONDO NGOMA 4. NIPELEKE KWA BABA NO.2-OTTU JAZZ 5. SI WAZURI BINADAMU-MLIMANI PARK ORCHESTRA Kama kuna mdau ataweza kuniaploadia online au anafahamu link ambayo nitaweza kuzipata nyimbo hizi, nitashukuru sana

Mkuu SI WAZURI BINADAMU imeimbwa na BICHUKA lakini akiwa na OSS sio MLIMANI PARK. "Ninakushukuru Mungu huso mshirikae kuiponya roho yangu ilotaka toweka binadamu madhurumu ana vituko vya sumu anavituko vya sumu kali kushinda ya nyokae si wazuri binadamu usione wachekaa ooh nhon."
 
Back
Top Bottom