ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

kuna wimbo mwingine unaimbwa; watoto wamekuja juuuuuuuuu, wanataka nyumba (mali) yaooooo
 
kuna wimbo mwingine unaimbwa; watoto wamekuja juuuuuuuuu, wanataka nyumba (mali) yaooooo
Huu Wimbo mbona upo humu Chifu?, angalia post namba 240...

 
Mkuu Balantanda heshima kwako jinsi ulivotukumbusha mbali sana. Infact mm mpaka sasa ni mdau wa muziki huu wa Vijana wa Zamani na ninaburudishwa sana na kuguswa na hisia nisikiapo muziki huu.

Naombeni mnisaidie kujua huu wimbo unaoitwa "
Joyce" umeimbwa na nani na bend gani na Je! nawezaje kuupata maana niliinao umeishia nusu, wakati nnaupenda mnooo...

Wimbo wenyewe unaimba hv...

">Ondoa mawazo yako nimekwishakusamehe
Mimi nakukanya Joyce usirudie tena
uliyoyafanya zamani ni mabaya sana
sasa yamekwisha Joyce usitende tena< "

rudia tena

-Unavoendelea ndio cjui saidieni wadau
 

hao walikua atomic jazz toka mkoani Tanga
 
"Ndugu na jamaa wameniweka kando kuwa hunifai ooo!" BAADHI YA MANENO KATIKA WIMBO WA AIJA ULIOPIGWA NA DDC MLIMANI PARK,WANA SIKINDE NGOMA YA UKAE,MWAKA 1984.
 
Wadau mwenye wimbo wa Siwema no.2 au maarufu SADIKI wa Dar International atupie link hapa, naukubari sana ule wimbo kuliko namba moja yake maana una mazingatio makubwa kwa dada zetu wanaodanganywa na kioo na pia kwetu wababa tunaosikiliza maneno ya upande mmoja na kukurupuka kwa maamuzi magumu.
 

Jana hayati tx moshi william alitimiza miaka 8 tokea afariki,(R.I.P),embu tujikumbushe enzi zake za muziki huyu msanii nguli
 
Mimi nitafurahi zaidi kama nitapata mtu atakeyenipa "title" za nyimbo ambazo ziliimbwa na bendi zetu miaka hiyo ya themanini na tisini, yaani zile zilizoimbwa kwa lugha za asili za makabila yetu. Nimezitafuta sana lakini nimshindwa kuzipata.
 
Mimi nitafurahi zaidi kama nitapata mtu atakeyenipa "title" za nyimbo ambazo ziliimbwa na bendi zetu miaka hiyo ya themanini na tisini, yaani zile zilizoimbwa kwa lugha za asili za makabila yetu. Nimezitafuta sana lakini nimshindwa kuzipata.

Tulele tubone 'UDAJazz' Malaine, Mizimu ya pambamoto 'Vijana jazz' Shakaza I n II ' Washirika n Bima lee' Kila munu avena kwao 'Makondeko' hizo nilizofanikiwa kukumbuka.
 
Sikinde - ubaya...

Mambo unayoyafanya huko ulikoo nimeshasikia...

nimefahamu lengo lako nieleze tunachogombania...

kama ni kipato chatokanaa na ujuzi wangu...
 
Wadau hatujamtendea haki Maalim Gurumo kwa kutotupia tanzia yake kwenye huu uzi, Allahu maghfirahum waskana hum fii jannah.

Naikumbuka sana sauti yake kwenye beti zifuatazo.

'Wewe ni mdogo kwangu bado chini hujakaa unataka kufanya hira unaodha kuongozaa'

'Natoa honyo kwa yeyote anaechezea chatu ni hatari atakuja asipate lolote la manufaa na ajali imkute bila ya kutegemeaa atakuja adhirika ajute na duniaa'

'ukiwa ulionipata mkubwa baada ya kufariki wazazi wangu alinichukua mjomba kaka yake mama yanguee amenilea hadi nimekua na akanisomesha mpaka nimemaliza ananifanyia mipango zaidi nami niishi vizuri'

'unapotoka kazini unahamia kwenye bar unapokaribishwa kiti unaagiza lete kama tulivyoo'

'wakati wa ujana wangu mimi baba yenuu shati dukani shilingi sita unapata kwa hivi sasa shilingi sita hata mkate hupati'

'mwanaume unapopatwa na matatizoo macho uwa mekundu kwa hasira lakini katukatu usikate tamaa'

'kijana nakusihi usipende kulewa hovyooee na akina dada hao jihepushe nao wanakupapatikia kwa sababu una pesa ee pesa zikikuishiaa watakukimbiaa'

'kazi yangu isiwe sababu au kisingizioo kuwa hilo gari si tax bali la kubeba vimadaa'

na nyingine nyingi sanaaaa apumzishwe alipojiandalia. Aamin
 
Kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Filauni, sasa huyu MWEHU wa kiponjoro katokea wapi kuja kujaza ushuzi kwenye uzi wenye heshima zake kama huu?

Ngoja nikamuitie kiboko yake wamfulumushe na mawe uchizi wake apeleke milembe huko sio humu.
cc Balantanda
cc Shifta
cc Mzizi mkavu et al.
 

Lazima uliachiwa radhi ndio maana umeishia kuwa mkorofi.... na ovyo ovyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…