Kuna kitu kinaitwa, "Kisa cha foto albam"
Kisa ni picha iliyopigwa zamani eeh katikati ya Dar es alaam eeh
Kisa ni picha iliyopigwa zamani ee
Katikati ya mji wa mwanza ee
Sheli Zinuna nakupa pole Zinuna ee.
2. Kupatwa kwa mwezi sio kiama- mwenge jazz.
3. Kata ya maji ukweni- sinahakika na bend ila nadhini bima Lee, muimba Maxmilian Bushoke.
Makumbele- maguezi du Zaire
Kaweke zege mbinguni- Bima lee
5. Ayoyo mie- Sammangwana.
6. Machawi na mulozi- Rwambo Mackiady & Sammangwana.
Ukatiri, ndoa ya mateso, namsaka mbaya wangu- Marjani Rajabu.
7. Tucheze ngoma za kwetu, masafa marefu, mapenzi gani haya, Mama- Tancurt Almas.
Nyabasi, Nimesimama kwenye kona, Asha mwana Seph, Huwezi kula muwa bila kukuta vundo, kulithi ndoa ya kaka- Juwata.
Nishike mkono, kibela acha chuki, sema ukweli wako- Mk group.
Nyimbo ziko nyingi. Ila leo niishie hapa, zamani watu walikula uhondo sana. Kipindi hicho nilikua napenda kufuatilia mziki sana ila uwezo wa kupata pesa ya kiingilio sikuwa nao nilijiunga nawenzangu kuchenza nje ya ukumbi, mpaka fungulia mbwa ndopo tunaingia ndani. Pale 82 hoteli sasa hivi San siro, pamoja bend zingine kupiga pale, ulikuwa ukumbi wa nyumbani wa washirika Tanzania stars. UFI Clabu, ulikuwa ukumbi wa nyumbani wa Bima Lee, Lion Hoteli, ulikua ukumbi wa nyumbani wa Mk beets, bend ndugu na MK group, watoto wa magorofani ukumbi wa nyumbani ni Africa hotel ghorofa la saba.
Sikinde wakati wanaitwa mrimani park, ukumbi wa nyumbani ulikua kule mlimani chuo kikuu, baada ya kumilikiwa na shirika la maendelea Dar es allam wakaitwa DDC mlimani park ukumbi wa nyumani ikawa DDC Kariakoo. JUWATA ukumbi wa nyumbani ulikua CCM Mwimjuma Mwananyala, ulikua unanunua gazeti la mfanyakazi unapata ratiba za bend, sinema kulikua na kumbi nane za sinema Dar. Ila kwenye mziki ukisikia saxs phone zikipigwa chama chetu za mapinduzi cha jenga nchi, jua mziki umefungwa. Ila kwa haya niliyoaandika kama kuna mwenye kumbukumbu sahihi anaweza weka sawa.