ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

R.I.P Harila Yusufu Tongolanga(Tongolanga means,Ongea tu,muongee,endeleeni kuongea nk)

Kila Munu Avena Kwao ile ya Mwanzo ilikua tamu. Kadri ya Awam za Remix ilivyoongezeka ndivyo utamu ulivyopungua.
Namkumbuka kwa wimbo wake mwingine-Saidaru
 
Kuna wimbo mmoja wa Vijana Jazz,nilikua ninaupenda sana,wimbo ukiitwa Mume acha Visa. Kwa hakika nikiweka top ten za Vijana Jazz nitaanza na hivi:
1. Kapu la Mjanja
2. Top Queen
3. Shoga
4. Ogopa Tapeli
5. Shingo Feni
6. V.I.P
7.Mwisho wa Mwezi
8. Wifi
9. Janja ya nyani
10. Bye Bye Umaskini(Tafrija la kuuaga Umaskini)
More Dedications:-
11. Thereza
12. Visa Vya Mume(Nikipika Ugali unasema unamabuja,sema. kinachokukera mumeeee)
13.Ngapulila
14. Mbuzi yake kamba
15. Penzi haligawanyiki!

"KAPU LA MJANJA"

Ndege wa rangi moja huruka pamojaaaa eeeeh,uliona wapi Bundi kwenye kundi la Njiwaaaeeeh, wamekususa wamekusuaseeee visa si visaaaa........

Kwa kweli ilikua raha sana,years have passed,we can not reverse. Ndo hivyo kwa kweli hata sijui nisemeje kwa karaha ya sasa ambapo hakuna muziki bali ni kelele na kuonyesha picha za magari ya kifahari(fake life)nyumba za kifahari na artificial ladies.
 
naomba milima ya kwetu tafadhali
 
Mkuu leo nimepita huko nikaondoka na wimbo wa MASUDI ulioimbwa na mbaraka mwinshehe. Nimefurahi sana na email yangu nimeiacha huko.
 
Maombi ya kutaka turudiane nimesikia unalalamikaaa. maisha kuishi na wanangu etii huyawezi.kurudiana na wewe siweez , nimeoa mke mwingine ninaishi naye.
Naitafuta hiyo nyimbo mkuu.
Pia penzi kizungumkuti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…