ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Copyright vipi lakini? Tusije fungwa mpakiaji na mpakuaji ahhh.
 
Mwenye "MWAKA WA TABU" wa Ally Choki tafadhali naomba ani PM tafadhali.
 
Wakuu nnaomba mwenye nyimbo hizi tafadhari;
1. kisa cha mpemba,,,,,twanga pepeta
2. siri,,,,deo mwanambilimbi ft banana zoro
3. Abuu Misambano na TOT Band,,,inaimbwa hivi"ooooh bwanaeee usilie na mimi babaaaa, mpenzi wako mimi sijamwita eeeh, kaona mambo ww huyawezii, ndipo kaja kwangu"
 
Wakuu nnaomba mwenye nyimbo hizi tafadhari;
1. kisa cha mpemba,,,,,twanga pepeta
2. siri,,,,deo mwanambilimbi ft banana zoro
3. Abuu Misambano na TOT Band,,,inaimbwa hivi"ooooh bwanaeee usilie na mimi babaaaa, mpenzi wako mimi sijamwita eeeh, kaona mambo ww huyawezii, ndipo kaja kwangu"
Mkuu usjali leo napakia ngoma nyingi, hope na hizi nitapakia
 
Mkuu itupie KILIO CHA YATIMA, kila siku naicheki kwa blog yako siioni, by MUUMINI MWINJUMA.
 
MWANAMUZIKI HALILA TONGOLANGA AFARIKI DUNIA

HALILA TONGOLANGA, Mwanamuziki wa siku nyingi ambaye alikuwa amelazwa katika hospitali ya Muhimbili amefariki dunia usiku wa kuamkia leo. Halila alikuwa amesafirishwa kutokea Ndanda kuja Muhimbili akihisiwa kuwa na matatizo ya figo. Licha ya kuwa alifika Muhimbili juzi Ijumaa usiku, lakini alikuwa hakufanyiwa vipimo vyovyote vikubwa mpaka umauti unamkuta. Jana Jumapili ililazimika kuanza kufanya jitihada za kupata daktari ambaye angemshughulikia kwa karibu zaidi, na daktari alipatikana ambaye aliahidi angeanza kufwatilia swala lake leo asubuhi lakini mapenzi ya Mungu yalikuwa tofauti. Juzi nilipomuona alinambia kuwa ana mengi anataka kunambia, lakini moja aliloweza kunambia pale ni kuwa yeye anajihisi ana kansa, 'Nilimuuliza anajuaje hilo, kwa vile hajapimwa hakuwa na jibu"

Wengi tutamkumbuka Tongolanga kwa wimbo wake wa Kimakonde aliouimba kwa mara ya kwanza akiwa na Les Mwenge 'Kila Munu Ave Na Kwao"..

Mwili wa marehemu unategemewa kusafirishwa leo saa tano kuelekea kwao Newala.

Mungu amlaze Pema peponi Halila Tongolanga

MUZIKI ZAMA ZILE: MWANAMUZIKI HALILA TONGOLANGA AFARIKI DUNIA
 
Nimestushwa sana na kifo hiki cha Halila Tongolanga 'Field Marshall'..

Tongolanga alikuwa na sauti tamu mnooo..Tangu akiwa bendi ya Mwenge, baadae Makondeko group ya Dk. Alex Khalid Mtavala (R.I.P)..Bendi ya Makondeko Group ilikuwa inapiga pale ukumbi waMakondeo uliokuwepo eneo la Mbezi Luguruni...Tongolanga anakumbukwa zaidi kwa wimbo wake wa Kila Munu Ave na Kwao (una matoleo zaidi ya matatu, aliuimba akiwa na bendi ya Mwenge, Makondeko group na baadae akaurudia tena akiwa na mdogo wake Sadani Tongolanga)...Pia alijiunga na akina TX Moshi William kuanzisha kundi la Bana Mwambe ambapo walitoa nyimbo kadhaa maarufu ukiwa ni wa Dotinata....

Pumzika kwa amani fundi Tongolanga....

Hapa chini nimewawekea original version ya wimbo Kila Munu Avena Kwao...


 

Attachments

Amani Iwe nanyi wakuu,
Baada ya Kuteseka na Kuhangaika huku na kule mitandaoni nikitafuta ni wapi nitapata Ku-download ngoma zote za hapo kitambo na kukosa, basi nimeona nifungue Blog yangu ZILIPENDWA ambapo kila muda naweka Nyimbo mbali mbali zilizowahi kuwika hapa Barani Africa. Nyumbani ndio kwa Sana.
Hivyo basi wale wadau wote wa Muziki wa Kale Tukutane >>> HAPA <<<
Wadau wote wa KILWA JAZZ, MSONDO, JUWATA, SUPER RAINBOW, TABORA JAZZ, SUPER MATEMBELE, IN AFRICA, MASHROOM, LESS WANYIK/SIMBA WA NYIKA nk BOFYA >>> HAPA twende Pamoja.

Shukran.


Ahsane sana mkuu.
 
Mkuu hii sina kwa Files zangu ila nina Nyimbo Kumi za Marquiz Ikiwa ni Pamoja na ile ya NI WEWE PEKEE ambayo teyari nmekwisha iweka kwenye Blog yetu.
Aksante
Mkuu naomba konjesta, kiu ya jibu na telegram za sikinde..zinanikosha sana
 
Back
Top Bottom