Kasaloo Ndio yupi hapa?!TANCUT ALMASI - URAFIKI WA UONGO
Na mtindo wao maarufu wa Kinye Kinye Kisonzo Togolaa !
Source : Zamani Leo
Du! Kumbe Hassan Dalali (aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Simba) alikuwa mwanamuziki nguli? Kumbe huyu jamaa ni kichwa aisee!!!Salama wakuu?,ni jumapili nyingine tulivu....
Leo naomba tujikumbushe bendi zetu zilizotamba sana miaka ya 80 na 90,bendi ambazo ama zimekufa ama zinaendelea kusuasua na ambazo ukisikiliza muziki wake leo hii unatamani ungerudisha wakati nyuma.
Kwa kuanzia tuanze na hawa Orchestra Vijana Jazz,bendi ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Umoja wa vijana wa CCM,bendi hii ilikuwa ikitumia mitindo ya Sindimba, Hekaheka, Heka koka, Watoto wa nyumbani, Air Pambamoto (awamu ya kwanza na ya pili) na baadae mtindo wa Saga Rhumba.
Kwangu mimi bendi hii ndiyo ilikuwa chaguo langu hasa. Ukitaka kuujua ukali wa bendi hii sikiliza nyimbo kama Chiku, Mary Maria, Penzi lamea penye penzi,Shemeji,Bujumbura,Ilikuwa lifti,Tambiko la Pambamoto, Adza(Aza), Ngapulila, Ogopa Tapeli, Mwisho wa Mwezi, Penzi haligawanyiki,Wivu, Malaine, Nyongise, Shoga,Theresa, V.I.P, Mama Chichi na nyingine nyingi tu tamu.
Bendi hii imewahi kuundwa na wanamuziki kama Hemed Maneti 'Chiriku', Hamza Kalala 'Komando', Manitu Mussa, Issa Chikupele, Hassan Dalali, Hassan Shaw, Ally Jamwaka, Abuu Semhando, Bakari 'Baker' Semhando, Mhina Panduka 'Toto Tundu', Adam Bakari 'Sauti ya zege', Eddy Sheggy, Shaban Yohana 'Wanted', Rashid Pembe 'Profesa', Kida Waziri,Beno Villa Anthony,Rahma Shally,Jerry Nashon 'Dudumizi',Suleiman Mbwembwe,Shaban Dogodogo,Aggrey Ndumbalo, John Kitime, Abdallah Mgonahazelu, Freddy Benjamin, Mohammed Gotagota, Said Hamis 'Misukosuko', Athumani Momba na wengine kibao.
Habari zaidi, soma=>Mashairi ya Kiswahili ya Nyimbo zote za Maquis du Zaire
Mkuu nyimbo za kale hazijuchi na zinavutia kuzisikiliza na kuzicheza. Sasa hivi wamekuja hawa wahuni akina Dayamondi na magenge yao ya watoto wanatuimbia nyimbo za ngono, wameuharibu muziki wetu kabisa. Naomba serikali iingilie kati.Salama wakuu?,ni jumapili nyingine tulivu....
Leo naomba tujikumbushe bendi zetu zilizotamba sana miaka ya 80 na 90,bendi ambazo ama zimekufa ama zinaendelea kusuasua na ambazo ukisikiliza muziki wake leo hii unatamani ungerudisha wakati nyuma.
Kwa kuanzia tuanze na hawa Orchestra Vijana Jazz,bendi ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Umoja wa vijana wa CCM,bendi hii ilikuwa ikitumia mitindo ya Sindimba, Hekaheka, Heka koka, Watoto wa nyumbani, Air Pambamoto (awamu ya kwanza na ya pili) na baadae mtindo wa Saga Rhumba.
Kwangu mimi bendi hii ndiyo ilikuwa chaguo langu hasa. Ukitaka kuujua ukali wa bendi hii sikiliza nyimbo kama Chiku, Mary Maria, Penzi lamea penye penzi,Shemeji,Bujumbura,Ilikuwa lifti,Tambiko la Pambamoto, Adza(Aza), Ngapulila, Ogopa Tapeli, Mwisho wa Mwezi, Penzi haligawanyiki,Wivu, Malaine, Nyongise, Shoga,Theresa, V.I.P, Mama Chichi na nyingine nyingi tu tamu.
Bendi hii imewahi kuundwa na wanamuziki kama Hemed Maneti 'Chiriku', Hamza Kalala 'Komando', Manitu Mussa, Issa Chikupele, Hassan Dalali, Hassan Shaw, Ally Jamwaka, Abuu Semhando, Bakari 'Baker' Semhando, Mhina Panduka 'Toto Tundu', Adam Bakari 'Sauti ya zege', Eddy Sheggy, Shaban Yohana 'Wanted', Rashid Pembe 'Profesa', Kida Waziri,Beno Villa Anthony,Rahma Shally,Jerry Nashon 'Dudumizi',Suleiman Mbwembwe,Shaban Dogodogo,Aggrey Ndumbalo, John Kitime, Abdallah Mgonahazelu, Freddy Benjamin, Mohammed Gotagota, Said Hamis 'Misukosuko', Athumani Momba na wengine kibao.
Habari zaidi, soma=>Mashairi ya Kiswahili ya Nyimbo zote za Maquis du Zaire
Kasaloo Ndio yupi hapa?!
Habari. Wimbo huu unaitwaje na uliimbwa na bendi gani?Mheshimiwa, kwa kweli nimekukubali.
Najaribu kuukumbuka wimbo wa Almasi, lakini maneno yanakuja halafu yanapotea.
Kulikuwepo na wimbo mwingine naukumbuka, ila nimesahau ulipigwa na nani (labda akina Hemedi Maneti au labda UDA wana bayankata), nafikiri ilikuwa kati ya 80-83.
Baadhi ya maneno yake yalikuwa hivi:
Safiri salama na usalimie wote,
Na ukifika salama nijulishe majibu mapema.
Salaam sana kwa baba, salaam sana kwa mama,
uwaeleze sijambo oh,
Lakini nakonda kwa gubu ya mume.
Jambo dogo kwake kubwa, atasema kutwa nzima,
Na usikuuu hatulali.
Hakina ninachokosa hapa nyumbani.
Kama chakula ninakula mpaka natupa.
Toka vitenge mpaka khanga hazinipiti,
Ila gubu tu la mume.....
Hizo zilikuwa enzi za kusikiliza RTD. Wenyewe tuliridhika na umaskini wetu, tukawa tunafurahia muziki wa dansi.
Wimbo unaitwa Gubu la mume. Ulipigwa na vijana jazz.Habari. Wimbo huu unaitwaje na uliimbwa na bendi gani?
BG up sana mdau umechangamsha bongo yangu jamaa wanaweza kweli kweli09 August 2021
NDOA YA MATESO (cover) Lejendari MARIJANI RAJABU
Kisauji and Babloom band live at Tiffany Diamond Hotel Makunganya street Dar es Salaam POSTA doing bomboka music Genre Bomboka Tanzania Marijan Rajabu Dar International.
Source : Babloom Kisauji
Huo sijawahi kuusikia wala katika maktaba za nyimbo walizohifadhi wazee wangu haipo. Ngoja niingie chimbo la intaneti labda utaibuka.bagamoyo kuna wimbo kaimba Remmy Ongala anasema akinywa gongo anafanya sana kazi kama unaujua jina lake naomba utupie hapa.
Hebu nitaftue wimbo huu " enyi wote wakezangu mapenzi yangu kwenu ni sawa mpendane ndio heshima ya ndoa ee"Huo sijawahi kuusikia wala katika maktaba za nyimbo walizohifadhi wazee wangu haipo. Ngoja niingie chimbo la intaneti labda utaibuka.