ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Habari humu mwenye nyimbo ya Zaita muzika inaitwa "happy birthday to you"
Mashairi yake
"Nimekununulia mkufu wa diamond pate........zaaako Ashura card yako ya birthday nimetuma siku nyingi.... happy birthday to you Ashura mpeeenzi "
Tafadhar mwenye nayo wahenga wenzangu
 
bagamoyo au mtu yeyote mwenye kibao cha Ashura kilichoimbwa na sambulumaa pls nakiomba

Ungeweka maneno mawili matatu yaendayo ya kibao hicho cha Ashura ningeweza kubashiri ni wimbo gani na nani kaupiga kama ni Sambulumaa band au bendi nyingine.

Maktaba ya wazee wetu imesheheni nyimbo nyingi, na uhakika ukiongeza nusu mstari wa wimbo huo, tutaweza ku upload hapa JF .
 
Wakati wa utoto ilikuwa bendi yangu bora. Mpaka leo nikisikiliza nyimbo zao sizichoki
 
Kama una maneno ya wimbo wa KIKO KIDS ya tabora chini ya Marehemu Salum Zahoro " MWAMTETEA BURE.....ohoohooo. hohohooo mwacheni huyooo, yaelekea hana kosa, kosa gani alilotenda, bure bure mwamfatafata..............
Chorus: mwamtetea bure, si mtu mwema huyo.......
 
Ok mkuu, acha mimi nikupe mistari miwili mitatu ya kuanzia ili uniangalizie nyimbo hizi mbili katika maktaba ya wazee.

1) Wa kwanza ni wa ukeweza ambapo muimbaji (mume) anaimba 👇

🎶Nyote wake zangu mapenzi yenu kwangu ni sawaa, mpendane ndio heshima ya ndoa eee🎶

Na nyingine ni kama vile mume amafiwa na mkewe aliekuwa anaitwa mama Jeni. Hivyo akawa anaimba 👇

🎶Mama Jeni mke wangu kwaheri mama, Mungu akulaze mahali pema peponi🎶

Natanguliza shukran kwa msaada wa nyimbo yoyote kati ya hizo mbili au zote utakazoniwekea hapa mkuu 🙏
 
Mkuu kuna mwamba kaweka hapo chini katika post ya mwisho kabisa namba 1,595 ila bado haujamtumia ili na sisi tuupate kupitia post yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…