Nenda YouTube search "eddie nassor" mtumie msg wimbo unaotaka ataupload,
Nina shida na KAPU LA MJANJA, JANJA YA NYANI pamoja na KULALA SEBULENI( uke wenza huu ni Washirika Tanzania Stars) hizo zingine mbili ni Vijana Jazz
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nenda YouTube search "eddie nassor" mtumie msg wimbo unaotaka ataupload,
Nina shida na KAPU LA MJANJA, JANJA YA NYANI pamoja na KULALA SEBULENI( uke wenza huu ni Washirika Tanzania Stars) hizo zingine mbili ni Vijana Jazz
Kulala Sebuleni : Washirika Tanzania StarsNina shida na KAPU LA MJANJA, JANJA YA NYANI pamoja na KULALA SEBULENI( uke wenza huu ni Washirika Tanzania Stars) hizo zingine mbili ni Vijana Jazz
Balantanda nimesikitika kusikia kuwa Elly Longomba kuwa alifariki. She knew how to dance the ikinda nkoi....Yap....Elly Longomba alifariki siku nyingi, tena alikufa baada tu ya kutoa/kuurudia upya wimbo wa baba yake Lovy Longomba wimbo wa 'Elly wangu' ambao alimshirikisha Papy Nguza 'Papy Kocha'...
Nakikumbuka sana kibao cha Bana Beta cha Beta Musica......Hii bendi ilitamba na kupotea ghafla...Wanamuziki waliounda bendi hii Ibonga Katumbi Jesus, Richard Mangustino, Totoo Ze Bingwa na Donat Zinga Nkuvu na mcheza shoo mahiri mwanama Salm Abeid 'Mama lao',,,
Kulala Sebuleni : Washirika Tanzania Stars
Mume wangu ana matatizo, yanayonifanya nikonde siku hadi siku mimi mwenzenu,
Mume wangu ana matatizo, yanayonifanya nikonde siku hadi siku mimi mwenzenu,
Kuniletea mke mwenzangu ndani ya nyumba, si jambo la kushangaza hilo,
Kinachoniuma moyoni ni kulala sebuleni oo, mimi na watoto jama,
Kuniletea mke mwenzangu ndani ya nyumba, si jambo la kushangaza hilo,
Kinachoniuma moyoni ni kulala sebuleni oo, mimi na watoto jama,
Yeye na mke mwenzangu hunisumbuasumbua, wanaporudi kutoka kwenye starehe zao,

Amesahau kama mimi ni mzazi mwenziwe, sijawahi kuona mume kumfanyia mke kama hivyo,
Nashindwa kudai talaka nimemzoea ee, naomba ushauri kwenu wenzangu, nifanyeje,
Kuniletea mke mwenzangu ndani ya nyumba, si jambo la kushangaza hilo,
Kinachoniuma moyoni ni kulala sebuleni oo, mimi na watoto jama,
Najitazama kwenye kioo mimi (mwenzenu eeeh), uzuri bado ninao mimi oooh (jama oooooh),
Najiuliza nina kasoro gani (mwenzenu eeeeh), Machozi yanidondoka mimi ooooh (jama oooooh),
Najitazama kwenye kioo mimi (mwenzenu eeeh), uzuri bado ninao mimi oooh (jama oooooh),
Najiuliza nina kasoro gani (mwenzenu eeeeh), Machozi yanidondoka mimi ooooh (jama oooooh),
Kwa nini mume wangu ananinyanyasa mimi eeeeh...
Kuniletea mke mwenzangu ndani ya nyumba, si jambo la kushangaza hilo,
Kinachoniuma moyoni ni kulala sebuleni oo, mimi na watoto jama......
Kapu la Mjanja - Vijana Jazz
Ndege wa rangi moja huruka pamoja ee, Uliona wapi Bundi kwenye kundi la Njiwa eee,
Ndege wa rangi moja huruka pamoja ee, Uliona wapi Bundi kwenye kundi la Njiwa eee,
Uliona wapi Bundi kwenye kundi la Njiwa eee...
Wamekususa wenzio, wamekuchoka ee, visa si visa balaa hakukaliki mamaa,
Wamekususa wenzio, wamekuchoka ee, visa si visa balaa hakukaliki mamaa,
Mwenzio kakuamini, kakufanya kama ndugu,
Mwenzio kakuamini, kakufanya kama ndugu,
Kumbe usingizi hupati udenda wakutoka,
Kumbe usingizi hupati udenda wakutoka, kaka ee kaka ee
Wamtamani mkewe, kaka wee, kaka wee
Wamtamani shemeji, kaka wee , kaka wee, yoyoo...aibuuu
Kimasomaso umejitoa, Oooo Kimasomaso umejitoaaaa,
Kimasomaso umejitoa, Oooo Kimasomaso umejitoaaaa,
Umemtamkia shemejio neno la mapenzi, Umemtamkia shemejio nipe nikate kiu..
Oooh aibu imekupa, Oooh aibu Mazabe imekupata...
Shetani kamuingia kakukubalia, Shetani kamuingia kakukubalia,
Dunia haina siri mwenyewe katambua ee, Dunia haina siri mwenyewe katambua ee,
Kaka ee kaka ee, kakufukuza nyumbani, Kaka ee kaka ee, kakufukuza kwake,
Kaka ee kaka ee, na utakula nini, Kaka ee kaka ee, sasa utalala wapi, Kaka ee kaka ee yoyoo, aibuu,
Ona sasa huna pa kula na kulala, Umekuwa kama Bundi ukionekana mkosi,
Elewa Kapu la Mjanja ,Mjinga hatii mkono, Elewa Kapu kama hilo Mjinga hatii mkono,
Elewa Kapu la Mjanja ,Mjinga hatii mkono, Elewa Kapu kama hilo Mjinga hatii mkono,
Elewa Kapu la Mjanja ,Mjinga hatii mkono, Mwenye mali ameshagukuta Dunia haina siri,
Elewa Kapu la Mjanja ,Mjinga hatii mkono, Mwenye mali ameshagukuta Dunia haina siri,
Elewa Kapu la Mjanja ,Mjinga hatii mkono, Hiyo kiu gani Zege ya kumtamani shemejiyo,
Elewa Kapu la Mjanja ,Mjinga hatii mkono, Umebaki kuwayawaya wamekususa wenzio,
Elewa Kapu la Mjanja ,Mjinga hatii mkono, Umebaki kuwayawaya wayawaya wayawaya....
Nawe nami, Bara mpaka Pwani, Pambamoto shambuliaaa....
Nawe nami, Bara mpaka Pwani, Pambamoto shambuliaaaaaaa....
Kundi Zima la The Kilimanjaro Band wakiendelea na muziki wakiwa pamoja kwa zaidi ya miaka 30 na huku wakiendelea kufanya mambo makubwa kwa mujibu za Waziri Ally naJohn Kitime na mie pia nakubaliana kabisa na maelezo hayo.
Msaada wenu wana jf msaada wa rekodi ya nyimbo hizi za zilipendwa online 1. DALILI-MSONDO NGOMA 2. CHEUSI MAGALA NO.1-OTTU JAZZ 3. MALARIA-MSONDO NGOMA 4. NIPELEKE KWA BABA NO.2-OTTU JAZZ 5. SI WAZURI BINADAMU-MLIMANI PARK ORCHESTRA Kama kuna mdau ataweza kuniaploadia online au anafahamu link ambayo nitaweza kuzipata nyimbo hizi, nitashukuru sana
Wakuu mimi natafuta sana nyimbo mbili za Ottu/Msondo Ngoma,ya kwanza ni Sekuntonza na ya pili ni Arabia fadhili. Kwa yeyote mwenye nazo naomba aweke hapa na ningefurahi zaidi kama ningepata na Video pia ya Arabia fadhili.
kuna wimbo unasema:-
Naikumbuka siku ileeee ulipokuja asubuhi na mapema,
ukifoka kwa ukali , kwamba ni mimi niliyetaka vunja ndoa yako.
Namshukuru baba mwenye nyumba,
aliyelizua panga lako,
lisishuke maungoni na kunipa kilema cha maisha.
Chorus:-
ukweli ulikuja kwa hasira sana (ehhh bwana ehhh)
bila kufahamu undani wa mambo yenyewe.
wimbo huo nautafuta sana, sikumbuki jina lake wala walioupiga