ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Dah! We jamaa umenikumbusha mbali sana.Nizamu ya kazi ni ushindi na mafanikio mema kazi,viongozi na wafanyakazi daima wote tuwe na nidhamu...migogoro na migongano ya kazini ni ukosefu wa nidhamu!! Aisee hapo ikiwa inapigwa hyo ngoma,mama anaunga kisamvu na ugari unanukia,hapo mshua amekalia kiti kama cha baba madenge anasoma gazeti la mzarendo...aisee mwenye nao atusaidie
Kama mnapatikana Dar, hizi nyimbo zinapatika mtaa Hayati Samora Machel, karibu TIB bank, kuna jamaa wanauza olds nyingi sana, and ukikuta hawana kwa muda huo basi wanakutafutia iwapo utawapa muda.
wadau kama kuna mtu anaufaham huu wimbo au anao.
Nidhamu ya kazi ni msingi wa mafanikio bora kazini, viongozi na wafanyakazi lazima wote muwe na nidhamu, migogoro na migongano makazini ni ukosefu wa nidhamu
 
Mamaaa eeeh eyaeeh Madona eenh!

Mamaaa eeeh eyaeeh Madona eenh!

Mtoto wa kwetu eenh Madona eenh!

Unipe habari eenh Madona eeenh!

Nipate kujua eenh Madona eenh!

Mwenyewe ulienda eenh Madona eenh!

Mtoto wa kwetu eenh Madona eenh!

Iyolelah Iyolelah Iyolelah.......!!!

Eeenh venye niliendaaaa!!

Oooh nakuya Na miyumbiiii..!!

Oooh miyumbi Ndio ya kwakoooo!!

Oooh ya babaee na Mamaa !!

Wanasema Mrudieeeh Mrudieeh..!!

WANASEMA Mrudie,

Mrudie Kasongo!

Wanasema Mrudie we baba!

Kwenye natoka kunawaka moto!

Kwenye natoka Kivumbi Na Jasho ooh!

Kweni kumujini ikaa eenh magangaa!

Oooooooh Kasongo! Hawa Jamaa walikua Na Mziki mzuri sana! Huwezi amini ukitazama hiyo video ya Kasongo! Wenyewe Wanasema ilikua Ni Miaka ya 1974/1975.. King Kikii Na wenzie wanafanya mambo! Hata Kiswahili walikua bado hawajakijua vizuri.
Mkuu
Nilikupa like na nimetaka kukuongeza like ingine but haiwezekani, hao jamaa walikuwa kamili, hicho kitu kimepigwa tena kama remix yaani ni hatariiiii sana, mara nyingi kinasikika kwenye pubs.

Nasikitika enzi hairudi mara mbili
 
Kuna Bendi ilikuwa inaitwa Diamond Sound mwaka 1997 ilitoa albam yenye wimbo "kibinda nkoi" Sina hakika kama nimepatia, naweza kupata audio yake?
1459088334828.jpg

Chukua hiyo halafu urudishe.
 
Hiki kitu unakipata Hapa KASONGO -




Mamaaa eeeh eyaeeh Madona eenh!

Mamaaa eeeh eyaeeh Madona eenh!

Mtoto wa kwetu eenh Madona eenh!

Unipe habari eenh Madona eeenh!

Nipate kujua eenh Madona eenh!

Mwenyewe ulienda eenh Madona eenh!

Mtoto wa kwetu eenh Madona eenh!

Iyolelah Iyolelah Iyolelah.......!!!

Eeenh venye niliendaaaa!!

Oooh nakuya Na miyumbiiii..!!

Oooh miyumbi Ndio ya kwakoooo!!

Oooh ya babaee na Mamaa !!

Wanasema Mrudieeeh Mrudieeh..!!

WANASEMA Mrudie,

Mrudie Kasongo!

Wanasema Mrudie we baba!

Kwenye natoka kunawaka moto!

Kwenye natoka Kivumbi Na Jasho ooh!

Kweni kumujini ikaa eenh magangaa!

Oooooooh Kasongo! Hawa Jamaa walikua Na Mziki mzuri sana! Huwezi amini ukitazama hiyo video ya Kasongo! Wenyewe Wanasema ilikua Ni Miaka ya 1974/1975.. King Kikii Na wenzie wanafanya mambo! Hata Kiswahili walikua bado hawajakijua vizuri.
 
Nakula Mavitu ya Miaka ile....nikisikiliza muda huu kifo cha penzi, ilikuwa lift, hiba,kibela n.k
 
Pia kuna Orch. Marquiz Original,kundi hili liliundwa miaka ya 70 na wanamuziki waliotoka katika jimbo la Shaba nchini Zaire(DRC) waliingia nchini wakiitwa Orchestre Super Gabby,baada ya kuingia nchini walibadilisha jina na kuanza kuitwa Orchestra Maquis du Zaire/Marquis Original.....Mitindo waliyoitumia ni pamoja na Ogelea Piga Mbizi,Zembwela na Sendema.....Ukumbi waliokuwa wakipiga(uwanja wao wa nyumbani) ni Lang'ata Social Hall pale Kinondoni(FM Club ambapo kwa sasa ni kanisa).....Hawa pia walikuwa wanaujua muziki hasa kutokana na aina ya muziki mchanganyiko wa kizaire(kavasha) na vionjo vya kitanzania walivyopiga....

Bendi hii ilitamba na nyimbo nyingi sana,nyimbo kama Mayanga,Ngalula,Makumbele,Mpenzi Luta,Mpenzi Scola,Karubandika,Seya,Tipwatipwa,Kisabengo,Wakati nilikuwa mdogo,Bi Sofia,Hali ngumu,Ni wewe pekee,Kibulwa,Huba wangu,Mapenzi sio masihara,Wanaume wa leo,Clara,Mayasa,Wema wangu,Double double,Mabruki,Anjelu,Balimwacha,Kazi yangu Baharia,Mapenzi ya pesa na nyingnie nyingi....Hawa jamaa wanaweza kuwa wanaongoza Tanzania kwa kuwa na nyimbo nyingi sana....

Bendi hii imewahi kuwa na wanamuziki kama Tshimanga Kalala Assosa,Issa Nundu,Mukumbule Lulembo 'Parash',Mbuya Makonga 'Adios',Ilunga Banza Mchafu.Dekula Kahanga 'Vumbi',Bobo Sukari,Fredito Butamu,Mbwana Kocks,Kabea Badu,Mutombo Lufungula Audax,Matei Joseph,Kaumba Kalemba,Mukuna Roy,Berry Kankonde,William Maselenge,Seif Said,Nguza Vicking,Kyanga Songa,Kasaloo Kyanga,Kiniki Kieto na wengine kibao..............

Hakika ya kale ni dhahabu...
Mkuu unaweza kunipa ufafanuz kuhusu mtiriko wa hiz nyimbo taraka rejea jinamiz la taraka na suruhu za shaban dede
 
Mkuu unaweza kunipa ufafanuz kuhusu mtiriko wa hiz nyimbo taraka rejea jinamiz la taraka na suruhu za shaban dede
Talaka rejea ni nyimbo aliyoitunga shabani dede baada ya kufukuzwa juwata jazz band na kisha kujiunga ddc mlimani park, alipofika ddc akatunga nyimbo ya talaka rejea kua hawezi tena kurudi juwata, 2010 akarudi msondo ngoma akatunga nyimbo ya suluhu kama kufuta kiapo chake cha nyimbo ya talaka rejea, sikinde wakamtungia nyimbo ya jinamizi la talaka kumkumbushia viapo vyake na jinsi alivyohama
 
Ivi ile nyimbo ya makutubu ya ottu jazz, jamaa walikua wanamuimbia nani?
 
Habari wakubwa, nanazitaka zile nyimbo za vipindi vya RTD enzi zile kama "Ugua Pole" au "mama na mwana" na nyinginezo kama unazikumbuka maana nazihitaji zote! naomba mnisaidie wajameni!
 
dahh!! kuna wimbo wa nadhani bi vijana jazz unaitwa barua ya telegram, nautafuta sijaupata, hata ktk mtandao haupatikani.
 
mumba naupata wapi huu wimbo?
Huo wimbo aliuimba akiwa ndekule akishirikiana na waimbaji wengine akiwemo mzee gurumo na skasi kasambula unaitwa shukrani kwa mjomba ukiwa ni utunzi wa mzee gurumo na unahusiana na maisha yake halisi.
 
Back
Top Bottom