ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Kwa leo ngoja nimalize na DDC Mlimani Park Orchestra..........Dah....Hata sijui nianzie wapi hapa maana maelezo yatakuwa marefu kweli,ngoja japo niyafupishe kidogo....

Historia ya Bendi hii inaanzia mwaka 1978 ambapo takriban wanamuziki wanane waliihama bendi ya Dar International na
kwenda kuanzisha bendi ya Orchestra Mlimani Park.Baadhi yao ni aliyekuwa mtaalamu wa kupiga ala zote King MichaelEnock, Joseph Benard, Joseph Mulenga, Abdalah Gama, Cosmas Chidumule, Machaku Salum na Habib Jeff,hawa waliungana na Muhidin Maalim Gurumo,Hassan Rehani Bitchuka na Abel Barthazar(ambaye ndio hasa muanzilishi wa Mlimani Park)..... Ilijulikan hivyo(Mlimani Park Orchestra) kutokana kuwa na maskani yake pale Mlimani Club mitaa ya Mwenge jijini Dar es Salaam chini ya umiliki wa Tanzania Transport and Taxi Services.

Mwaka 1983 waliokuwa wamiliki wa bendi hiyo walifilisika na na hatimaye bendi hiyo ikachukuliwa na Dar es Salaam Development Corporation (DDC) na hapo ndiyo ikaanza kuvuma kwa jina la DDC Mlimani Park Orchestra ikiwa chini ya wanamuziki galacha na waasisi, Muhidin Maalim Gurumo, Abel Baltazar, Hassan Rehani Bitchuka, ambao walitokea JUWATA Jazz Band huku Cosmas Thobias Chidumule, Michael Enoch ‘King Michael' na mpiga gitaa la solo mahiri, Joseph Batholemeo Mulenga, wakiwa wametwaliwa kutoka Dar International. ............Mtindo walioutumia tangu enzi hizo ni ule wa Sikinde Ngoma ya ukae.....

Baadhi ya nyimbo zilizotamba sana za Sikinde ni pamoja na Sauda/MV Mapenzi(namba 1 na 2),Neema,Usitumie Pesa kama fimbo,Mume wangu Jerry,Clara,Hiba,Matatizo ya nyumbani,Majirani huzima redio,Nidhamu ya kazi,Kassim amefilisika,Talaka ya hasira,Hadija,Barua toka kwa mama,Celina,Editha,Fikiri nisamehe,Pole mkuu mwenzangu,Diana,Pesa,Hata kama,Bubu ataka sema,Mnanionesha njia ya kwetu,Tangazia mataifa yote,Mtoto akililia wembe,Nalala kwa tabu,Duniani kuna mambo,Kiu ya jibu,Dua la kuku,Nawashukuru wazazi,Pata potea,Nelson Mandela,Uzuri wa mtu,mdomo huponza kichwa,Taxi Driver,Tucheze Sikinde,Conjesta na nyimbo niyngine nyingi tamu.....

Wanamuziki walioipitia bendi hii ni pamoja na King Michael Enock, Joseph Benard, Joseph Mulenga, Abdalah Gama, Cosmas Chidumule, Machaku Salum,Habib Jeff,Muhidin Maalim Gurumo,Hassan Rehani Bitchuka,Abel Barthazar,Henry Mkanyia,Fresh Jumbe,Hussein Jumbe,Benno Villa Anthony,Tino Masinge 'Arawa',Hassan Kunyata,Francis(Nassir) Lubua,Maalim Hassan Kinyasi,Abdallah Gama,Max Bushoke,Muharami Said,Kassim Mponda,Julius Mzeru,Said Chipelembe,Ally Jamwaka,Machaku Salum,Ally Yahaya,Shaban Lendi,Joseph Bernard,Juma Hassan Town na wengine wengi....

Suleiman Mwanyiro, Abdallah Dogodogo,
 
Afrika Mokili Mobimba by African Jazz...kibao hatari sana kutolewa na Joseph Kabasele a.k.a Grand Kalle.. kibao hiki kilirudiwa pia Tabu Ley Rochareua na Afrisa International, Sam Mangwana, Tsala Muana na Faya Tess
 
SKASSY KASAMBULA LIVE WITH THE NGORONGORO HEROES BAND,O 1 YR, MUSICIANS INTRODUCTION at "BAHAMA MAMA CLUB" Dar es Salaam , Tanzania

Choggy Sly akiwatambulisha wanamuziki wa bendi ya Ngorongoro Heroes
Source : Sulutani Kasambula
 
Kalubandika remix (Maquiz) by Boboo Sukari and Blanchard Boto

Source : Bobo Sukari Official

Mbuya Makonga wa Maquiz Du Zaire

Kilimanjaro Connection Band na Ngorongoro Heroes Band ktk Show ya pamoja zama hizoo

Bendi hizo zilikuwa na wanamuziki-tajwa wanaoonekana ktk show hiyo kabambe live kama kina Shabani Yohana Wanted, Dekula Vumbi, Burhani Muba, Selemani Mwarami, Hamisi Mlengi, Kyanga Songa & Kasaloo Kyanga, Skassy Kasambula, Mpoyi Kalonji, Maneno Uvuruge, Kalonji, Aimala Mbutu, Kanku Kelly Nkashama, Abdallah Dogodogo Challenger, Huruka Uvuruge, Jose Mulunga, Hassan Show, Thadeo Mkama, Shomari na wengineo wakiongoza mashambulizi katika Show ya pamoja Kilimanjaro Connection na Ngorongoro heroes jijini Dar es Salaam Tanzania
Source : Muziki Halisi
 
Afrika Mokili Mobimba by African Jazz...kibao hatari sana kutolewa na Joseph Kabasele a.k.a Grand Kalle.. kibao hiki kilirudiwa pia Tabu Ley Rochareua na Afrisa International, Sam Mangwana, Tsala Muana na Faya Tess

kabasele aliimbiwa wimbo wa kumuomboleza na Franco pamoja na tabu ley ni wimbo mzuri sana .
“naswa ganga wapi eh naswaganga wapi “ wanajiuliza watapata mganga wapi amrudishie uhai kabaselle
 
Salama wakuu?,ni jumapili nyingine tulivu....

Leo naomba tujikumbushe bendi zetu zilizotamba sana miaka ya 80 na 90,bendi ambazo ama zimekufa ama zinaendelea kusuasua na ambazo ukisikiliza muziki wake leo hii unatamani ungerudisha wakati nyuma.

Kwa kuanzia tuanze na hawa Orchestra Vijana Jazz,bendi ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Umoja wa vijana wa CCM,bendi hii ilikuwa ikitumia mitindo ya Sindimba, Hekaheka, Heka koka, Watoto wa nyumbani, Air Pambamoto (awamu ya kwanza na ya pili) na baadae mtindo wa Saga Rhumba.

Kwangu mimi bendi hii ndiyo ilikuwa chaguo langu hasa. Ukitaka kuujua ukali wa bendi hii sikiliza nyimbo kama Chiku, Mary Maria, Penzi lamea penye penzi,Shemeji,Bujumbura,Ilikuwa lifti,Tambiko la Pambamoto, Adza(Aza), Ngapulila, Ogopa Tapeli, Mwisho wa Mwezi, Penzi haligawanyiki,Wivu, Malaine, Nyongise, Shoga,Theresa, V.I.P, Mama Chichi na nyingine nyingi tu tamu.

Bendi hii imewahi kuundwa na wanamuziki kama Hemed Maneti 'Chiriku', Hamza Kalala 'Komando', Manitu Mussa, Issa Chikupele, Hassan Dalali, Hassan Shaw, Ally Jamwaka, Abuu Semhando, Bakari 'Baker' Semhando, Mhina Panduka 'Toto Tundu', Adam Bakari 'Sauti ya zege', Eddy Sheggy, Shaban Yohana 'Wanted', Rashid Pembe 'Profesa', Kida Waziri,Beno Villa Anthony,Rahma Shally,Jerry Nashon 'Dudumizi',Suleiman Mbwembwe,Shaban Dogodogo,Aggrey Ndumbalo, John Kitime, Abdallah Mgonahazelu, Freddy Benjamin, Mohammed Gotagota, Said Hamis 'Misukosuko', Athumani Momba na wengine kibao.

Habari zaidi, soma=>Mashairi ya Kiswahili ya Nyimbo zote za Maquis du Zaire
Sagha Rhumba ni Baba lao.
 
Marquiz du zaire - Mama Maria Nyerere

Field Marshal Nguza Chimbwiza Vicking na Maestro Ndalla Kasheba wakiongoza kundi zima la Maquiz Du Zaire kumtakia Mama Maria Nyerere maisha ya marefu na mema ya ustaafu kijijini Butiama baada ya kazi ngumu za majukumu ya kama First Lady.
Source: zamani leo

Hili ni bonge moja la Songi...dah 🙌🏾
Ila lilikosa saxa na trumpet...
 
Vundumuna Band

Kanku Kelly Nkashama (Kounkou) na wenzake enzi hizoo walikuwa bendi-tajwa.

Vundumuna personnel:
B. B. Mo-Frank (keyboards, vocal, percussion)
Tabu Frantal (guitar, vocals, percussion)
Tabu Ngongo (alto sax, vocals, percussion)
Kelly Kanku (trumpet, flute, vocal, percussion)
Wabansilu Daid Manytsho (bass, vocal, percussion)
Kabakaba (guitar, vocal, percussion)
Kapela (drums, vocal, percussion)
Micky Jagajaga (drums)
Source : B.B.Mo - FRANCK
 
Dekula Band performs Dezo Dezo

19 Apr 2014
Dekula Band performs Dezodezo - Soukous Explosion - High Life at Mosebacke, Södra Teatern, Stockholm, Sweden. Dekula Kahanga Vumbi, Boboo Sukari , Sammy Kasule ..
Dezodezo : (a copy song of Zaita Musica Band from its Yellow Card album By Freddy Ndala Kasheba
Source : Jonas Fogelström
 
Hivi ule wimbo unaimbwa 'mama nipe nauli nikamfuate Monica,amekimbia Zambia na treni ya mizigo'unaitwaje?je unapatikana ukitaka Ku download?
 
Kuna wimbo una maneno "Paka na panya waliishi nyumba moja.." Ni Wa kitambo sana sijui hata waloimba mana nilikuwa nausikia nikiwa mdogo
 
Salama wakuu?,ni jumapili nyingine tulivu....

Leo naomba tujikumbushe bendi zetu zilizotamba sana miaka ya 80 na 90,bendi ambazo ama zimekufa ama zinaendelea kusuasua na ambazo ukisikiliza muziki wake leo hii unatamani ungerudisha wakati nyuma.

Kwa kuanzia tuanze na hawa Orchestra Vijana Jazz,bendi ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Umoja wa vijana wa CCM,bendi hii ilikuwa ikitumia mitindo ya Sindimba, Hekaheka, Heka koka, Watoto wa nyumbani, Air Pambamoto (awamu ya kwanza na ya pili) na baadae mtindo wa Saga Rhumba.

Kwangu mimi bendi hii ndiyo ilikuwa chaguo langu hasa. Ukitaka kuujua ukali wa bendi hii sikiliza nyimbo kama Chiku, Mary Maria, Penzi lamea penye penzi,Shemeji,Bujumbura,Ilikuwa lifti,Tambiko la Pambamoto, Adza(Aza), Ngapulila, Ogopa Tapeli, Mwisho wa Mwezi, Penzi haligawanyiki,Wivu, Malaine, Nyongise, Shoga,Theresa, V.I.P, Mama Chichi na nyingine nyingi tu tamu.

Bendi hii imewahi kuundwa na wanamuziki kama Hemed Maneti 'Chiriku', Hamza Kalala 'Komando', Manitu Mussa, Issa Chikupele, Hassan Dalali, Hassan Shaw, Ally Jamwaka, Abuu Semhando, Bakari 'Baker' Semhando, Mhina Panduka 'Toto Tundu', Adam Bakari 'Sauti ya zege', Eddy Sheggy, Shaban Yohana 'Wanted', Rashid Pembe 'Profesa', Kida Waziri,Beno Villa Anthony,Rahma Shally,Jerry Nashon 'Dudumizi',Suleiman Mbwembwe,Shaban Dogodogo,Aggrey Ndumbalo, John Kitime, Abdallah Mgonahazelu, Freddy Benjamin, Mohammed Gotagota, Said Hamis 'Misukosuko', Athumani Momba na wengine kibao.

Habari zaidi, soma=>Mashairi ya Kiswahili ya Nyimbo zote za Maquis du Zaire
Aysee kweli JF kisima!! Kupitia huu uzi nimeupata wimbo wa Julie wa Washirika Tanzania band,mkuu Balantanda asante sana
 
Hivi ule wimbo unaimbwa 'mama nipe nauli nikamfuate Monica,amekimbia Zambia na treni ya mizigo'unaitwaje?je unapatikana ukitaka Ku download?
Naona bora niende zambia nikamtafute monica, nimlete daresalam anapambane na kesi yakeeeer, ooo monica eeeee uko wapi. Ngoma tamu sana hii. Ingia gugo fasta tu unaipakua, inaitwa KESI YA KANGA.
 
Back
Top Bottom