Zimebaki siku nne tu kwa mujibu wa katiba kumtangaza, kuthibitishwa na bunge na kuapishwa kwa Makamu wa Rais

Zimebaki siku nne tu kwa mujibu wa katiba kumtangaza, kuthibitishwa na bunge na kuapishwa kwa Makamu wa Rais

Binafsi nilikuwa namuona January kwenye hiyo nafasi ila tangu wadau wanitolee macho kuwa jamaa haitawezekana kutokana na dini, basi karata yangu nairusha kwa Nchimbi, hata nikititazama utendaji wake alipokuwa kiongozi wa UVCCM na jinsi anavyokijua chama, hapo naona kabisa anaweza kupata nafasi.
Kwani January dini gani?
 
Hahahaaa ila Membe katika watu wamechanganyikiwa na huu msiba ni Ben M. Yaaani angekuwa kule chama kubwa bado alikua anateleza tu nafasi hiyo halafu ajipange 2025
Alikosa subira.. sasa hivi anaugulia ndani.
 
Binafsi nilikuwa namuona January kwenye hiyo nafasi ila tangu wadau wanitolee macho kuwa jamaa haitawezekana kutokana na dini, basi karata yangu nairusha kwa Nchimbi, hata nikititazama utendaji wake alipokuwa kiongozi wa UVCCM na jinsi anavyokijua chama, hapo naona kabisa anaweza kupata nafasi.
Mangula hana hayo majina. VP lazima apigiwe kura ya vema na mzee Mangula.
 
Kama mzee Mangula ni lazima apige vema basi sioni kikwazo kwa Nchimbi maana hao ndio walikuwa CCM kindakindaki, wanakijua chama na wakati wa uongozi wao hapakuwa na hizi habari za ukanda na MATAGA PRAISE TEAM.
Mimi pia naona huyu Emmanuel anaweza kuwa na nafasi kubwa japo surprise inaweza kutokea.
 
Mimi pia naona huyu Emmanuel anaweza kuwa na nafasi kubwa japo surprise inaweza kutokea.
Nikweli Chief, surprise kwa CCM ni mambo ya kawaida kabisa, unaweza kushangaa Mwigulu anapewa shavu wote tukabaki mdomo wazi.
 
Wakuu

Kuanzia tarehe 17/3/2021 mpaka leo ni siku kumi. Kwakuwa katiba inatamka ndani ya siku 14 makamu awe amepatikana, basi sasa rais na chama wamebakiwa na siku 4 kutuletea makamu.

Niwatakie kila la heri na watuletee mtu mwenye uwezo.
Musiba anaweza kuibukia jengo jeupe
 
Mpaka kufikia jana kuna mahali niliweza kusikia tetesi halisi za majina pendekezwa, mpaka sasa ni majina mawili tu kwa uhakika yaliyokuwa yanafanyiwa vetting, na niliposikia hayo majina nilistaajabu, maana hakuna hata mmoja miongoni mwao anatokea kwenye kundi la watu wanaotajwa sasa au kuwahi kusikika kwenye majukwaa ya kisiasa hapa Tanzania.

Nimesita kuandika hayo majina hapa kwa sababu ya kulinda bahati zao. Nahisi kusemwa semwa mitandaoni kunaweza kuwaharibia, na mmoja kati yao ni mtu niliyewahi kufahamiana naye kwa karibu siku za nyuma.
 
Back
Top Bottom