"Zimwi" la Richmond bado linamtesa Edward Lowassa na mbio za urais

"Zimwi" la Richmond bado linamtesa Edward Lowassa na mbio za urais

willy ze great

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2013
Posts
1,071
Reaction score
1,303
VIONGOZI waliokuwa serikalini wakati wa mkataba wa kuzalisha umeme wa dharula wa Richmond bado wanaendelea kung'ang'aniwa
kwenye kashifa ya kushiriki kwenye ufisadi wa mkataba huo.

Wanaotajwa kushiriki kikamilifu, ni Edward Lowassa aliyekuwa waziri mkuu. Wengine waliokuwa mawaziri kwa nyakati tofauti katika
wizara ya nishati na madini, Dk. Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi.

Taarifa zinasema mipango ya siri ndani ya serikali ndiyo ilifanikisha mradi wa kifisadi wa Richmond/Dowans.

Je hii hiko vp na mbio za LOWASA kwenye uchaguzi 2015 atapo chuana na SLAA.

Soma
 
watanzania huyo mtu apelekwe mahakamani si ikulu. wezi ikulu kufanya nini au mnataka akaendelee na wizi? tubadilike jamani sisi huku njombe hatutaki hata kumsikia kwakua tunaogopa kuibiwa tena
 
Kumbuka, Tanzania kuna wafuata mkumbo wengi. Watu huwa hawafanyi analysis makini kwa chama au mtu. Mbinu hii ni rahisi sana kumfanya mtu awe popular na kuungwa mkono na wafuata mkumbo as long as unaweza kufinance kwa ustadi mkubwa coverage ya kupotray image nzuri ambayo kimsingi huna. Kama una image nzuri/ sifa nzuri huna haja ya kuhonga media outlets zikufanyie coverage ya upendeleo.

Tukirudi kwa ishu yako tena, EL kwa kweli amechafuka sana na Richmond hata kama ametumia mbinu ya kudai kuwa si yeye peke yake (Ref kikao cha CCM huko nyuma)..... yani kila step JK alikuwa anajua! Na alichafuka tena pale Nyerere alipomwuliza amekuaje wealthy kwa kipindi kifupi kuzidi yeye ambaye amekuwa rais for 24 years (ref Julius Nyerere speech 1994/95). Hajaweza kujibu hoja wala kupinga kupitia CCM au mahakama mpaka leo zaidi ya kulalamika tu na kuonyesha chuki kwa late Julius Nyerere.

Mkuu waTz wengi hatuelewi tatizo kuu la nchi yetu kwa sasa. Kwa mtazamo wangu tuna tatizo kubwa la RUSHWA na UFISADI. Mengine ni mazalia na maoteo yake (vifaranga vyake). Hayo ndio matatizo makuu ya nchi yetu. Rais ajae anatakiwa kuwa mtu atakaekuwa mkali sana (MBABE) na awe na absolutely ZERO TOLERANCE na rushwa kuanzia ngazi za juu. Rushwa inatuathiri sana kama taifa kimaendeleo, kimaadili na kimkakati.

Kama Mh EL anaweza kupambana na rushwa na kutupeleka mbele ndio issue ya kutafakari kwa wale wanaomfagilia. Kwa upande wangu naona kama ana uchapa kazi kiwango fulani kizuri tu, mbabe which is good, ila kwenye kupambana na rushwa + ufisadi nampa maksi chache sana kama si zero kabisa! As a person he is a good guy too, nampa big ups kwa hilo!
Waziri
 
jibuni maswali nyinyi CCM na LOWASA wenu na ufisadi wa umeme halafu leo ndio mnataka agombee urais,nauliza swali 11 ni kwanini LOWASA alimkimbia NYERERE baba wa taifa alipotaka kuitisha kikao cha kamati kuu ya CCM ali aweze kumsafisha na tuhuma za rushwa zilizo kuwa zinamkabili LOWASA enzi hizo?ccm ni vurushi la misumari huyo ndio lowasa na waziri mkuu wake JUMA Kapuya Alhaji mbunge wa tabora viva ma ccm viva LOWASA mzee wa Elimu Bure
 
Kuna kitu kinaitwa "set up" au "framed" na ndicho kilichomkuta Lowassa

Kilichomwondoa Lowassa ilikuwa ni "Politics" na sio "Ufisadi" kama ambavyo asilimia kubwa ya watanzanania walivyoaminishwa na kwa kuwa sie watanzania ni wavivu kufikiri basi ni bora liende tu

Na ndio maana leo "siasa" zinatumika kumaliza tembo..

Na wananchi walikuwa mstari wa mbele kuipinga hii operation mwisho wa siku tembo wanaisha na majangili wanaendelea kunywa kahawa
 
Lowasa can take the country at any time he wants. Hawezi kuzuiwa na Six wala Membe. Hiyo hiyo Richmond yenyewe ilimpa pesa ya kutosha kumwingiza Ikulu.
Sababu Mwl. alituusia kuwa tuogope mafisadi ni kuwa, atatumia hiyo fedha yake kuwahonga watu ili wamchague. CCM wamemwandalia njia saafi. Umaskini wetu. Huwezi amini, wengi wa watz. wa leo. Hawana uwezo wa kupata mlo wa siku. Yeye anaweza kuwalisha kwa wiki bila kutetereka.
Chukua hesabu kidogo tu: Tulimlipa mil. 150 @ siku. Kwa muda wa siku 180. Wanaofuatilia mahesabu ya zile anazochangisha kwa harambee wanajua mpaka sasa hajatoa pato la Richmond la siku 2.
Akiamua kutoa pato la siku moja tu akawagawia Watz wote tuko milion 45 hivi. Tutapewa kila mtu million 3. Upo hapo? Ndo maana anatoa boda boda leo, anatoa harambee za kufa mtu. Sio misikitini sio makanisani. Ameamua kuingia kila mahali kujifanya kutoa misaada. Bomu lake la mwisho baado.
Kwa njaa tuliyo nayo Watz. Kama ZZK alikisaliti chama chake kilichomlea sijui kama kuna atakayebaki siku EL akiamua. Ni mawazo yangu tu lakini
 
Suburi atajua vizuri richmond kama mpango wake ndo huo wa urais. Wametuona mazuzu....siyo
 
EL na slaa tayari wameshafanya deal,wanatuzuga tu muda sio mrefu nitauweka mkakati wao kabambe humu ila tutakaoumia ni chadema
 
Kuna kitu kinaitwa "set up" au "framed" na ndicho kilichomkuta Lowassa

Kilichomwondoa Lowassa ilikuwa ni "Politics" na sio "Ufisadi" kama ambavyo asilimia kubwa ya watanzanania walivyoaminishwa na kwa kuwa sie watanzania ni wavivu kufikiri basi ni bora liende tu

Na ndio maana leo "siasa" zinatumika kumaliza tembo..

Na wananchi walikuwa mstari wa mbele kuipinga hii operation mwisho wa siku tembo wanaisha na majangili wanaendelea kunywa kahawa

wewe ndo mvivu wa kufikiri! lowasa ni fisadi, alitajwa orodha ya mafisadi 11, alisemwa na nyerere mara kibao mpaka nyerere akaomba kikao cha cc ya maccm akamsafishe EL akakataa!, nyerere aliwambia wajumbe wa cc mwaka 1995 wakati wanaccm wanaomba kuteuliwa kupeperusha bendera ya ccm kwenye urais kwamba kama majina ya lowasa, malechela yangekuwemo kwenye kujadiliwa yeye katu asingethubutu kuhudhulia kikao hicho! leo lowasa anazunguka nchi nzima anaonga pesa makundi mbalimbali, anatafta nini hasa? hizo pesa anasema ni kutoka kwa marafiki zake, wanampango gani na nchi hii hawa? watanzania hatuwez kumkabidhi fisi kulinda bucha!!
 
kumbe chadema mmesha mpitisha padr slaa kuwa mgombea wa urais kabla ya kamati?

Safari hii(2015) mko dilemma maana Hamna mgombea wa dini yenu lazima mu opt either CUF au Kafir yeyote was CCM.Uwiiiiiiiiiiii poleni wachagua mwenzetu!!!!
 
Msijarb kumsafsha EL n mchaf tena sana hafai hana sifa ya kuwa raisi labda kigezo kikiwa n kwa alie ibia sana nchi basi ikulu ataingia aendelee kugawa pesa, boda boda, 2tapokea ila kura hapati
 
VIONGOZI waliokuwa serikalini wakati wa mkataba wa kuzalisha umeme wa dharula wa Richmond bado wanaendelea kung'ang'aniwa
kwenye kashifa ya kushiriki kwenye ufisadi wa mkataba huo.

Wanaotajwa kushiriki kikamilifu, ni Edward Lowassa aliyekuwa waziri mkuu. Wengine waliokuwa mawaziri kwa nyakati tofauti katika
wizara ya nishati na madini, Dk. Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi.

Taarifa zinasema mipango ya siri ndani ya serikali ndiyo ilifanikisha mradi wa kifisadi wa Richmond/Dowans.

Je hii hiko vp na mbio za LOWASA kwenye uchaguzi 2015 atapo chuana na SLAA.

Ulipaswa tu kusema kwamba:

Unaatamani kuona swala la Richmond linaamka tena na kumzuia Edward Lowasa katika harakati zake za urais 2015.
 
watanzania huyo mtu apelekwe mahakamani si ikulu. wezi ikulu kufanya nini au mnataka akaendelee na wizi? tubadilike jamani sisi huku njombe hatutaki hata kumsikia kwakua tunaogopa kuibiwa tena

sio mahakamani ni gerezani! itumike sheria ya 'detention without trial " huyu fisadi anyee ndoo! hivi haya mambulura yanayomtetea lowasa hayana uchungu na nchi hii? yenyewe yanatibiwa wapi? yanasoma wapi? utawezaje kumpeleka mwizi ikulu ? nyerere alisema ikulu ni mahala patakatifu,pasigeuzwe pango la walanguzi! ikulu si pango la mafisadi na manyanga'u! watanzania tuwe macho, tuwe makini, tutakuja kujuta, !!
 
Back
Top Bottom