"Zimwi" la Richmond bado linamtesa Edward Lowassa na mbio za urais

"Zimwi" la Richmond bado linamtesa Edward Lowassa na mbio za urais

Kwakua umeshika nyadhifa mbalimbali ktk serikali ya jamhuri ya muungano wa Tz toka enzi za baba ulipojiuzulu kwa sakata la Richmond ni wazi kwamba unafaham mafisad wote wa Richmond Na wewe ulikuwa unahusika na ndo maana ukajiuzulu sasa kama wewe mzalendo na unataka kulitumikia taifa tunaomba ututajie mafisadi wote walio husika na
1. Richmond
2.Kagoda
3.Epa
4.Escrow
5.Na uwa ambie Watanzania Balali yuko wapi

Tutajie hadharani bila kuogopa
Ukifanya Hayo Utakuwa Mzalendo Mtanzania wa pili baada ya Baba wa Taifa na Watanzania tutakukubali
 
Mtabadilisha ID mpaka basi. Kama hayo uliyouliza unataka majibu yake tumia ID yako ya zamani Sh wa a ni wewe
 
Thubutuuuuuuu!! Hawezi hata kidogo maana huo ndio utakua mwisho wa maisha yake.
 
Kwakua umeshika nyadhifa mbalimbali ktk serikali ya jamhuri ya muungano wa Tz toka enzi za baba ulipojiuzulu kwa sakata la Richmond ni wazi kwamba unafaham mafisad wote wa Richmond Na wewe ulikuwa unahusika na ndo maana ukajiuzulu sasa kama wewe mzalendo na unataka kulitumikia taifa tunaomba ututajie mafisadi wote walio husika na
1. Richmond
2.Kagoda
3.Epa
4.Escrow
5.Na uwa ambie Watanzania Balali yuko wapi

Tutajie hadharani bila kuogopa
Ukifanya Hayo Utakuwa Mzalendo Mtanzania wa pili baada ya Baba wa Taifa na Watanzania tutakukubali

Kwa hiyo umejiunga JF kwa kazi hii au?? I hope utakuwepo pia baada ya uchaguzi!!
 
Unataka akate tawi ambalo amelikalia kwani hajui mwisho wake ni nini.......Hawezi kuthubutu kusema chochote. Kwenye vikao vya chama kwa kiasi fulani alitaka kuropoka aliposema. Mwenyekiti (akimaanisha kikwete), lolote nililofanya wewe ulijua na wewe ndio ulinituma. Mwisho wa kunukuu. Hawa mapacha watatu (kikwete, lowasa na rostamu) walipiga ile diri pamoja ila lowasa aliomba amnusuru mwenyekiti, watz wamesahau kuwa mwakyembe alisema km wangesema kila kitu kuhusu ricmond basi serikali ingeanguka. Kama w/mkuu alisiginwa vile na mpaka akajiuzuru unadhani ni nani alibaki kutajwa kwenye ripoti, ndo maana kila wkt mamvi alikuwa anasema hakukutana na kikwete barabarani coz alijua atakuja kusafishwa bahati mbaya kwenye siasa there is no permanent friend rather there is permanent interests.
 
kipimo cha urais kwa sisi kina gogo la shamba tulishasema kwamba,ni kumuangalia mtu alisema nini kwenye sakata la wizi wa Escrow?
 
Unataka akate tawi ambalo amelikalia kwani hajui mwisho wake ni nini.......Hawezi kuthubutu kusema chochote. Kwenye vikao vya chama kwa kiasi fulani alitaka kuropoka aliposema. Mwenyekiti (akimaanisha kikwete), lolote nililofanya wewe ulijua na wewe ndio ulinituma. Mwisho wa kunukuu. Hawa mapacha watatu (kikwete, lowasa na rostamu) walipiga ile diri pamoja ila lowasa aliomba amnusuru mwenyekiti, watz wamesahau kuwa mwakyembe alisema km wangesema kila kitu kuhusu ricmond basi serikali ingeanguka. Kama w/mkuu alisiginwa vile na mpaka akajiuzuru unadhani ni nani alibaki kutajwa kwenye ripoti, ndo maana kila wkt mamvi alikuwa anasema hakukutana na kikwete barabarani coz alijua atakuja kusafishwa bahati mbaya kwenye siasa there is no permanent friend rather there is permanent interests.

Kweli kabisa mkuu
 
Edward Ngoyai Lowassa, ni mmoja kati ya wanachama wakongwe wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) nchini Tanzania. Jina lake linatajwa kuwa miongoni mwa watu wenye nafasi kubwa ya kuwa Rais wa awamu ya tano wa Tanzania.Mengi yanazungumzwa, mengi yanasemwa juu ya sifa na uwezo wake, makala haya hayalengi kujadili uwezo wake kama kiongozi ila nafasi yake kama mwanachama halali na mtii kwa Chama Cha Mapinduzi.Februari 18, 2014, Edward Lowassa pamoja na makada wengine wa Chama Cha Mapinduzi walipewa adhabu ya miezi 12 kwa kukiuka kanuni za uongozi na maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara 6(7)(i). Kifungo hicho kimemalizika siku chache zilizopita.Maswali mengi waliyonayo watanzania ni je nini hasa hatma ya Lowassa? Na je kihistoria Lowassa ni nani hasa ndani ya chama cha mapinduzi?Bahati mbaya sina majibu ya swali la kwanza, hata hivyo nina majibu ya swali la pili na hilo linaweza kutusaidia kujibu lile la kwanza. Je Lowassa ni mwanachama wa aina gani wa CCM?Jibu rahisi ni Lowassa ni ‘Mwana CCM Mtiifu’. Hebu tuitazame kidogo historia yake ndani ya chama. Edward Ngoyai Lowassa alizaliwa Agosti 26, 1953 na katika Kijiji Cha Ngarash huko Monduli, Lowassa ni mtoto mkubwa wa kiume kwa mzee Ngoyai Lowassa.

Kielimu, Lowassa ana Shahada ya Uzamivu (masters degree) katika Maendeleo kutoka Chuo Kikuu Cha Bath nchini Uingereza aliyohitimu mwaka 1984, na kabla ya hapo alihitimu shahada ya kwanza katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1977.Kikazi, Lowassa amekulia na kufanya kazi zaidi ndani ya CCM na serikali yake. Lowassa amejiunga na CCM akiwa chuo kikuu cha Dar es Salaam. Huko alikuwa mwanachama hai na baadae kiongozi wa Tanganyika African National Union (TANU) Youth League (baadae CCM Youth League). Mara baada ya kuhitimu masomo, aliajiriwa na CCM kama katibu msaidizi na baadaye katibu wa wilaya.Hili pekee linatosha kuonyesha kuwa Lowassa amekulia katika misingi ya chama, ameanza kuaminiwa na chama akiwa kijana mdogo (bila shaka baada ya viongozi wa chama kujua weledi, uzalendo na utiifu wake) na ameshiriki toka ujana wake kwenye ujenzi wa CCM na Tanzania kwa ujumla. Akiwa kijana ndani ya CCM alipata kuwa msaidizi wa Mzee Rashid Mfaume Kawawa, Daudi Mwakawago na Horace Kolimba.Mzee Kawawa alikuwa Waziri Mkuu wa Tanganyika na Tanzania, mmoja wa waasisi wa chama na taifa letu.

Bila shaka Lowassa alijifunza mengi kutoka kwake, na kama sio utiifu wa hali ya juu na uzalendo wake kwa chama na taifa, asingekweza kufanya kazi na mzee Kawawa,anayesifika kuwa na misimamo ya hali ya juu.Pia Lowassa ni Luteni wa jeshi, licha ya kupigana vita dhidi ya Idd Amin nchini Uganda mwaka 1978/1979, pia akiwa jeshini alifanya kazi kwa ukaribu na Rais Jakaya Kikwete pamoja na katibu mkuu wa CCM wa sasa Mh Abdulrahman Kinana ambao wote ni makada wa CCM kwa miaka mingi. Wote tunajua kuwa jeshini ndiko kulikobobea kwa kufunzwa uzalendo na utiifu wa hali ya juu.Mwaka 1985,Lowassa aliteuliwa kuwa Mbunge kupitia Umoja Wa vijana CCM (UVCCM), sambamba na Mama Anne Makinda (Spika wa Bunge la sasa) na Jenerali Ulimwengu. Mwaka 1990 alichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Monduli akipeperusha bendera ya CCM ambako amekuwa mwakilishi hadi leo.Toka mwaka 1977 Lowassa amekuwa akiaminiwa na CCM na hakuwahi kukiangusha, amekwisha kabidhiwa dhamana nyingi za uongozi zenye kumpa dhamana ya kusimamia na kutekeleza ilani za chama, nyadhifa ambazo kila wakati alizitekeleza kwa ufanisi wa hali ya juu. Lowassa amekwisha kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania (2005-2008), Waziri wa Maji na Mifugo (2000-2005), Ardhi na Makazi (1993-1995), Haki na Mambo ya Bunge (1990-1993), na Mazingira na Mapambano dhidi ya umasikini katika ofisi ya Makamu wa Rais.

Utiifu wa Lowassa kwa chama ulijidhihirisha wazi mwaka 2008 alipokubali kwa ridhaa yake kuachia nafasi yake ya Uwaziri Mkuu ili kulinda heshima ya serikali nzima, Chama tawala CCM na pia ili kuepuka mgawanyiko miongoni mwa wanachama, wananchi na viongozi. Huu ni uungwana na uzalendo wa hali ya juu, wenye moja ya vielelezo vya utawala bora.Mwaka 2014 tumeshuhudia sakata la Escrow ambapo pamoja na kuwa na ushahidi wa wazi wa pesa kwenye akaunti zao, baadhi ya Mawaziri waligoma kuwajibika kwa hiari yao na wengine kusimamishwa kazi na Rais. Lowassa alijiuzuru kwa tuhuma tu, ambazo hazikuwa na mashiko wala ushahidi yakinifu, wala walau kupewa nafasi kuhojiwa na kamati teule ya bunge.Kwa maelezo hayo nachelea kusema kuwa, Lowassa amekuwa mwanachama mtiifu kwa Chama Cha Mapinduzi kwa miaka mingi na hajawahi kukiangusha chama wala serikali wala taifa kwa namna yoyote ile. Watu kama hawa wanastahili pongezi na ni mfano wa kuigwa ndani na nje ya chama.
 
Wananchi wanamjua mwenye Richmond ndio maana Mh.Lowassa walimpa kura mpaka mkamwibia Mungu analipa hapa hapa duniani CCM wanaweweseka Na Lowassa Kipenzi cha watanzania kakaa kimya on a wewe mpumbavu umekurupuka
 
Samahani sana jamani mi nimekuta simu yangu ambayo kipindi hicho nilikuwa naitumia ndo nimekuta hizi thread
 
Back
Top Bottom