Zinedine Zidane kala shavu Qatar

Zinedine Zidane kala shavu Qatar

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
12,320
Reaction score
11,327
Zinedine Zidane amepata contract ya kuifundisha timu ya taifa ya Qatar kwa miaka minne kwa Pauni milioni 50 ambazo ni sawa na bilioni 152 na milioni 22 za kitanzania kwa mwaka, ambazo atakua analipwa pauni laki 1 na 20 ambazo ni sawa na milioni 364 na ushee kwa siku.

Qatar ndio wataandaa fainal za kombe la dunia mwaka 2022.

Kuna msemo maarufu "ukiona cha nini wengine wanajiuliza watapata lini".

Ni wazi kabisa japo watu wanapindisha pindisha ni kwamba zidane ameondoka Bernabeu sababu ya kutosikilizwa anapotoa ushauri haswa kwenye mambo ya usajili na mengineyo yanayolenga benchi la ufundi, na kuna kipindi watu wamesahau ambapo real iliyumba yumba kwenye mechi za ligi, na sababu ilikua ni hiyo, Zidane akisema hiki kwa maslahi ya timu, mwenye timu(Perez) anaenda tofauti, nahisi huu uamuzi aliufanya muda na alihakikisha kwamba atapambana ili achukue kombe la mwisho la UEFA ili waone umuhimu wake then ASEPE na amelifanikisha hilo.

nintchdbpict000393805949-e1527844510876.jpg
nintchdbpict000410014975-e1527845206610.jpg
IMG-20180601-WA0006.jpg
 
Pongezi kwa Qatar kumsainisha Zinedine Zidane..nayaona mafanikio yao ya haraka kwenye soccer la kidunia

Hata kwenye world cup 2022, Qatar itakuwa imepiga hatua kubwa sana
ni move nzuri sana hii, kwao pesa sio ISHU ila wanataka sasa na wao wawepo katika ramani ya mpira na malengo yao nadhani mwaka 2022 wakat watakapoandaa kombe la dunia basi timu yao ya taifa ifike mbali .
 
duuuu million 365 per day!!!
Kuna Watu wanabahati aiseee
Kwa hiyo hela aliyoandika mtoa mada kwamba zidane atakuwa akipata kwa siku ina makosa, bilioni 40 kwa mwaka ina maan a kwa miaka minne atapata bilioni 160, ukichukua milioni 365 ukazidisha kwa miaka minne unapata bilioni mia tano na kitu.
 
Kwa hiyo hela aliyoandika mtoa mada kwamba zidane atakuwa akipata kwa siku ina makosa, bilioni 40 kwa mwaka ina maan a kwa miaka minne atapata bilioni 160, ukichukua milioni 365 ukazidisha kwa miaka minne unapata bilioni mia tano na kitu.

Kuna watu wana pesa za kuchezea. Huku kwetu mchezaji wa simba sidhani kama anafikisha 10m kwa mwezi
 
Back
Top Bottom