Zinedine Zidane Zizzou alikuwa vipi enzi zake?

Hebu leo tumzungumzie huyu maestro Babu zizzou unakumbuka nini toka kwake enzi anasakata kabumbu

Ninachojua tu ni kwamba Wachezaji wote walijifunza mpira baada ya Kuzaliwa ila kwa Zinedine Yazid Zidane ' Zizzou ' Yeye tokea alipokuwa Tumboni mwa Mama yake alikuwa akicheza mpira huko huko na huku duniani alikuja tu kuumalizia baada ya Kuzaliwa.

Wakati nikiwa nacheza Mpira nilikuwa nikijitahidi sana ' Kumuiga ' ila mara zote nilikuwa najiumiza tu ' Enka ' yangu ndipo nikagundua ya kwamba kumbe kila Mtu hapa duniani Mwenyezi Mungu amemuumba na Kipaji chake na kumpa ' Shani ' yake na nikamuachia tu hayo ' maujuzi ' yake yote Zidane.

Ni bonge la Midfielder ambaye kila mara nilikuwa sichoki kumtizama na nilimkubali sana tena kwa 100%.
 
yani mkuu umeuongelea moyo wangu, kila timu sasa hivi ukiangalia wakabaji wao miaka ya sasa na zamani utaona imedrop. Angalau kidogo ile juve ya Bonucci na Chielini unaweza kui compare na beki za zamani.

na hili linachangiwa sana na ulipaji mishahara, mauzo ya jezi na mikataba mingine minono wanayopewa washambuliaji na wakabaji kusahauliwa.
 
Inawezekana ukawa na makengeza kidogo mkuu.

Alichokua akiweza kufanya Ronaldo De lima uwanjani ni dream tu Kwa Cristina ataishia kutizama kwenye TV tu vitu kama vile.

Ingawa cr7 simpendi lakini unafanya mistake kumfananisha na de lima...kitu gani cha ajabu alichofanya uwanjani cr7 hakufanya? Tim yake kailetea mafanikio makubwa kuliko uyo de lima, ballon de ana 5, fifa best player 5 times makombe mengi tu,, Huoni kuwa humtendei haki?

All in All Messi is from another planet...
 

Mskaji vipi weye. Cristina ata kutuliza mipra vizuri hawezi unamfanananisha na watu wenye magic skills.
 
Bange nibangue akili zangu niachie
 
Nafikiri wanashindwa kutofautisha soka la sasa na la zamani kidogo yaani huyu cr7 na messi wako wangekutana na vigingi vya kina canavaro na nesta au hiero ingekuwa kila siku wanawekwa kwenye mabango ........tatizo mabeki wa sasa ni mabishoo tu
 
toa ujinga wako hapa..!Messi na CR7 peleka chooni huko
 

Mpira wa sasa ni mgumu ukilinganisha na wa zamani bwana. Msipende kubadilisha vitu,, nikikuuliza pele alizipataje zile goli 1000 utanijibu nini?

Kwa sasa hata goli 500 asingefikisha ukweli ndio huo, na ukizingatia sheria zilivyo ngumu kipindi hiki acha kabisa
 
Mkuu hili la pele na kupinga,
kuna video moja youtube wamejaribu kuwapambanua wakali wote wa kuanzia miaka ya 2000 mpaka sasa n
Ni kwa jinsi gani wameiga vingi uwanjani kutoka kwake. tizama hapa
 
wa pele tunaweza danganya hapa sababu hatujauona ila wa kina zidane, figo nimeuona na wa kina ronaldo na messi nimeuona si kweli kwamba wa sasa ni mgumu.

nikupe tu homework

1. barcelona wana Beki kama puyol sasa hivi?
2. Madrid wana Beki kama Hierro, Carlos, salgado?
3. Man U wana Beki kama Ferdinand na Vidic na Evra?
4. Ac Milan wana Beki kama Nesta na Maldini?
5. Arsenal wana Beki kama Campbell na Tony Adams?
6. Chelsea wana beki kama Terry na Carvalho?
7. inter wana beki kama Lucio, zanetti na cannavaro?
8. bayern wanayo tena beki ya kina Lahm, lizarazu, sagnol na kuffour?

Hapo nimejaribu kukuonyesha mabeki wazuri miaka ya 90 hadi 2006 club kubwa ambao walicheza na kina Zidane, Ronaldo etc hao ni mabeki tu bado holding midfield za kina Gatusso, cambiaso, keane, viera, makelele, ze roberto etc

ukija makipa kina khan, dida, casilas, toldo, buffon, peter schimichel etc

kulikuwa na quality za hali ya juu. ndio maana wachezaji wote walikuwa hawana goli nyingi, sasa hivi nimetoa ushahidi comment ya juu, Messi na Ronaldo ndio wana consistency ila wachezaji kibao wanafika level ya goli 50.

mwaka ulioisha Harry kane ndio muingereza wa kwanza kufikisha Goli 50, kwa logic zetu Harry kane ni mchezaji bora kupata kutokea? Hana kombe hata moja ila magoli 50 anayo, hii inathibitisha sasa hivi ni rahisi kufunga.

muangalie ibra, cavani, suarez, dosti, falcao, na wengine wengi kwa vipindi tofauti wametupia magoli mengi ambayo hao ma legend hawajawahi je ina maana na wao nj bora?

quantity ni bora kuliko quality?
 
Mkuu hawa Malegend unawafahamu vizuri lakini? Me naona mpira umeanza kufuatilia majuzi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…