Zingatia haya kwa mtoto wako wa kiume wa Miaka mitano

Zingatia haya kwa mtoto wako wa kiume wa Miaka mitano

OCC Doctors

Senior Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
113
Reaction score
172
Mtoto wako wa kiume kuanzia miaka mitano (miezi 60) atahitimu mahudhurio ya kliniki. Hakikisha anafahamu namna ya kutumia zana za hapo nyumbani ikiwemo namna ya kutumia panga, shoka, nyundo, msumeno, jembe, fyekeo, reki, manati, na usafi wa bustani, iwe bustani ya mboga au ya mauwa kutamsaidia kupambana bila woga na wadudu hatari wanaovamia nyumba.

Awe na marafiki na uwe unawafahamu rafiki zake, afahamu namna ya kuendesha beskeli katika umri huo, kuandaa meza kabla na baada ya chakula. Awe anafahamu namna ya kuhakikisha usalama wa hapo nyumbani, ikiwemo kukagua milango kabla ya kulala, na kuzunguka eneo la nje ya nyumba walau kwa wiki mara moja.

Mfundishe utunzaji wa akiba kwa kumpatia pesa akuhifadhie na umuombe baada ya muda mrefu kupita. Huu ndio umri wa mtoto wa kiume kujifunza kuogelea na kulenga shabaha.

D1061_5_366_1200.jpg
 
asante sana mkuu umetukumbusha vitu muhimu sana katika malezi ila hapo kwenye hela hapoo🙄
 
Back
Top Bottom