Zingatia mambo haya unapopiga au kupigiwa simu ili usiwe kero

Zingatia mambo haya unapopiga au kupigiwa simu ili usiwe kero

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
14,395
Reaction score
13,273
Simu ni chombo muhimu sana cha mawasiliano lakini wakati mwingine kina weza kuwa karaha kutokana na sababu mbali mbali.

A: Unapo mpigia mtu simu zingatia mambo haya.
1. Ukipiga simu ukiona haipokelewi kata usisubiri mpaka mtandao ukuambie kuwa simu yako haipokelewi. Usishikilie line muda mrefu inaita wewe umeng'ang'ania tu. Simu ikiita kwa sekunde 10 au 15 haipokelewi tafadhali kata subiri hata kwa dakika moja kisha piga tena. Ukiona kimya acha piga baada ya nusu saa au saa moja. Usipige simu zaidi ya mara mbili kama haipokelewi mpe nafasi mwenye simu huenda wakati huo ana sababu ya za msingi za kutopokea simu yako usimlazimishe. Kuna watu ndani ya dakika moja una kuta kakupigia missed calls 20 Shida nini hadi uhangaike hivyo? Kwani unaye mpigia ni Fire unataka aje kuzima nyumba yako?

2. Ukimpigia mtu simu ukiona anaikata usipige tena. Huenda wakati juo mazingira haya mrusu kupokea simu. Subiri kama ni muhimu mpigie baadaye lakini usimng'ang'anize kupokea simu yako. Hapa napo kama ni mwelewa ukimpigia mtu simu akikata usimpigie tena wakati huo huo kwani hizo sasa zitakuwa ni fujo na kumnyima uhuru. Kama ni lazima mtumie ujumbe lakini using'ang'anie kupiga simu wakati unaona ina katwa. Unaweza kuta labda alisahau kuzima yupo kwenye nyumba ya ibada, kikao, anaendesha gari, ana kula sakramenti ya ndoa simu yako inaweza kumtoa kwenye reli na kumsababishia usumbufu kwa mkewe au mumewe nk

3. Ukimpigia mtu simu ukajikuta umekosea namba mwombe samahani sio tena uanze kumuuliza wewe nani uko wapi? Umesha kosea namba una taka habari zake za nini tena

4. Ukimpigia mtu simu kama huwa mnataniana, mchepuko au rafiki usianze masihara kabla ya kujua aliye pokea ndiye huyo mlie zoena naye. Kuna mdada alimpigia mchepuko wake mume wa mtu bahati mbaya akapokea mkewe jamaa siku hiyo aliisahau simu jina kwenye simu likasomeka, Mlinzi getini. Wife akafikiri mume kapiga kupitia simu ya mlinzi ili amweleze kuwa kasahau simu. Ile wife anapokea tu kabla ya kusema haloo akakutana na "baby uko wapi mbona nakusubiri muda mrefu hapa guest jamani?" Mwingene naye alimwita mama mkwe wake "we mngese uko wapi nipo na maku yako hapa baa" kumbe rafiki yake alipiga akiwa amepitia ukweni kwa jamaa huko akampa mama aongee kabla ya yeye kuanza kwa kuwa ndiyo lugha zao na jamaa ikawa hivyo. Wengine hujibu simu "we mbwa, we malaya, we konyo, we mngese" nk hata kabla ya kujiridhisha kuwa unae ongea naye ndiye kweli unaweza kuta siku hiyo kapokea mchungaji wako na wewe unajulikana kuwa ni mlokole

5.
6.

B: Ukipigiwa simu ukakoswa au hutaki kuipokea fanya haya;
1. Ukiona unapigiwa sana na huapo katika nafasi ya kupokea ni vizuri kumtumia sms mpigaji kuwa apige baadaye ukiona anasumbua sana zima simu kwa muda kidogo kisha baadaye mpigie.

2. Ukikuta missed calls za namba ngeni ni vizuri kumpigia kujua ana shida gani huenda ni mtu mwenye uhitaji mkubwa au ana kutafuta kwa jambo zuri. Kama una wasi wasi jaribu kwanza kufanya kama una mtumia pesa ili ujue ni nani. Wakati mwingine unaweza kuta ni mkeo, mumeo au ndugu wa karibu aliishiwa salio au chaji akaomba simu ya mtu ili awasiliane na wewe. Si vizuri kukwepa namba ngeni hata kama una daiwa sana. Hii hutokea sana kwa watu wenye madeni akipigiwa na mdai wake hapokei. Sasa ikiingia namba ngeni ana dhani mdai wake kaamua kutumia namba ngeni ili kumpata hivyo hapokei hata hiyo ngeni.

3. Ukipigiwa simu na mkeo, mumeo au anaye kudai na ukataka kumdanganya uliko jitahidi kabla huja mdanganya umejiridhisha kweli hajui uliko. Unaweza kuta anakupigia kumbe mpo wote baa moja au gari moja au ukute kuna rafiki au jirani yako kakutana na mkeo au mumeo halafu aka mwambia uliko sasa wewe ukipigiwa unasema bado upo Chalinze labda utafika baada ya masaa matatu au upo msibani ndio ibada inaendelea.

4.
5...

Hayo ni baadhi ya mambo muhimu ya kuzingatia ukipiga au kupigiwa simu. Ongezea uyajuayo.
 
Haya mambo tungekumbushana 2005 simu ndio zinaanza kupamba moto.
 
Kuna watu wanapiga simu,
unapokea afu unaskia bado anaongea na watu wengine pembeni.

Inakera Sana
 
Back
Top Bottom