Zingatia Sifa Kuu 3 za Mwanamke wa Kujenga naye maisha (wife material)

Zingatia Sifa Kuu 3 za Mwanamke wa Kujenga naye maisha (wife material)

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2023
Posts
382
Reaction score
687
Kwanza kabla ya kuangalia sifa za mwanamke, angalia sifa zako kwanza kisha ujitathmini kama unastahili kuwa mwanamke mwenye sifa hizi.

Ni muhimu kumpima mwanamke uliyenaye kama anafaa kuwa nawe maishani. Sio uwe naye sababu ndio mwanamke aliyekuonesha upendo.

Ndio maana wakati wa uchumba inabidi umeangalie na umchunguze kama ana sifa zitakazokufanya useme ‘yes, hapa nimepata’.

Japo sifa zipo nyingi zinazoweza kusema huyu mwanamke anastahili au la, lakini hizi ni za msingi kuanzia

Anajali
~ Anajali afya yake, hata kabla hujakutana naye amekuwa anajijali, umekua naye kimahusiano, bado pia anajijali. Yupo tayari kuhangaikia afya yake, hakatii tamaa mwonekano wake sababu yupo tayari kukufurahisha na uzuri wake.

~ Anajali na mwonekano wake pia, kwa sisi wanaume tunavutiwa kirahisi na mwonekano wa mwanamke, wa nje haraka sana. Kama mwanamke alikuvutia kwa mwili wake wa wastani lakini baadae akafutuka kuwa kibonge, lazima hamu yako ya mapenzi kwake itapungua.

Mwanamke anayelitambua hili, lazima ataendelea kujitunza kulingana na mwonekano aliojaliwa ili na mwanaume wake afurahie pia. Kama unaona mwanamke wako hajali afya yake, je itakuaje kuhusu mtoto wako atakayembeba tumboni?

Anajijali kiroho, anafanya vitu vinavyomsaidia kukua kiroho. Anatunza amani yake na amani ya familia. Anajali uhusiano wake na Mungu.

Anajali kuhusu familia, anaonesha kujali kuhusu familia yako na yake. Ana ukaribu na familia yake. Anajali uhusiano wa familia na Mungu. Pia yupo tayari kuwa na familia.

Mtu wa msamaha, uvumilivu na shukurani
Mwanamke wa hivi utamjua kwa kuangalia jinsi anavyoishi na watu wengine. Hasa shosti zake. Hawasemi vibaya marafiki zake nyuma yao. Anawasemehe waliomkosea mana anajua naye si mkamilifu.

Pia ni mtoaji.

Mwanamke wa hivi ni rahisi kuweka naye malengo kimaisha. Mwanamke wa hivi ni rahisi kukuvumilia kipindi ambacho unayumba.

Kinyume cha huyu ni mwanamke; mlalamishi, mtu wa kulaumu sana, hana shukrani wala msamaha.
Anaweza asikuoneshe ihzo tabia mwanzoni, akaficha na kuigiza tabia mbele zako, lakini, ukitaka kumjua kirahisi mwanamke wa hivi, angalia anavyoongelea kuhusu watu wengine. Hasa mashosti zake.

Je, anaongelea mashosti zake vibaya wasipokuwepo? Je, anakulalamikia kuhusu shosti zake/ vitu vya kazini kwake mno? Ujue ipo siku we ndio utakua wa kulalamikiwa mpaka hamu yako ya mapenzi naye itakata.

Je, kila muda anasema yaani yule fulani siwezi kumsamehe na matusi juu? Ujue ipo siku huo ubao utakugeukia wewe. Wanawake wa hivyo si wazuri kwa afya yako na maisha yako.

Hana historia ya wapenzi wengi. Hajatembea na wanaume wengi, yaani hajafanya mapenzi na wanaume wengi. Maana yake amehifadhi ngono kwa ajili ya mwanaume anayestahili zaidi, sio kila awezaye kumvua chupi.

Maana yake anaweza kujiongoza na kutokulala na kila mwanaume anayeonesha nia naye. Maana yake anaweza kukutunzia tunda endapo utateleza kwenye mahusiano na sio kuligawa kwa watu wengine hovyo.

Hapa ujiulize, mwanamke ambaye miaka yake yote anadanga, kipi utamfanyia asiache kudanga akiwa na wewe, kisha angalia kama hajawahi fanyiwa icho kitu, utagundua we sio wa kwanza.

Pia kuna wanawake aina mbili, wanaopenda kuchombeza wanaume wengine hovyo na ambao wanahidhi chombezo zao kwa ajili ya wanaume wao.

Usije ukajichanganya kutaka kujenga maisha na ambaye yupo tayari kuchombezana na wengine ili apate furaha.

Usije ukaruka kukimbilia kuishi na mwanamke bila kujihakikishia ana sifa hizo. Afya yako ni muhimu na malengo yako kutimiza yatakua ni rahisi kama ukiwa na mwanamke ambaye hakupi mawazo.

Kuna jamaa mmoja jirani yangu, anajitahidi kweli kufanya kazi ili apate hela zaidi aishi maisha vizuri, lakini ukifika muda wa kurudi nyumbani anaumwa sababu nyumbani anakutana na mwanamke ambaye anamlalamikia kwa kila kitu na shukrani kidogo, ubaya pia ni kwamba amezaa naye. Hivyo, kuwa makini.

Kama we ni mwanamke unasoma, zingatia haya, jijali, kuwa mtulivu usiwe mdangaji, na uwe na tabia ya msamaha na shukrani.
 
HAYA MAMBO NI MAGUMU MNO MKUU, HAWATABIRIKI HAWA NA WALA HAWANA FORMULA MAALUMU YA KUWAPATA
 
Huyu anaota akiwa chin ya kitanda
 
Back
Top Bottom