Shukrani na hongera sana kwa kuanzisha huu uzi. Nikiwa na mzigo china, say machinery uko tayari kwa kuchukuliwa kutoka kiwandani, na unatosha kabisa kujaza kontena. Je shipping agent wa hapa TZ anaweza kutuma contena kiwandani kwenda kuuchukua na kuusafirisha kuja TZ, au mi ndo mwenye wajibu wa kumfikishia kwenye warehouse yake kama wafanyavyo wenye loose cargo? Na je, ni kampuni gani hapa TZ inayoaminika kwa kazi kama hiyo? Na je, kama nimepata certificate of incentives ya TIC, hivyo vyote kampuni ya usafirishaji itashughulikia wakati wa kugomboa kontena bandarini? Natanguliza shukrani🙏
🙏🙏
Mkuu,
Kwa ufupi ni kuwa hizi shipping lines siyo za watanzania, hivyo nyingi zipo huko duniani, huku Tanzania wana mawakala.
Kama unatoa mzigo china, huyo shipper wako (kiwandani) anaweza kukusaidia kufanya process za export huko.
Yeye atakusaidia kufanya booking na ku stuff mzigo kwenye container,
Kuna shipping lines nyingi hivyo anaweza tafuta/chagua kulingana na urahisi kwake.
Akishapakia na kulipa freight charges, atakutumia kitu kinaitwa BILL OF LADING, (hii inaweza kuwa original, Way bill non negotiable au Telex release) ili wewe ufanye process za importation huku.
Kumbuka huku hutaweza kutoa mzigo wewe mwenyewe lazima utafute clearing agent aliyesajiriwa TRA.
Atakusaidia process zote za huku.
Kwa container uwe makini na sharp na ujiandae na pesa za ushuru wote ili kuepuka storage charges na demurage charges.
Pia uandae na deposit fee ambayo inarudi kama dollar 500 ili shipping line wakuruhusu kutoka na container yao. Ukiwarudishia wanakurudishia pesa yako.
Kwenye agent hapo ndo uwe makini. Na malipo yote muombe control number ulipe mwenyewe labda ya shipping line ndo yana invoice.
All the best
Naamini nimekupa mwanga kidogo