Sasa mimi nimekwenda supermarket kupeleka korosho zangu kwa muhindi anadai anataka risiti za EFD machine, sasa mimi nanunua korosho kutoka kwa mkulima kule shambani kusini ambapo haelewi hata nini maana ya hiyo kitu ina maana nikija kuuza korosho zangu supermarket nakuwa natoa risiti za kuuza tu sina risiti za kununulia. Je hiyo ouput na iput itakokotolewa vipi hapo? Si nakuwa inakula kwangu tu?
#Keynessian
Aisee kwanza VAT Ni somo pana Ile kishenzi.
Bidhaa Zina angukia kwny category 3.
Exempted-Hizi hazichajiwi VAT
Standard rated-Zina chajiwa 18%
Zero rated-Zinachajiwa 0%
Korosho ambazo Ni unprocessed hizo zinakua exempted(hazichajiwi VAT),zikiwa processed hizo zinakua charged(18%).
Ili kujua amount utakayopeleka TRA au utakayokua refunded, formula Ni = VAT Output(sales)-Input tax claimed(Purchases)
Kwny hio formula ukipata Positive no. Then hio ndio amount utapeleka huko TRA na ukipata Negative No. then hio ndio utakua refunded na TRA.
Sasa wewe kununua korosho kutoka kwa wakulima maana yake unanunua bidhaa ambayo Ni exempted(unprocessed korosho) na huwezi uka claim input tax kutoka kwny exempted good.
Input tax inakua claimed kutoka kwny bidhaa Zinazo chajiwa at Standard rate(18%) au Zero rated(0%)-Zero rated hapa Zina angukia bidhaa/huduma nyingi zinazokua exported kwenda nchi za nje.
Sasa wewe kwa mfano: umenunua korosho za mil 1 maana yake hapo hio Input tax(yaani VAT kwny manunuzi) huwezi uka-claim,then unapoenda kuuza kwa mhindi kwa mfano labda kwa sh. 1,500,000
Inabidi ujue hio bidhaa yako umeshaiwekea VAT kwny hio Bei unayouza(VAT inclusive) au hujaiwekea VAT(VAT exclusive)
1)Kama hio 1.5mil Ni VAT inclusive ili kujua VAT output(VAT kwny kwny mauzo yako) unafanya 1.5mil×18/118=Tsh 228,813
Na kujua VAT itakayopelekwa TRA inakua, VAT output-input tax claimed=228,813-0=Tsh.228,813
2)Na Kama hio Bei yako Ni VAT exclusive then VAT output inakua 1.5mil×18%=270,000
Na kujua VAT itakayopelekwa TRA inakua VAT output-input tax claimed 270,000-0=Tsh 270,000
Lkn swali langu Ni je wewe unaqualify kua VAT registered?Sababu Kuna category nyingi za watu wanaokua VAT registered,wewe kwa category yako ili qualify Ni lazima uwe una mauzo ya mil 100 kwa mwaka(na bidhaa unazouza ziwe kwny category ya Standard rated au Zero rated) au uwe na mauzo ya jumla ya Tsh. Mil 50mil kwa miezi 6.
Lkn kua na machine ya EFD sio lazima uwe VAT registered,mtu yoyote akifikisha mauzo ya Tsh. Mil 11,000,000 kwa mwaka anatakiwa awe nayo hio machine.
Naona mhindi anakomaa kutaka kufanya biashara na mtu mwenye EFD machine na ambae Ni VAT registered ili aweze ku-claim input tax yake la sivyo hataweza ku-claim.
Sijui Kama nime eleweka boss,Ila VAT Ni somo pana chief.