Zipi ni Hasara za kutumia mashine za EFD kwa mfanyabiashara?

Zipi ni Hasara za kutumia mashine za EFD kwa mfanyabiashara?

Elimu inahitajika sana kuwaelewesha wafanyabiara ndogo ndogo kuhusu kodi hii ya VAT ya 18%.
1. Kodi anayelipa ni mlaji wa mwisho, hivo kutokuchukua risiti Manake umemwachia muuzaji hii Pesa. Muuzaji haumii kwa namna yoyote kwenye hii kodi

2. Kuna kitu kinaitwa VAT refund yani tofauti ya input na output tax, Manake ni kodi ya VAT muuzaji aliyolipa akinunua mzigo vs ile aliyopokea wakati wa kuuza bidhaa. Tuite ya kwanza A na ya Pili B.
A ikiwa kubwa kuliko B ataclaim icho kilichozidi TRA

3. Machine za EFD zinapatikana database inayoweka record ya mauzo kwa kipindi husika .
Wafanyabiashara wengi wanakwwpa kutumia ili mauzo yote yasiwe captured kwenye mfumo na mwisho wa siku TRA wa kadirie kuliko kupata mapato halisi ambayo ni Mara nyingi huwa ni mengi.

Nikipata wasaaa ntafafanua zaidi badae
Kwa maelezo haya ni wazi mfanyabiashara wa Kati akitoa risiti kwa kila BIDHAA anayouza atafirisika
 
Elimu inahitajika sana kuwaelewesha wafanyabiara ndogo ndogo kuhusu kodi hii ya VAT ya 18%.
1. Kodi anayelipa ni mlaji wa mwisho, hivo kutokuchukua risiti Manake umemwachia muuzaji hii Pesa. Muuzaji haumii kwa namna yoyote kwenye hii kodi

2. Kuna kitu kinaitwa VAT refund yani tofauti ya input na output tax, Manake ni kodi ya VAT muuzaji aliyolipa akinunua mzigo vs ile aliyopokea wakati wa kuuza bidhaa. Tuite ya kwanza A na ya Pili B.
A ikiwa kubwa kuliko B ataclaim icho kilichozidi TRA

3. Machine za EFD zinapatikana database inayoweka record ya mauzo kwa kipindi husika .
Wafanyabiashara wengi wanakwwpa kutumia ili mauzo yote yasiwe captured kwenye mfumo na mwisho wa siku TRA wa kadirie kuliko kupata mapato halisi ambayo ni Mara nyingi huwa ni mengi.

Nikipata wasaaa ntafafanua zaidi badae
Asante,naomba ukipata wasaa urudi kuelezea hasa kwenye VAT refund tujue inafanyaje kazi na je inatekelezwa na TRA?

Je Inawezekana wafanyabiashara wanaogopa bure tu?
 
Sasa mimi nimekwenda supermarket kupeleka korosho zangu kwa muhindi anadai anataka risiti za EFD machine, sasa mimi nanunua korosho kutoka kwa mkulima kule shambani kusini ambapo haelewi hata nini maana ya hiyo kitu ina maana nikija kuuza korosho zangu supermarket nakuwa natoa risiti za kuuza tu sina risiti za kununulia. Je hiyo ouput na iput itakokotolewa vipi hapo? Si nakuwa inakula kwangu tu?
#Keynessian
Hapo wewe ndio utaumia
 
ungekuwa muhindi asingedai
 
Faida ya kutumia masine za EFD ni kuwa serkali inapata haki yake, na wewe mnunuzi unaponunua kitu ile kodi ya sales tax ambayo unalipa wewe mnunuzi unapelekwa kunakohusika...serkalini. Ukinunua mathalani sahani sh 500 na ukalipa sales tax sh 50, basi hiyo 50 si mali ya muuzaji bali serkali. Yeye anakusanya kwa nuiaba ya serkali. Lakini wafanyabiashara wanachukuwa faida yao na ile kodi ya sales tax ya serkali.
Na hasara ya kutumia mashine ya EFD kwa mfanyabiashara ni ipi?au hakuna hasara yoyote?
 
Elimu inahitajika sana kuwaelewesha wafanyabiara ndogo ndogo kuhusu kodi hii ya VAT ya 18%.
1. Kodi anayelipa ni mlaji wa mwisho, hivo kutokuchukua risiti Manake umemwachia muuzaji hii Pesa. Muuzaji haumii kwa namna yoyote kwenye hii kodi

2. Kuna kitu kinaitwa VAT refund yani tofauti ya input na output tax, Manake ni kodi ya VAT muuzaji aliyolipa akinunua mzigo vs ile aliyopokea wakati wa kuuza bidhaa. Tuite ya kwanza A na ya Pili B.
A ikiwa kubwa kuliko B ataclaim icho kilichozidi TRA

3. Machine za EFD zinapatikana database inayoweka record ya mauzo kwa kipindi husika .
Wafanyabiashara wengi wanakwwpa kutumia ili mauzo yote yasiwe captured kwenye mfumo na mwisho wa siku TRA wa kadirie kuliko kupata mapato halisi ambayo ni Mara nyingi huwa ni mengi.

Nikipata wasaaa ntafafanua zaidi badae

Wafanyabiashara wadogo hawana VAT acha kudanganya
 
Aisee kwanza VAT Ni somo pana Ile kishenzi.

Bidhaa Zina angukia kwny category 3.

Exempted-Hizi hazichajiwi VAT
Standard rated-Zina chajiwa 18%
Zero rated-Zinachajiwa 0%

Korosho ambazo Ni unprocessed hizo zinakua exempted(hazichajiwi VAT),zikiwa processed hizo zinakua charged(18%).

Ili kujua amount utakayopeleka TRA au utakayokua refunded, formula Ni = VAT Output(sales)-Input tax claimed(Purchases)

Kwny hio formula ukipata Positive no. Then hio ndio amount utapeleka huko TRA na ukipata Negative No. then hio ndio utakua refunded na TRA.

Sasa wewe kununua korosho kutoka kwa wakulima maana yake unanunua bidhaa ambayo Ni exempted(unprocessed korosho) na huwezi uka claim input tax kutoka kwny exempted good.

Input tax inakua claimed kutoka kwny bidhaa Zinazo chajiwa at Standard rate(18%) au Zero rated(0%)-Zero rated hapa Zina angukia bidhaa/huduma nyingi zinazokua exported kwenda nchi za nje.

Sasa wewe kwa mfano: umenunua korosho za mil 1 maana yake hapo hio Input tax(yaani VAT kwny manunuzi) huwezi uka-claim,then unapoenda kuuza kwa mhindi kwa mfano labda kwa sh. 1,500,000

Inabidi ujue hio bidhaa yako umeshaiwekea VAT kwny hio Bei unayouza(VAT inclusive) au hujaiwekea VAT(VAT exclusive)

1)Kama hio 1.5mil Ni VAT inclusive ili kujua VAT output(VAT kwny kwny mauzo yako) unafanya 1.5mil×18/118=Tsh 228,813

Na kujua VAT itakayopelekwa TRA inakua, VAT output-input tax claimed=228,813-0=Tsh.228,813

2)Na Kama hio Bei yako Ni VAT exclusive then VAT output inakua 1.5mil×18%=270,000

Na kujua VAT itakayopelekwa TRA inakua VAT output-input tax claimed 270,000-0=Tsh 270,000

Lkn swali langu Ni je wewe unaqualify kua VAT registered?Sababu Kuna category nyingi za watu wanaokua VAT registered,wewe kwa category yako ili qualify Ni lazima uwe una mauzo ya mil 100 kwa mwaka(na bidhaa unazouza ziwe kwny category ya Standard rated au Zero rated) au uwe na mauzo ya jumla ya Tsh. Mil 50mil kwa miezi 6.

Lkn kua na machine ya EFD sio lazima uwe VAT registered,mtu yoyote akifikisha mauzo ya Tsh. Mil 11,000,000 kwa mwaka anatakiwa awe nayo hio machine.

Naona mhindi anakomaa kutaka kufanya biashara na mtu mwenye EFD machine na ambae Ni VAT registered ili aweze ku-claim input tax yake la sivyo hataweza ku-claim.

Sijui Kama nime eleweka boss,Ila VAT Ni somo pana chief.
Maelezo ni mazuri japo ni marefu mno kwa mfanyabishara wa kawaida kuelewa Ila naomba tujadili hapo mwishoni ulipomalizia kwamba;

Mfanyabishara anayeuza 11,000,000 kwa mwaka anatakiwa apewe mashine ya EFD,yeye huyu akipewa mashine na akatoa risiti kwa kila bidhaa kama inavyotakiwa Je atapata faida ilihali hayupo VAT registered?
 
Muuza Duka kanunua mzigo kutoka kwa mfanyabiashara mkubwa e.g Unga shilingi 100,000
Muuza duka anauleta dukani kwake na kuamua kuuza shilingi 120,000
20,000 ndio Gross profit.
EFD inamtaka atoe risiti ya shilingi 120,000 ambapo ndani yake kuna mtaji na faida.

Kodi 18% ya 120,000 ni 21,6000
Kodi ni kubwa kuliko faida ulioipanga ya shilingi 20,000

Wafanyabiashara wengi hawajaelimishwa kuhusiana na huo mkanganyiko hivo wengi wameishia kukwepa kutoa risiti

Samahani niruhusu nikusahihishe

18% ni 21,600/= siyo 216,000/=
 
Uzuri yale mamashine ni kuharibika, likiharibika unalirudisha kisha unapumzika, wakilileta linaharibika tena
Umejiuliza zile route za kwenda na kurudi TRA kugongewa muhuri wa kuuza bidhaa na receipts za kitabu zinavyokupotezea muda wako?
 
Uzuri yale mamashine ni kuharibika, likiharibika unalirudisha kisha unapumzika, wakilileta linaharibika tena
Ingekuwa mie ningekuwa naipigisha shoti tu😅 izingue basi kisha naendelea na biashara kama kawaida
 
Back
Top Bottom