Kaka Elia, kama nimekuelewa wewe unatamani kupata mke, na sio demuuuuuuu!!
Kumbuka mke mwema anatoka kwa Mungu, haina maana usimtokee msichana kumwambia hilo hitaji lako hapana.
ILa mshirikishe Mungu, Muombe Mungu akuongoze katika hilo. Omba Mungu akupe utulivu wa moyo.
Halafu usiwe na haraka, hata kama unadhani una haraka ktk hilo. Utulivu ni mzuri kwa sababu hutakurupuka ktk maamuzi yako.
Finally utashangaa utampata mke mwema.
Note: Mke mwema humpati kwa sababu una pesa, au we ni mzuri, au una kazi nzuri, au unajua sana kuongea, au ni msafi sana,au chochote kile kinachoonekana kwa macho. Hivyo vyote ni zaida tu.
Ila mke mwema anakuja kwako kwa sababu wakati aliokupangia Mungu kuoa umefika.