Zipo baadhi ya nchi zilizouza maeneo yao

Zipo baadhi ya nchi zilizouza maeneo yao

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
ukiingia google ukasearch kwa heading

List of territory purchased by a sovereign nation from another sovereign nation​

Utaletewa nchi nyingi sana zimefanya biashara hii na wanakuletea mpaka bei walinunua

Mifano michache

Louisiana - Marekani ilinunuliwa kutoka France kwa USD 15,000,000
Florida - Marekani ilinunuliwa kutoka Spain kwa USD 5,000,000
California, Nevada, Utah, Arizona - Marekani zilinunuliwa kutoka Mexico.

Orodha ipo kubwa na jambo ambalo Tunatakiwa kuogopa ni kwamba nchi ikiuzwa kulipa madeni wenyeji hamtaenda kuenjoy maisha mazuri ya huko mlikonunuliwa bali watakuja wageni na kuchukua ardhi zenu, mali zetu na nyinyi kufanywa watumwa.

Sijasema viongozi wetu wanataka kutuuza bali hoja ni tuelezane ukweli kuwa nchi zinazouzwa zipo na tunapoamua kukopa tukope kwa staha, kwa ajili ya mambo ya msingi yenye tija na tuwe na uwezo wa kulipa
 
Bila kusahau Alaska..(kutoka Russia)

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
job alikuwa sahihi ,Ila watu hawapendi kuambiwa ukweli!
 
Zilinunuliwa miaka ipi na ukiangalia zote sababu ilikuwa ya kidemokrasia. Na wafalme ndo waliuza
 
Sidhani kama mfano huu uko sawa na haya ya kwetu
Kweli zilinunuliwa lakini waliouza ni mataifa yaliyotawala huko na kumuuzia USA
Je ziliuzwa kwa ajili ya madeni na nani alidaiwa na nani

Au sijaelewa
 
Ikija hoja ya kuuza sehemu ya nchi watu watapiga kelele, lakini ni jambo la kawaida tu na lenye faida kama tu viongozi ni wawazi na wawajibikaji baada ya kupata fedha za mauzo,

Kwa mfano, tunaiuza Geita kwa TSH Trilion 400 -500 hivi. Pesa hii itaboresha kwa kiasi kikubwa nyanja za kiuchumi na kijamii kwa maeneo mengine ya nchi, kuliko kuendelea kuishi kwa shida wakati hatujahamia humu Duniani. Standard gauge ngapi zitajengwa?

Hii nchi ina rasilimali zinazopatikana karibu kila sehemu ya nchi, hivyo hakuna ubaya kuuza baadhi ya maeneo yenye rasilimali kwani ni mengi. Kwa mfano, mbuga za wanyama zipo kibao, hivyo tukiiuza Ngorongoro, tunapata hela na tunabaki na Serengeti, Mikumi, Katavi nk.

Ni bora kuuza eneo la nchi kuliko kulikodisha. Kwa mfano, kama hayakufanyika mabadiliko, Geita Gold Mine (GGM) alikodishiwa mwekezaji kwa miaka 99. Hii ilikuwa ni mwaka 1999 au 2000 kama sijakosea. Mpaka miaka 99 iishe, Geita itakuwa ni mashimo, ila kama tunaiuza, hayo mashimo hayatuhusu.

Wazungu hawakuwa wajinga kuuza maeneo kwa USA, kwani walipata hela ya kufanya mambo yao mengine.

Mfano, mwaka 2019 Trump alikumbushia dili la kukinunua kisiwa cha Greenland, baada ya Denmark kuona anapata hasara ya kukihudumia.

Hivyo, ni bora tupige mnada baadhi ya maeneo kuliko kukodisha. Hebu fikiria bandari inachukuliwa kwa miaka 100! Si ni bora kuuza eneo fulani la nchi na kulipa deni kisha mnabaki na bandari yenu?

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom