Zipo tabia zinazoashiria kwamba mhusika hataishi maisha marefu. Je, wewe uko kwenye kundi hilo?

Zipo tabia zinazoashiria kwamba mhusika hataishi maisha marefu. Je, wewe uko kwenye kundi hilo?

Mathanzua

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2017
Posts
17,449
Reaction score
23,124
da264506bab67aaabc0c37d4b37479dc

Kwa kawaida maisha ya binadamu mwisho wake huwa ni kufa,kwa hiyo kila mwenye pumzi ni lazima siku moja ataonja mauti.Hata hivyo wapo watu wengi wanaokufa mapema na kijinga kabla ya muda aliopanga Mungu.

Kuna tabia au viashiria fulani ambavyo huweza kuonyesha kwamba watu fulani huenda wakapoteza maisha mapema kutokana na mfumo wao wa maisha.

Miongoni mwa dalili,viashiria au tabia ambazo huweza kuashiria kwamba mhusika anaweza kuwa na maisha mafupi duniani ni pamoja na hizi zifuatazo.

1.Watu wanaopenda anasa na starehe.
Watu wa aina hii huwa katika hatari ya kupoteza maisha haraka hata kabla ya siku zao kutokana na kuwa na hatari kubwa ya kupatwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo yatokanayo na zinaa.Hatuna budi pia kukumbuka kwamba dhambi inaua.

2. Wavutaji wa sigara.
Watu wanaovuta sigara huwa katika hatari ya kuishi maisha mafupi zaidi kuliko wale ambao hawatumii sigara kwani watu wa aina hii huwa katika hatari ya kukumbwa na magonjwa kama saratani,kisukari,magonjwa ya moyo nk. ambayo huweza kukatisha uhai wa mhusika hata kabla ya siku zake.

3. Kutofanya mazoezi au kukaa bila kazi
Watu ambao huwa miili yao haina mazoezi kabisa nao huwa katika hatari ya kupoteza maisha mapema kutokana na kushambuliwa na magonjwa yasiyoambukiza kama vile shinikizo la damu, kisukari nk.

4. Unywaji wa pombe.
Watumiaji wa vileo na huwa katika hatari ya kupoteza maisha yao mapema kutokana na mambo matatu makuu.

a) Kupata ajali kutokana na kutumia vyombo vya moto wakati wakiwa wamelewa na baadaye kujikuta wanapoteza maisha.

b) Ugomvi ambao huweza kuibuka kutokana na mihemko ya vilevi wanavyokuwa wamekunywa na kuweza kusababisha ugomvi mkubwa. Mfano kupigana na chupa na baadaye kupoteza uhai.

c. Magonjwa .
i.Magonjwa ya moyo.
ii.Ugonjwa sugu wa kongosho.
iii.Ugonjwa wa ini kutokana na pombe, iv. Kansa
v.Uharibifu kwa mfumo mkuu wa neva na mfumo wa neva za pembeni.Hii inaweza kusababishwa matumizi kila mara ya pombe na hatimaye kifo.Matumizi ya pombe kupita kiasi kwa muda mrefu yanaweza kuharibu takribani kila kiungo na mfumo katika mwili.Ubongo unaokua wa kijana aliyebaleghe huwa hasa katika hatari kubwa ya kudhurika na sumu ya pombe.

5. Ulaji wa vyakula vya viwandani.
Mara nyingi vyakula hivi havina faida yeyote mwilini na hivyo huitwa junk foods.Ni vitamu sana,na vimetengezwa hivyo ili watu watamani kuvila.Vyakula hivi ni hatari sana kwa afya zetu,na hivyo ni vema tukaviepuka kabisa.Vyakula hivi huleta magonjwa mengi kama kisukari,magonjwa ya moyo,pressure,cancer nk.

Kuna wale ambao mara nyingi wamekuwa wakila vyakula vya makopo ambavyo vinapotumiwa mara kwa mara huweza kuwa na madhara kadhaa,yakiwemo tatizo la saratani. Hivyo kundi hili nalo linaweza kuwa katika hatari ya kupoteza maisha kabla ya siku zao.

6.Kuishi bila Mungu.
Hatuna budi kama binadamu kukumbuka kwamba sisi ni viumbe vya Mungu na kwamba Mungu ametuumba kwa makusudi ya kumuabudu na kutimiza malengo yake kwa wanadamu wengine. Kama tusipofanya hivyo,hakuna sababu yeyote ya sisi kuendelea kuishi duniani,kwa hiyo Mungu huondoa ulinzi wake.

Katika mazingira hayo, Shetani husitisha uhai wetu kwa njia yeyote anayo ona inafaa.Hata hivyo Mungu ni mvumilivu sana,tukigeuka na kuacha uovu wetu,yeye ni muamifu na wa kutegewa,na atatusamehe uovu wetu wote.
 
Stayfar
Samahani,hata kama hupendi,lakini ni pombe yeyote mkuu.Labda umekulia kwenye makabila au dini ambazo zimehalalisha pombe,lakini hiyo haina maana kwamba ni halali.Kumbuka kwamba,ipo njia ionekayo machoni pa mtu kuwa sawa,lakini mwisho wake ni mauti.
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya dalili na tabia.
Nikajua mtu anaekaribia kufa anaanza kupoteza kumbukumbu, haongei sana, kucha zinabadilika rangi, ngozi inaanza kuwa kavu, anakosa usingizi n.k.

Sasa wewe umeelezea tabia, inamaana walevi wote wana maisha mafupi? Wavuta sigara, wazinzi, wasioamcha Mungu, wote hao wana maisha mafupi?

Na huko kanisani au wasiokunywa pombe au wanaojitenga na starehe hawafi mapema?
 
Sasa watanzania pekee ndio wanaoishi haya maisha???

This thread is irrevelant..
Ni irrelevant kwako,kwa kuwa labda umetopea kwenye uovu,lakini naamini the thread is relevant to a lot of people.Sijasema kwenye bandiko langu popote kwamba Watanzania ndio peke yao wanaoishi haya maisha,this is a general out look.
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya dalili na tabia.
Nikajua mtu anaekaribia kufa anaanza kupoteza kumbukumbu, haongei sana, kucha zinabadilika rangi, ngozi inaanza kuwa kavu, anakosa usingizi n.k.

Sasa wewe umeelezea tabia, inamaana walevi wote wana maisha mafupi? Wavuta sigara, wazinzi, wasioamcha Mungu, wote hao wana maisha mafupi?

Na huko kanisani au wasiokunywa pombe au wanaojitenga na starehe hawafi mapema?
Nilicho andika ni sahihi kabisa.Chunguza Watu wanaokufa mapema wana tabia gani,and come back to me.I have done it na nimeona ni kweli.Even the Bible says sin kills.
 
Pombe ilihalalishwa katika dini ya Kiyahudi.
Unasemaje kuhusu hilo?
Samahani,hata kama hupendi,lakini ni pombe yeyote mkuu.Labda umekulia kwenye makabila au dini ambazo zimehalalisha pombe,lakini hiyo haina maana kwamba ni halali.Kumbuka kwamba,ipo njia ionekayo machoni pa mtu kuwa sawa,lakini mwisho wake ni mauti.
 
Mkuu hizi ni dalili au tabia?

Pia unawezaje kusema au kudhani mtu fulani atakufa mapema eti kisa ana tabia fulani fulani? Unapata wapi huo ujasiri Mkuu?

Kifo hakina formula mkuu,kinaweza kukupitia wewe ukiwa umelala zako ndani na kikawaacha salama wana wanaopiga Masanga Pub muda huo. Kinaweza kikamjeruhi bodaboa anaedrive hovyo na kumuua mtembea kwa miguu anaezingatia sheria/taratibu zote.

Wapo walio kuwa ni wakemeaji wazuri wa hayo tunayoyaita maovu mfano: Sigara na Pombe ila ajabu wao ndio walianza kufa na hao walevi na wavuta sigara wakawazika.

So linapofikia suala la kifo liache tu kwasababu si mimi wala wewe ambaeanajua atakufaje.
 
Ujasiri naupata wapi?!Kifo ni matokeo ya tabia zetu mkuu.Na hiyo inaweza kuwa dalili au tabia,what ever you want to call it.Hivi unataka kuniambia tabia ya uasherati haina consequences kweli.Si katika uasherati wako unaweza kukutana na Ukimwi.Na ulevi je,si unaweza ukapata ugonjwa wa ini.Mkuu tabia yeyote mbaya inakupeleka kaburini mapema,huo ndio ukweli,whether we like it or not.Dawa ni kuepuka uovu.
 
Ujasiri naupata wapi?!Kifo ni matokeo ya tabia zetu mkuu.Na hiyo inaweza kuwa dalili au tabia,what ever you want to call it.Hivi unataka kuniambia tabia ya uasherati haina consequences kweli.Si katika uasherati wako inaweza kukutana na Ukimwi.Na ulevi je,si unaweza ukapata ugonjwa wa ini.Mkuu tabia yeyote mbaya inakupeleka kaburini mapema,huo ndio ukweli,whether we like it or not.Dawa ni kuepuka uovu.

Sijapinga hiyo nadharia ya kwamba tabia hatarashi huweza kupelekea kifo(kumbuka;hata matendo mema hupelekea kifo), ila tu napingana na ufafanunuzi wako hapo juu. Katika ufafanunuzi wako ni wazi umeonyesha kuwa watu wenye tabia hizi wapo hatarini kufariki mapema zaidi ya wasio na tabia hizi.

Kifo hakina hodi mkuu,kinamkuta mwanadamu yeyote yule muda wowote ule haijalishi unalewa au hulewi,unazini au huzini una vuta sigara au huvuti.

Kifo ni fumbo kubwa sana.
 
Mkuu hizi ni dalili au tabia?
Pia unawezaje kusema au kudhani mtu fulani atakufa mapema eti kisa ana tabia fulani fulani? Unapata wapi huo ujasiri Mkuu?
Kifo hakina formula mkuu,kinaweza kukupitia wewe ukiwa umelala zako ndani na kikawaacha salama wana wanaopiga Masanga Pub muda huo. Kinaweza kikamjeruhi bodaboa anaedrive hovyo na kumuua mtembea kwa miguu anaezingatia sheria/taratibu zote.
Wapo walio kuwa ni wakemeaji wazuri wa hayo tunayoyaita maovu mfano: Sigara na Pombe ila ajabu wao ndio walianza kufa na hao walevi na wavuta sigara wakawazika.

So linapofikia suala la kifo liache tu kwasababu si mimi wala wewe ambaeanajua atakufaje.
Unaweza kupanga kifo chako kwa tabia zako mkuu,change your mind set.Mtu unaendesha gari umelewa halafu eti useme hujapanga kifo chako!Au unafanya uasherati na kila mwanamke you find around halafu eti useme hujapanga kifo chako!You eat junk food halafu wewe kila siku uko mbele ya TV screen,huna mazoezi yeyote halafu utuambie hujapanga kifo chako.No let us change our mind set, vifo vingi tunavitengeneza wenyewe,let's wake up.
 
Sijapinga hiyo nadharia ya kwamba tabia hatarashi huweza kupelekea kifo(kumbuka;hata matendo mema hupelekea kifo), ila tu napingana na ufafanunuzi wako hapo juu. Katika ufafanunuzi wako ni wazi umeonyesha kuwa watu wenye tabia hizi wapo hatarini kufariki mapema zaidi ya wasio na tabia hizi.
Kifo hakina hodi mkuu,kinamkuta mwanadamu yeyote yule muda wowote ule haijalishi unalewa au hulewi,unazini au huzini una vuta sigara au huvuti.

Kifo ni fumbo kubwa sana.
Napenda Watu waelewe jambo hili,kwamba Mungu amepangia kila mtu majira na nyakati ambapo atakufa.Sasa tunaweza kujiletea kifo mapema kwa kuishi maisha yasiyo faa.This is what I am talking about.
 
Back
Top Bottom