Kwa kawaida maisha ya binadamu mwisho wake huwa ni kufa,kwa hiyo kila mwenye pumzi ni lazima siku moja ataonja mauti.Hata hivyo wapo watu wengi wanaokufa mapema na kijinga kabla ya muda aliopanga Mungu.
Kuna viashiria fulani ambavyo huweza kuonyesha kwamba watu fulani huenda wakapoteza maisha mapema kutokana na mfumo wao wa maisha.
Miongoni mwa dalili ambazo huweza kuashiria kwamba mhusika anaweza kuwa na maisha mafupi duniani ni pamoja na hizi zifuatazo.
1.Watu wanaopenda anasa na starehe.
Watu wa aina hii huwa katika hatari ya kupoteza maisha haraka hata kabla ya siku zao kutokana na kuwa na hatari kubwa ya kupatwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo yatokanayo na zinaa.Hatuna budi pia kukumbuka kwamba dhambi inaua.
2. Wavutaji wa sigara.
Watu wanaovuta
Watu wanaovuta sigara huwa katika hatari ya kuishi maisha mafupi zaidi kuliko wale ambao hawatumii sigara kwani watu wa aina hii huwa katika hatari ya kukumbwa na magonjwa kama saratani,kisukari,magonjwa ya moyo nk. ambayo huweza kukatisha uhai wa mhusika hata kabla ya siku zake.
3. Kutofanya mazoezi au kukaa bila kazi
Watu ambao huwa miili yao haina mazoezi kabisa nao huwa katika hatari ya kupoteza maisha mapema kutokana na kushambuliwa na magonjwa yasiyoambukiza kama vile shinikizo la damu, kisukari nk.
4. Unywaji wa pombe.
Watumiaji wa vileo na huwa katika hatari ya kupoteza maisha yao mapema kutokana na mambo matatu makuu.
a) Kupata ajali kutokana na kutumia vyombo vya moto wakati wakiwa wamelewa na baadaye kujikuta wanapoteza maisha.
b) Ugomvi ambao huweza kuibuka kutokana na mihemko ya vilevi wanavyokuwa wamekunywa na kuweza kusababisha ugomvi mkubwa. Mfano kupigana na chupa na baadaye kupoteza uhai.
c. Magonjwa .
i.Magonjwa ya moyo.
ii.Ugonjwa sugu wa kongosho.
iii.Ugonjwa wa ini kutokana na pombe, iv. Kansa
v.Uharibifu kwa mfumo mkuu wa neva na mfumo wa neva za pembeni.Hii inaweza kusababishwa matumizi kila mara ya pombe na hatimaye kifo.Matumizi ya pombe kupita kiasi kwa muda mrefu yanaweza kuharibu takribani kila kiungo na mfumo katika mwili.Ubongo unaokua wa kijana aliyebaleghe huwa hasa katika hatari kubwa ya kudhurika na sumu ya pombe.
5. Ulaji wa vyakula vya viwandani.
Mara nyingi vyakula hivi havina faida yeyote mwilini na hivyo huitwa junk foods.Ni vitamu sana,na vimetengezwa hivyo ili watu watamani kuvila.Vyakula hivi ni hatari sana kwa afya zetu,na hivyo ni vema tukaviepuka kabisa.Vyakula hivi huleta magonjwa mengi kama kisukari,magonjwa ya moyo,pressure,cancer nk.
Pata taarifa zaidi kutoka kwenye link ifuatayo.
https://sw.hesperian.org/hhg/New_Where_There_Is_No_Doctor:Vyakula_vipya,_matatizo_mapyamapya
Kuna wale ambao mara nyingi wamekuwa wakila vyakula vya makopo ambavyo vinapotumiwa mara kwa mara huweza kuwa na madhara kadhaa,yakiwemo tatizo la saratani. Hivyo kundi hili nalo linaweza kuwa katika hatari ya kupoteza maisha kabla ya siku zao.
6.Kuishi bila Mungu.
Hatuna budi kama binadamu kukumbuka kwamba sisi ni viumbe vya Mungu na kwamba Mungu ametuumba kwa makusudi ya kumuabudu na kutimiza malengo yake kwa wanadamu wengine. Kama tusipofanya hivyo,hakuna sababu yeyote ya sisi kuendelea kuishi duniani,kwa hiyo Mungu huondoa ulinzi wake.
Katika mazingira hayo, Shetani husitisha uhai wetu kwa njia yeyote anayo ona inafaa.Hata hivyo Mungu ni mvumilivu sana,tukigeuka na kuacha uovu wetu,yeye ni muamifu na wa kutegewa,na hivyo hutusamehe uovu wetu wote.