PostGE2025 Zitto aangukia Pua, Mahakama yasema Baba Levo hana kesi ya kujibu

PostGE2025 Zitto aangukia Pua, Mahakama yasema Baba Levo hana kesi ya kujibu

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Kigoma muda mfupi uliopita leo, Alhamisi tarehe 16/07/2026 Mahakama imeifuta kesi ya uchaguzi iliyokuwa imefunguliwa Mahakamani hapo na wananchi wanne (4) waliojitambulisha kuwa wapiga kura wa Jimbo la Kigoma Mjini dhidi ya Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini (CCM) Clayton Revocatus Chipando (Baba Levo).

1784192343382.png

Uamuzi uliosomwa Mahakamani hapo leo na Jaji Victoria Nongwa aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo iliyokuwa inapinga uhalali wa 'Ubunge wa Baba Levo' amesema hoja zote zilizoletwa na walalamikaji ikiwemo hoja za utekaji, madai ya rushwa, udini nk, zimeshindwa kuishawishi Mahakama moja kwa moja kukubaliana kutokana na kwamba ushahidi uliowasilishwa Mahakamani hapo umekosa mashiko.

Mahakama imesema kutokana na dosari kadhaa zilizobainishwa na Mahakama kutoka kwa walalamikaji ambao ni wanachama wa ACT Wazalendo, ushahidi uliowasilishwa Mahakamani hapo haina mashiko na kwamba walalamikiwa wote ikiwemo INEC hawana kesi ya kujibu.

Via: Jambo TV
 
Kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Kigoma muda mfupi uliopita leo, Alhamisi tarehe 16/07/2026 Mahakama imeifuta kesi ya uchaguzi iliyokuwa imefunguliwa Mahakamani hapo na wananchi wanne (4) waliojitambulisha kuwa wapiga kura wa Jimbo la Kigoma Mjini dhidi ya Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini (CCM) Clayton Revocatus Chipando (Baba Levo)

Uamuzi uliosomwa Mahakamani hapo leo na Jaji Victoria Nongwa aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo iliyokuwa inapinga uhalali wa 'Ubunge wa Baba Levo' amesema hoja zote zilizoletwa na walalamikaji ikiwemo hoja za utekaji, madai ya rushwa, udini nk, zimeshindwa kuishawishi Mahakama moja kwa moja kukubaliana kutokana na kwamba ushahidi uliowasilishwa Mahakamani hapo umekosa mashiko

Mahakama imesema kutokana na dosari kadhaa zilizobainishwa na Mahakama kutoka kwa walalamikaji ambao ni wanachama wa ACT Wazalendo, ushahidi uliowasilishwa Mahakamani hapo haina mashiko na kwamba walalamikiwa wote ikiwemo INEC hawana kesi ya kujibu
well done mahakama huru ya Tanzania. Well done wananchi wote kwa kuziamini na kuzitumia vyema mahakama huru za Tanzania katika kutafuta haki zenu.🐒
 
Kesi imefutwa mahakamani. Ushahidi umeonyesha hana kesi ya kujibu.
👇
 

Attachments

  • 20260716_121221.jpg
    20260716_121221.jpg
    245.2 KB · Views: 17
Zitto ni mtu mnafiki sana.

Watu walipokua wanadai reforms alisema kauli ya "mhuni hasusiwi" & "Linda Kura" akaenda mbali na kumhujumu Mpina ili avute pesa za udalali maana walijua fika Mpina amehamia mwezi chini ya mmoja hawezi kugombea urais wakaunda genge akawekewa pingamizi ili Samuya abaki pekeyake na Zitto akageuka na kauli ya kura za ubunge kwa Zitto na urais kwa Samuya kwa ufupi Zitto akaanza kumpigia kampeni Samuya.
 
CCM wakishakutumia wanakutupa kama toilet paper. Zitto alipokubali tuu kutoa bei "Price tag" around 2014, nilijua mwisho wake kisiasa umefika.
Muda unatabia ya kuhukumu kwa haki; leo Zitto ni wa kushindwa ubunge na huyo Comedian na kula zaidi ya nusu! 😆
 
well done mahakama huru ya Tanzania. Well done wananchi wote kwa kuziamini na kuzitumia vyema mahakama huru za Tanzania katika kutafuta haki zenu.🐒
Hivi mahakama zinakuwaje huru wakati majaji wanateuliwa na mwenyekiti wa chama tawala?
Anyways, kwa kuwa kwa sasa upo upande wa wanyongaji huwezi kujibu.
 
Back
Top Bottom