PostGE2025 Zitto aangukia Pua, Mahakama yasema Baba Levo hana kesi ya kujibu

PostGE2025 Zitto aangukia Pua, Mahakama yasema Baba Levo hana kesi ya kujibu

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Hivi mahakama zinakuwaje huru wakati majaji wanateuliwa na mwenyekiti wa chama tawala?
Anyways, kwa kuwa kwa sasa upo upande wa wanyongaji huwezi kujibu.
Gentleman,
ni nchi ipi huru duniani ambako majaji wanajiteua wenyewe na ambako hawateuliwi na utawala?

hebu waeleze wadau wa Jf hayo maajabu na huo muujiza gentleman, nadhani itapendeza zaidi 🐒
 
Kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Kigoma muda mfupi uliopita leo, Alhamisi tarehe 16/07/2026 Mahakama imeifuta kesi ya uchaguzi iliyokuwa imefunguliwa Mahakamani hapo na wananchi wanne (4) waliojitambulisha kuwa wapiga kura wa Jimbo la Kigoma Mjini dhidi ya Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini (CCM) Clayton Revocatus Chipando (Baba Levo).


Uamuzi uliosomwa Mahakamani hapo leo na Jaji Victoria Nongwa aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo iliyokuwa inapinga uhalali wa 'Ubunge wa Baba Levo' amesema hoja zote zilizoletwa na walalamikaji ikiwemo hoja za utekaji, madai ya rushwa, udini nk, zimeshindwa kuishawishi Mahakama moja kwa moja kukubaliana kutokana na kwamba ushahidi uliowasilishwa Mahakamani hapo umekosa mashiko.

Mahakama imesema kutokana na dosari kadhaa zilizobainishwa na Mahakama kutoka kwa walalamikaji ambao ni wanachama wa ACT Wazalendo, ushahidi uliowasilishwa Mahakamani hapo haina mashiko na kwamba walalamikiwa wote ikiwemo INEC hawana kesi ya kujibu.

Via: Jambo TV

Kaangukia pua kwa uchaguzi upi....!? Huu huu wa MO29 au kulikuwa na uchaguzi mwingine?
 
Back
Top Bottom