GE2025 Zitto ashikiliwa na Polisi usiku wa manane Lindi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Chama cha ACT Wazalendo kimetoa taarifa kali ya kulaani kile kinachodaiwa kuwa ni uvamizi na kushikiliwa kwa muda kwa Kiongozi wake wa Chama Mstaafu, Zitto Zuberi Kabwe, na maofisa wa Jeshi la Polisi usiku wa tarehe 14 Julai 2025, akiwa katika hoteli mkoani Lindi

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Tanzania Bara, Ester Thomas, tukio hilo lilitokea majira ya saa sita usiku, ambapo polisi kutoka wilaya na mkoa wa Lindi waliwasili katika hoteli aliyofikia Zitto na baadaye kumpeleka katika kituo cha polisi kwa mahojiano ya zaidi ya nusu saa, pasipo kufahamisha mara moja kosa lake

“Hatimaye, baada ya majibizano ya muda mrefu, polisi, majira ya saa saba na dakika nane usiku, walieleza na kubainisha kwamba wanamshikilia Kiongozi wa Chama Mstaafu kwa kosa la kutoa kauli za vitisho, kwa mujibu wa kifungu cha 89(2) cha sheria ya makosa ya jinai. Polisi hao walieleza kwamba kauli hizo za vitisho zilitokana na hotuba ya Ndugu Zitto Kabwe aliyoitoa siku ya tarehe 10/07/2025, akiwa kwenye mkutano wa hadhara Tunduru Kaskazini”, imeeleza taarifa hiyo

Zitto Kabwe ameeleza kuwa atatoa maelezo yote mahakamani na alikataa kueleza zaidi kwa polisi, akisisitiza kuwa hiyo ni haki yake ya kisheria. Aliachwa huru majira ya saa nane usiku bila masharti yoyote

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni, Zitto alitoa onyo kali kwa maafisa wa polisi na watendaji wengine wa serikali wanaoshiriki katika kile alichokiita uingizaji wa kura bandia kwenye uchaguzi, akisema chama hicho hakitasita kuchukua hatua hata kama mhusika ni askari wa vyombo vya ulinzi na usalama, onyo ambalo baadhi ya wachambuzi na wafuatiliaji wa masuala ya siasa wamelieleza kuwa ndiyo huenda imesababisha Zitto kuhojiwa Polisi

Akihutubia siku ya Alhamisi Julai 10, 2025 katika Jimbo la Tunduru Kaskazini, wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Zitto alieleza kuwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024, ACT Wazalendo ilimkamata afisa wa polisi akiwa amepakia kura bandia kwa lengo la kuzisambaza kwenye kituo cha kupigia kura, akisisitiza kuwa chama hicho hakitavumilia tena majaribio yoyote ya kuvuruga uchaguzi kwa ‘mbinu chafu’ kama hizo

View attachment 3405408
View attachment 3405409
Soma pia: Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

​
Drama tu hizi
 
Kwa sasa tupo na hili la HPP tutarejea hivi punde.
 
Wote mliosema Act ni CCM B ni sawa, mliosema simba hang'ati mkia wake ni sawa, mliosema ni drama maigizo ni sawa
Na mimi nasema Zito siyo mpinzani.
Naongezea mlamba asali hang'ati kidole chake. Wanatafuta mifano ya kuulia wapinzani halisi.
 
Policcm wanapaswa wamkamate hata kiongozi mwanaccm mmoja kwa drama kisha wamuachie ili ionekane wamebalansi maana kwa hali ilivyo sasa hata mtoto wa chekechea ameaminishwa kuwa upinzani kwenye hii nchi ni uasi na ugaidi!
 
Chama cha ACT Wazalendo kimetoa taarifa kali ya kulaani kile kinachodaiwa kuwa ni uvamizi na kushikiliwa kwa muda kwa Kiongozi wake wa Chama Mstaafu, Zitto Zuberi Kabwe, na maofisa wa Jeshi la Polisi usiku wa tarehe 14 Julai 2025, akiwa katika hoteli mkoani Lindi

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Tanzania Bara, Ester Thomas, tukio hilo lilitokea majira ya saa sita usiku, ambapo polisi kutoka wilaya na mkoa wa Lindi waliwasili katika hoteli aliyofikia Zitto na baadaye kumpeleka katika kituo cha polisi kwa mahojiano ya zaidi ya nusu saa, pasipo kufahamisha mara moja kosa lake

“Hatimaye, baada ya majibizano ya muda mrefu, polisi, majira ya saa saba na dakika nane usiku, walieleza na kubainisha kwamba wanamshikilia Kiongozi wa Chama Mstaafu kwa kosa la kutoa kauli za vitisho, kwa mujibu wa kifungu cha 89(2) cha sheria ya makosa ya jinai. Polisi hao walieleza kwamba kauli hizo za vitisho zilitokana na hotuba ya Ndugu Zitto Kabwe aliyoitoa siku ya tarehe 10/07/2025, akiwa kwenye mkutano wa hadhara Tunduru Kaskazini”, imeeleza taarifa hiyo

Zitto Kabwe ameeleza kuwa atatoa maelezo yote mahakamani na alikataa kueleza zaidi kwa polisi, akisisitiza kuwa hiyo ni haki yake ya kisheria. Aliachwa huru majira ya saa nane usiku bila masharti yoyote

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni, Zitto alitoa onyo kali kwa maafisa wa polisi na watendaji wengine wa serikali wanaoshiriki katika kile alichokiita uingizaji wa kura bandia kwenye uchaguzi, akisema chama hicho hakitasita kuchukua hatua hata kama mhusika ni askari wa vyombo vya ulinzi na usalama, onyo ambalo baadhi ya wachambuzi na wafuatiliaji wa masuala ya siasa wamelieleza kuwa ndiyo huenda imesababisha Zitto kuhojiwa Polisi

Akihutubia siku ya Alhamisi Julai 10, 2025 katika Jimbo la Tunduru Kaskazini, wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Zitto alieleza kuwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024, ACT Wazalendo ilimkamata afisa wa polisi akiwa amepakia kura bandia kwa lengo la kuzisambaza kwenye kituo cha kupigia kura, akisisitiza kuwa chama hicho hakitavumilia tena majaribio yoyote ya kuvuruga uchaguzi kwa ‘mbinu chafu’ kama hizo

View attachment 3405408
View attachment 3405409
Soma pia: Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

​
Mambo ni moto unapoona CHADEMA wanasema No Reform No Electio kuna jambo,Zito endelea kupambana tuone kama utashinda sifa ya unafiki Tanzania.
 
Policcm wanapaswa wamkamate hata kiongozi mwanaccm mmoja kwa drama kisha wamuachie ili ionekane wamebalansi maana kwa hali ilivyo sasa hata mtoto wa chekechea ameaminishwa kuwa Wapinzani ndo maadui wa taifa.
Na huu ndiyo ugonjwa unaoligharimu taifa letu
 
Back
Top Bottom