GE2025 Zitto ashikiliwa na Polisi usiku wa manane Lindi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Chama cha ACT Wazalendo kimetoa taarifa kali ya kulaani kile kinachodaiwa kuwa ni uvamizi na kushikiliwa kwa muda kwa Kiongozi wake wa Chama Mstaafu, Zitto Zuberi Kabwe, na maofisa wa Jeshi la Polisi usiku wa tarehe 14 Julai 2025, akiwa katika hoteli mkoani Lindi

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Tanzania Bara, Ester Thomas, tukio hilo lilitokea majira ya saa sita usiku, ambapo polisi kutoka wilaya na mkoa wa Lindi waliwasili katika hoteli aliyofikia Zitto na baadaye kumpeleka katika kituo cha polisi kwa mahojiano ya zaidi ya nusu saa, pasipo kufahamisha mara moja kosa lake

“Hatimaye, baada ya majibizano ya muda mrefu, polisi, majira ya saa saba na dakika nane usiku, walieleza na kubainisha kwamba wanamshikilia Kiongozi wa Chama Mstaafu kwa kosa la kutoa kauli za vitisho, kwa mujibu wa kifungu cha 89(2) cha sheria ya makosa ya jinai. Polisi hao walieleza kwamba kauli hizo za vitisho zilitokana na hotuba ya Ndugu Zitto Kabwe aliyoitoa siku ya tarehe 10/07/2025, akiwa kwenye mkutano wa hadhara Tunduru Kaskazini”, imeeleza taarifa hiyo

Zitto Kabwe ameeleza kuwa atatoa maelezo yote mahakamani na alikataa kueleza zaidi kwa polisi, akisisitiza kuwa hiyo ni haki yake ya kisheria. Aliachwa huru majira ya saa nane usiku bila masharti yoyote

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni, Zitto alitoa onyo kali kwa maafisa wa polisi na watendaji wengine wa serikali wanaoshiriki katika kile alichokiita uingizaji wa kura bandia kwenye uchaguzi, akisema chama hicho hakitasita kuchukua hatua hata kama mhusika ni askari wa vyombo vya ulinzi na usalama, onyo ambalo baadhi ya wachambuzi na wafuatiliaji wa masuala ya siasa wamelieleza kuwa ndiyo huenda imesababisha Zitto kuhojiwa Polisi

Akihutubia siku ya Alhamisi Julai 10, 2025 katika Jimbo la Tunduru Kaskazini, wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Zitto alieleza kuwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024, ACT Wazalendo ilimkamata afisa wa polisi akiwa amepakia kura bandia kwa lengo la kuzisambaza kwenye kituo cha kupigia kura, akisisitiza kuwa chama hicho hakitavumilia tena majaribio yoyote ya kuvuruga uchaguzi kwa ‘mbinu chafu’ kama hizo

View attachment 3405408
View attachment 3405409
Soma pia: Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

​
Huyo wampige mit tu
 
Policcm wanapaswa wamkamate hata kiongozi mwanaccm mmoja kwa drama kisha wamuachie ili ionekane wamebalansi maana kwa hali ilivyo sasa hata mtoto wa chekechea ameaminishwa kuwa upinzani kwenye hii nchi ni uasi na ugaidi!

..wamewatesa Chadema kupita kiasi.

..haiwezekani tena kufanya mchezo wa ku-balance.

..uta-balance vipi wakati Chadema wametekwa, wameuwawa, wamefunguliwa makesi mabaya?

..kuna mwana-Ccm yuko tayari kufunguliwa kesi ya uhaini, au ugaidi, ili ku-balance?
 
Kwa muda, halafu simu moja tu. Mwachieni Mara moja.
Huyo ni mtu wetu.
 
Chama cha ACT Wazalendo kimetoa taarifa kali ya kulaani kile kinachodaiwa kuwa ni uvamizi na kushikiliwa kwa muda kwa Kiongozi wake wa Chama Mstaafu, Zitto Zuberi Kabwe, na maofisa wa Jeshi la Polisi usiku wa tarehe 14 Julai 2025, akiwa katika hoteli mkoani Lindi

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Tanzania Bara, Ester Thomas, tukio hilo lilitokea majira ya saa sita usiku, ambapo polisi kutoka wilaya na mkoa wa Lindi waliwasili katika hoteli aliyofikia Zitto na baadaye kumpeleka katika kituo cha polisi kwa mahojiano ya zaidi ya nusu saa, pasipo kufahamisha mara moja kosa lake

“Hatimaye, baada ya majibizano ya muda mrefu, polisi, majira ya saa saba na dakika nane usiku, walieleza na kubainisha kwamba wanamshikilia Kiongozi wa Chama Mstaafu kwa kosa la kutoa kauli za vitisho, kwa mujibu wa kifungu cha 89(2) cha sheria ya makosa ya jinai. Polisi hao walieleza kwamba kauli hizo za vitisho zilitokana na hotuba ya Ndugu Zitto Kabwe aliyoitoa siku ya tarehe 10/07/2025, akiwa kwenye mkutano wa hadhara Tunduru Kaskazini”, imeeleza taarifa hiyo

Zitto Kabwe ameeleza kuwa atatoa maelezo yote mahakamani na alikataa kueleza zaidi kwa polisi, akisisitiza kuwa hiyo ni haki yake ya kisheria. Aliachwa huru majira ya saa nane usiku bila masharti yoyote

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni, Zitto alitoa onyo kali kwa maafisa wa polisi na watendaji wengine wa serikali wanaoshiriki katika kile alichokiita uingizaji wa kura bandia kwenye uchaguzi, akisema chama hicho hakitasita kuchukua hatua hata kama mhusika ni askari wa vyombo vya ulinzi na usalama, onyo ambalo baadhi ya wachambuzi na wafuatiliaji wa masuala ya siasa wamelieleza kuwa ndiyo huenda imesababisha Zitto kuhojiwa Polisi

Akihutubia siku ya Alhamisi Julai 10, 2025 katika Jimbo la Tunduru Kaskazini, wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Zitto alieleza kuwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024, ACT Wazalendo ilimkamata afisa wa polisi akiwa amepakia kura bandia kwa lengo la kuzisambaza kwenye kituo cha kupigia kura, akisisitiza kuwa chama hicho hakitavumilia tena majaribio yoyote ya kuvuruga uchaguzi kwa ‘mbinu chafu’ kama hizo

View attachment 3405408
View attachment 3405409
Soma pia: Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

​
Geresha
 
View attachment 3405414View attachment 3405416View attachment 3405418
Kiongozi mstaafu wa Chama, ndugu Zitto Zuberi Kabwe, amedaiwa kukamatwa na polisi saa 6 usiku wa kuamkia Julai 14, 2025 na kisha kupelekwa kituo cha polisi Wilaya ya Lindi, lakini baadaye aliachiliwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, John Imori alipotafutwa kwa simu kuzungumzia suala hilo, hakupatikana, lakini taarifa ya ACT Wazalendo imesema Zitto amedaiw akutoa kauli za vitisho katika hotuba yake aliyoitoa Julai 10 akiwa kwenye mkutano wa hadhara Tunduru Kaskazini Mkoa wa Ruvuma.

Taarifa hiyo iliyotolewa”

kupitia mtandao wa X leo Julai 14 imesema askari polisi walivamia hoteli aliyokuwa amefikia Zitto na kujaribu kumkamata.

“Baada ya purukushani katika hoteli hiyo, Ndugu Zitto Kabwe alienda katika kituo cha polisi cha wilaya ya Lindi, huku akiongozana na polisi, wanachama na mwanasheria wa chama. Kwa zaidi ya dakika 30, Kiongozi wa Chama Mstaafu alizongwa na polisi hao pasipo kuelezwa anashikiliwa kwa kosa gani.

“Hatimaye, baada ya majibizano ya muda mrefu, polisi, majira ya saa saba na dakika nane usiku, walieleza na kubainisha kwamba wanamshikilia Kiongozi wa Chama Mstaafu kwa kosa la kutoa kauli za vitisho, kwa mujibu wa kifungu cha 89(2) cha sheria ya makosa ya jinai. Polisi hao walieleza kwamba kauli hizo za vitisho zilitokana na hotuba ya Ndugu Zitto Kabwe aliyoitoa siku ya tarehe 10/07/2025, akiwa kwenye mkutano wa hadhara Tunduru Kaskazini.”

Taarifa hiyo imesema, Zitto alitoa taarifa binafsi na kueleza kuwa maelezo mengine yote atayatoa mahakamani.

“Licha ya kueleza hivyo, polisi waliendelea kumzonga wakimtaka kiongozi afafanue ya kwamba alimaanisha nini katika hotuba yake. Hata hivyo, Ndugu Zitto Kabwe alisisitiza kwamba kama atahitajika kutoa maelezo hayo mahakamani, basi atafanya hivyo, na si vinginevyo. Hatimaye, majira ya saa nane ndugu Zitto aliachiwa kutoka kituoni hapo pasipo masharti yeyote yale.

“Chama cha ACT Wazalendo tunatangaza kwa msisitizo mkubwa, hatuko tayari kuendelea kuona misingi ya haki inakiukwa na kuendelea kushuhudia nchi yetu inaendeshwa kihuni na genge la wahuni wachache. Tunakemea na tutakemea uhuni na ukiukwaji wote wa haki kwa maneno na kwa vitendo.”
Geresha .......spinning
 
Huyu hakushikiliwa bali alichukuliwa akapewe maagizo mapya. Simba hang'ati mkia wake hata awe mkali namna gani.
Hahaha hata mimi instincts zangu zinanieleza kabisa kuwa hili ni igizo kubalance mambo🤣🤣
 
mwami hana faida yeyote kwenye hii nchi, ni msaliti na hata huko kushikiliwa hatuamini kama kweli ameshikiliwa au anatengeneza tukio pamoja na watawala ili kutupoteza ramani ya kupigania haki au ili na yeye aonekana anafanya kitu. mpotezeeni. zito ni mdini, na wakati gwajima anafungikwa kanisa, badala ya kujadili hoja za kupoteza na kuuawa watu yeye alianza kujadili ramani ya Israel madhabahuni, na kuingiza kwamba gwajima ameweka bendera ya wauaji wa wapalestina madhabahuni, bila kujua makanisa mengi sana yana bendera hiyo. huyu hafai kwa lolote.
 
Chama cha ACT Wazalendo kimetoa taarifa kali ya kulaani kile kinachodaiwa kuwa ni uvamizi na kushikiliwa kwa muda kwa Kiongozi wake wa Chama Mstaafu, Zitto Zuberi Kabwe, na maofisa wa Jeshi la Polisi usiku wa tarehe 14 Julai 2025, akiwa katika hoteli mkoani Lindi

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Tanzania Bara, Ester Thomas, tukio hilo lilitokea majira ya saa sita usiku, ambapo polisi kutoka wilaya na mkoa wa Lindi waliwasili katika hoteli aliyofikia Zitto na baadaye kumpeleka katika kituo cha polisi kwa mahojiano ya zaidi ya nusu saa, pasipo kufahamisha mara moja kosa lake

“Hatimaye, baada ya majibizano ya muda mrefu, polisi, majira ya saa saba na dakika nane usiku, walieleza na kubainisha kwamba wanamshikilia Kiongozi wa Chama Mstaafu kwa kosa la kutoa kauli za vitisho, kwa mujibu wa kifungu cha 89(2) cha sheria ya makosa ya jinai. Polisi hao walieleza kwamba kauli hizo za vitisho zilitokana na hotuba ya Ndugu Zitto Kabwe aliyoitoa siku ya tarehe 10/07/2025, akiwa kwenye mkutano wa hadhara Tunduru Kaskazini”, imeeleza taarifa hiyo

Zitto Kabwe ameeleza kuwa atatoa maelezo yote mahakamani na alikataa kueleza zaidi kwa polisi, akisisitiza kuwa hiyo ni haki yake ya kisheria. Aliachwa huru majira ya saa nane usiku bila masharti yoyote

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni, Zitto alitoa onyo kali kwa maafisa wa polisi na watendaji wengine wa serikali wanaoshiriki katika kile alichokiita uingizaji wa kura bandia kwenye uchaguzi, akisema chama hicho hakitasita kuchukua hatua hata kama mhusika ni askari wa vyombo vya ulinzi na usalama, onyo ambalo baadhi ya wachambuzi na wafuatiliaji wa masuala ya siasa wamelieleza kuwa ndiyo huenda imesababisha Zitto kuhojiwa Polisi

Akihutubia siku ya Alhamisi Julai 10, 2025 katika Jimbo la Tunduru Kaskazini, wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Zitto alieleza kuwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024, ACT Wazalendo ilimkamata afisa wa polisi akiwa amepakia kura bandia kwa lengo la kuzisambaza kwenye kituo cha kupigia kura, akisisitiza kuwa chama hicho hakitavumilia tena majaribio yoyote ya kuvuruga uchaguzi kwa ‘mbinu chafu’ kama hizo

View attachment 3405408
View attachment 3405409
Soma pia: Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

​
Mmechelewa sana kuicheza hii Filamu ya CCM Serikali na ACT. Kwahiyo baada ya kuona EU inakaribia kuipiga Pini Tanzania kwa Suala la Tundu Lissu wa CHADEMA kwa Kuonewa Kwake pamoja na Manyanyaso kwa Chama chake cha CHADEMA mkaona sasa mtengeneze Picha ya kumkamata Zitto Kabwe ili kuonyesha kuwa si tu Lissu pekee na CHADEMA yake wanakamiwa bali ni Watu wa vyama vyote tu.

Kwa wenye Akili na tunaofuatilia mambo kwa ukaribu tunajua kuwa Zitto Kabwe huwa anaongea Kichochezi zaidi ya Tundu Lissu ila kwakuwa ni Mtu wenu na mnamtumia Kimkakati wala huwa hamumkamati.

Hovyoooooooooooooooooo.....!!!!!
 
Back
Top Bottom