Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 54,762
- 59,204
Hivi mlitaka Chama kiishije?Nimeshangazwa na majibu ya mkuu wa chama cha ACT Wazalendo ndugu Zitto Kabwe aliyoyatoa kwenye mtandao wa twitter.
Zitto alikuwa akimjibu mwananchi mmoja aliyekuwa akionyesha frustrations zake juu ya uamuzi wa chama cha ACT kujiunga na Serikali ya CCM huko Zanzibar katika kile kinachoitwa serikali ya umoja wa kitaifa. Mwananchi huyo anaonyesha kuwa kuingia kwa ACT katika hiyo serikali hakuwezi kusaidia wabanchi kupata uhuru mpana waliokuwa wakitamani kuwa nao.
Katika hali isiyo ya kawaida, isiyo ya uungwana na isiyo ya kiuongozi mkuu wa chama cha ACT ndugu Zitto badala ya kutumia fursa hiyo kumuelewesha au atleast akae kimya wananchi watumie haki yao ya kutoa maoni, yeye anamjibu kwa ufedhuli na jeuri kuwa "Kama unaona tumekosea basi anzisha chama chako".
Kwa kweli sikutegemea kiongozi haswa wa upinzani kutoa majibu ya nyodo kama haya kwa wananchi wanapouliza maswali ya msingi juu ya mienendo ya kisiasa nchini.
Labda Zitto afahamu tu kuwa sababu mojawapo ya leo ACT kuwa hapa ni haohao wananchi ambao leo anawajibu kwa nyodo kuwa "anzisheni chama chenu"
Lakini pia Zitto akumbuke kuwa kuna watu wamekifia hicho chama, Wakati akijibu kwa majibu ya "Anzisheni chama chenu" Je amelifikiria hili kuwa kuna watu wame-pay ultimate price kwa hicho chama au kwa course yake waliyoinadi kwao na kwa hiyo ndugu, jamaa, marafiki na wananchi wana haki ya kuhoji ukinyongakinyonga wa misimamo iliyowafanya hapo awali wawe tayari kukipigania hicho chama?
Lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida, Viongozi wa ACT sasa hivi wameacha kujibu maswali magumu ya wananchi juu ya hatua yao ya kuingia kwenye SUK wakati waliitangazia dunia na nchi kiujumla kuwa uchaguzi uliopita ulikuwa haramu, Zitto mwenyewe akaweka saini tamko la pamoja la Upinzani kuwa hawautambui uchaguzi ule pamoja na natunda yake, Sasa leo wananchi wakihoji wanaambiwa jamani eeh kama hamtaki tulichokifanya basi nendeni CCM, au NCCR yaani ni majibu ya kifedhuli uliopitiliza!. Sasa wameacha kutoa majibu kwa wananchi, wameanza kublackmail wanachama wa ACT na kutoa kauli za nyodo kwa wananchi, kuwa "ACT ina wenyewe na nyie kaanzisheni chama chenu"
Sasa leo tunaona kwa macho yetu, watu tuliodhani ni wakomavu wa kisiasa, tuliodhani kuwa mashambulizi yao kwa CCM basi wao labda wana ngozi ngumu na kwamba labda wao wakipewa nchi basi watakuwa humble, watakuwa na humility, watajibu hoja kwa hoja kumbe hawa jamaa ni arrogant(wenye viburi), intolerant(wasio wavumilivu) na wanajiona wao ni wamiliki wa taasisi kwa kuwa walizianzisha na si wahudumu tu wa taasisi ambao wao ni wanachama.
Hawa wapinzani hawana blank cheque ya kutuletea jeuri sisi wananchi, Kwa miaka mingi tumeuwa tukiishabumbulia CCM, lakini na wenyewe hawana impunity, tutawaekeza ukweli maana hivyo vyama kwa namba moja au nyingine vinanufaika kwa jasho la wananchi iwe kwa ruzuku au wanasiasa wao kulipwa kwa kodi za wananchi n.k
Zitto acha jeuri kwa wananchi, Jibu hoja na frustrations zao kwa hekima, utulivu, nidhamu na utu. Bila wananchi usingekuwa hapa kuwa na humility.
View attachment 1648516
Zitto pale katengeneza pesa ndefu sana.