Zitto ataka wanaoikosoa ACT-Wazalendo waanzishe chama chao

Zitto ataka wanaoikosoa ACT-Wazalendo waanzishe chama chao

Hawa hawa wananchi ambao wanalaumu huku Tanganyika ndio hata kwenye maandamano hawakuonekana.Kazi kukosoa watu kwenye keyboard tu, kujitokeza mbele hapana. Waacheni wanasiasa waamue yao maana hawakuungwa mkono na wanachama wao. Nao wameona labda walichofanya kwa kuitisha maandamano nyinyi wazee wa lawama mlikuwa hamkipendi kwa hiyo wamefata umoja na serikali labda ndio mnapenda. Ndio maana hamkuandamana wala kujitokeza kwa wingi kupiga kura. Mtu analaumu kwa mitandao unaweza kukuta hata kura hajapiga.
 
Labda unajidanganya wewe kiukweli mh.maalim seif amechoka kilichobaki ni ujuzi tu wa kisiasa kwani ujuzi hauzeeki

Si haba kutambua yafuatayo:

1. Ipo tofauti ya Seif na ACT kama chama. Kumbuka alipo, tupo!
2. Kipaumbele cha Seif ni Zanzibar. Yeye ni m-bara hadi ya Kigoma yamuumize kichwa?
3. Seif kaipambania Zanzibar maisha yake yote. Anaendelea kupambana na atapambana hadi kifo kimtenge!

Kuwahi kudhania kuwa Seif ni mjinga itakuwa ni kutojitendea haki kuliko pitiliza!
 
Yupo sahihi... Ni kama vile chama tawala vile huwezi kukupangia cha kufanya...




Cc: mahondaw
 
Hawa wapinzani hawana blank cheque ya kutuletea jeuri sisi wananchi, Kwa miaka mingi tumekuwa tukiishabumbulia CCM, lakini na wenyewe hawana impunity, tutawaekeza ukweli maana hivyo vyama kwa namba moja au nyingine vinanufaika kwa jasho la wananchi iwe kwa ruzuku au wanasiasa wao kulipwa kwa kodi za wananchi) hii sentesi ni ishara mbaya! Kumbe tz itaendelea kupambana na maadui wale wanne hata ikiwa kikongwe. (Ujinga, maradhi, umasikini, ....)
 
kwa kauli ya Zitto hapaswi kulaumiwa ya kusema asiyetaka akaanzishe chama kumbuka Zitto sasa yupo ndani ya ndoa hivyo hawezi tena toa kauli ya kuwatetea wapiga kura wake na pia kumbuka Zitto Kabwe amekataliwa na wana Kigoma kadri siku zinavyo enda Zitto anaanza rudi Lumumba na sisi wana Lumumba tunamkaribisha ata kama hata rudisha kadi basi mutarajie Zitto Kabwe kuunga juhudi au kusifu kazi za mzee.

Leo Zitto kawa MWEPESI SIO ZITTO TENA, KAKA ANGU ZITTO TANZANIA NI YA WOTE NAJUA KWA SASA WAJUTIA YALE MAMBO YA KUWASALITI WATANZANIA KULE WORD BANK LAKINI NJOO UTUBU TUJENGE TANZANIA
 
Zitto ameshafanya biashara hivyo kwake maisha kama kawa ni mtelezo.
 
Ona ulivyo fala wa kisiasa, yaani mtu akose hamu ya kula kwa kelele za wapuuzi kama wewe, unajua anaishi vipi? Mijinga kama wewe unakuta inashabikia Cdm hata kula tu shida alafu inabaki kuwaza maisha ya Zitto.

Nimecheka kwa nguvu, kilaza wa october 2020 umeingia kwa kasi ya ajabu. Umefunga turbo nini?
 
Pamoja na kwamba huwa simpendi Zitto, naunga mkono majibu aliyotoa. Ninyi mnaojifanya wajuaji mitandaoni anzisheni chama chenu ili mkiendeshe mnavyotaka sio kulazimisha wengine wafanye mnavyotaka. Zitto alikuwa Chadema, akafukuzwa akaanzisha chama chake ACT Wazalendo. Nanyi mmeshushuliwa. Anzsheni sasa chama chenu.

Zitto ndio kaanzisha ACT? Hebu tuanzie hapo.
 
Zitto yupo sahihi, tunafatiliana Sana wakati hapa duniani ni about ugali na mboga mambo ya Haki, Usawa na Amani ni about God's power... Ni upumbavu wa hali ya juu kumbebesha Zitto zigo la kuwaletea Haki , Usawa na Amani ...jumlisha myth story za maisha bora....wakati juzi Kati katika last stand ya final battle aliwaambia tuingie road lakin wote wakaingia mitini , ko yeye abaki bila ugali ...mnaumwa nn

Yeye aliingia road au alikuwa na remote mahali anabonyeza kuona kama channel zinafunguka? Alipaswa kuwa road kisha aite watu huko barabarani. Sisi tulitekeleza wajibu wetu wa kupiga kura, kuingia barabarani ni kujitoa muhanga, jambo ambalo hata yeye hajawahi kufanya. Ila hakuna shida, atakuja kuomba kura tena, labda hicho chama ndio kiwe mwisho wake sasa. Kwa huko Znz labda ndio watapata kura za wananchi maana Maalim Seif ndio mungu wao.
 
Nimeshangazwa na majibu ya mkuu wa chama cha ACT Wazalendo ndugu Zitto Kabwe aliyoyatoa kwenye mtandao wa twitter.

Zitto alikuwa akimjibu mwananchi mmoja aliyekuwa akionyesha frustrations zake juu ya uamuzi wa chama cha ACT kujiunga na Serikali ya CCM huko Zanzibar katika kile kinachoitwa serikali ya umoja wa kitaifa. Mwananchi huyo anaonyesha kuwa kuingia kwa ACT katika hiyo serikali hakuwezi kusaidia wananchi kupata uhuru mpana waliokuwa wakitamani kuwa nao.

Katika hali isiyo ya kawaida, isiyo ya uungwana na isiyo ya kiuongozi mkuu wa chama cha ACT ndugu Zitto badala ya kutumia fursa hiyo kumuelewesha au atleast akae kimya wananchi watumie haki yao ya kutoa maoni, yeye anamjibu kwa ufedhuli na jeuri kuwa "Kama unaona tumekosea basi anzisha chama chako".

Kwa kweli sikutegemea kiongozi haswa wa upinzani kutoa majibu ya nyodo kama haya kwa wananchi wanapouliza maswali ya msingi juu ya mienendo ya kisiasa nchini.

Labda Zitto afahamu tu kuwa sababu mojawapo ya leo ACT kuwa hapa ni haohao wananchi ambao leo anawajibu kwa nyodo kuwa "anzisheni chama chenu"

Lakini pia Zitto akumbuke kuwa kuna watu wamekifia hicho chama, Wakati akijibu kwa majibu ya "Anzisheni chama chenu" Je amelifikiria hili kuwa kuna watu wame-pay ultimate price kwa hicho chama au kwa course yake waliyoinadi kwao na kwa hiyo ndugu, jamaa, marafiki na wananchi wana haki ya kuhoji ukinyongakinyonga wa misimamo iliyowafanya hapo awali wawe tayari kukipigania hicho chama?

Lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida, Viongozi wa ACT sasa hivi wameacha kujibu maswali magumu ya wananchi juu ya hatua yao ya kuingia kwenye SUK wakati waliitangazia dunia na nchi kiujumla kuwa uchaguzi uliopita ulikuwa haramu, Zitto mwenyewe akaweka saini tamko la pamoja la Upinzani kuwa hawautambui uchaguzi ule pamoja na natunda yake, Sasa leo wananchi wakihoji wanaambiwa jamani eeh kama hamtaki tulichokifanya basi nendeni CCM, au NCCR yaani ni majibu ya kifedhuli uliopitiliza!. Sasa wameacha kutoa majibu kwa wananchi, wameanza kublackmail wanachama wa ACT na kutoa kauli za nyodo kwa wananchi, kuwa "ACT ina wenyewe na nyie kaanzisheni chama chenu"

Sasa leo tunaona kwa macho yetu, watu tuliodhani ni wakomavu wa kisiasa, tuliodhani kuwa mashambulizi yao kwa CCM basi wao labda wana ngozi ngumu na kwamba labda wao wakipewa nchi basi watakuwa humble, watakuwa na humility, watajibu hoja kwa hoja kumbe hawa jamaa ni arrogant(wenye viburi), intolerant(wasio wavumilivu) na wanajiona wao ni wamiliki wa taasisi kwa kuwa walizianzisha na si wahudumu tu wa taasisi ambazo wao ni wanachama.

Hawa wapinzani hawana blank cheque ya kutuletea jeuri sisi wananchi, Kwa miaka mingi tumekuwa tukiishabumbulia CCM, lakini na wenyewe hawana impunity, tutawaekeza ukweli maana hivyo vyama kwa namba moja au nyingine vinanufaika kwa jasho la wananchi iwe kwa ruzuku au wanasiasa wao kulipwa kwa kodi za wananchi n.k

Zitto acha jeuri kwa wananchi, Jibu hoja na frustrations zao kwa hekima, utulivu, nidhamu na utu. Bila wananchi usingekuwa hapa kuwa na humility.

View attachment 1648516

Na mahali pengine anamjibu mwananchi hivi:

View attachment 1648775
Kapoteza mwelekeo na Sasa tunajua kabisa huyu ni mchumia tumbo.Ajibu hoja na issue si kuanzisha chama.Kutakuwa na vyama vimgapi endapo kila mtu ataanzisha chama?Demokrasia I'ma mipaka yake.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Hawa hawa wananchi ambao wanalaumu huku Tanganyika ndio hata kwenye maandamano hawakuonekana.Kazi kukosoa watu kwenye keyboard tu,kujitokeza mbele hapana.Waacheni wanasiasa waamue yao maana hawakuungwa mkono na wanachama wao.Nao wameona labda walichofanya kwa kuitisha maandamano nyinyi wazee wa lawama mlikuwa hamkipend kwahyo wamefata umoja na serikal labda ndio mnapenda.Ndio maana hamkuandamana wala kujitokeza kwa wingi kupiga kura.Mtu analaumu kwa mitandao unaweza kukuta hata kura hajapiga.
Maandamano tarehe 2 lakini tarehe 1 siku moja kabla Polisi kwa amri za CCM wakawakamata viongozi wa CHADEMA, waliogopa nini? iweje hawakusubiria tarehe 2 waone? Kwenye sanduku la kura walijitokeza kwa wingi wakauchagua Upinzani lakini NEC, Tume, wakurugenzi na Polisi wakaulawiti, kuubaka, kuunajisi uchaguzi mkuu kwa njia haramu, watu hawataki biashara haramu za siasa kama sasa.
 
Muwe mnatofautisha JF na Instagram na TwItter

JF tunataka ushahidi sio kusema tu.

Dola milion 5 siyo dola bilion 500 acha kuongeza hesabu zako binafsi, Ushahidi uletewe hapo gheto unaposhinda ukivuta Bangi? Povu baki nalo huko huko mwenyewe uliyekuja na dola bilion 500
 
Back
Top Bottom