Zitto ataka wanaoikosoa ACT-Wazalendo waanzishe chama chao

Zitto ataka wanaoikosoa ACT-Wazalendo waanzishe chama chao

Tundu amewaambia muingie road mpinge uchaguzi hamjaenda,hawa viongozi mnataka wafuate matakwa yenu tu,wakiwaambia mfuate yao hamtaki
Kuingia barabarani kuna watu watauwawa na kuachiwa vilema, wao wasipoungana na hao wezi wa kura na wamwaga damu, ni watu wangapi watakufa na kupata vilema?
 
Zitto na Maalim Seif wamechukua Dola milion 5 cash wamegawana kimya kimya ndiyo maana Zitto kaanza kuwa na kiburi cha kishamba
Haya madai ni mazito lakini siwezi kushangaa kwa sababu huyo jamaa amesemwa sana huko nyuma kuwa ni mlaji mkubwa wa hongo.

Hata safari hii sidhani kama Jiwe na genge lake waliweka mpunga mezani ili hawa jamaa watulie au waingie serikalinj basi hawa jamaa walilaza damu, kuna kila dalili ya hongo kwa hawa jamaa kukubali kuingia serikalini huko Zanzibar
 
Jibu zuri sana. Lengo la siasa sio kuishi kwa uhasama muda wote. Binadamu kapewa siku chache sana chini ya jua.

Maendeleo kwanza siasa baadae. Zitto katazama pia namna yeye anavyofaidika kwa viongozi wa chama chake kuwa na nafasi serikalini.

Maisha ya nongwa muda wote ni upuuzi uliopitiliza, wanasiasa wa TZ lazima wajifunze.
 
Kama Wewe una haki ya kuuliza chochote basi tambua pia una wajibu wa kupokea majibu yoyote

Huwa simkubali kabisa huyu Mkongo ila ninatambua ana haki nae kujibu anachoona sahihi cha msingi asitukane tu!

Hakuna Chama chochote cha Upinzani hapa Nchini kinaweza kukataa offer ya kuunda Serikal ya Umoja wa kitaifa, kinachotokea ni kijicho tu

Kuna watu walipopewa fursa ya kuhudhuria sherehe za Uhuru zilizofanyika Mwanza Mwaka Jana waliipokea kwa Mikono miwili na Mbowe alihudhuria akamshukuru sana Rais, Zitto aliikosa fursa akakakejeli sana na kuwaita wenzie wame legeza msimamo na kujiona Mwamba … Safari hii kapata Zitto waliokosa wanamkejeli Zitto

Hao viongozi kadhaa wa CDM walioenda kwenye sherehe za uhuru huko Mwanza kutaka maridhiano, sisi wafuasi wao tuliwapinga waziwazi na tuliwapa ukweli wao. Kimsingi walijikuta wenyewe bila support yetu sisi washabiki wao. Haya tunayomwambia Zitto leo, hata viongozi wa CDM walioenda kutaka maridhiano uchwara tuliwananga, na post za kupinga ule upuuzi wa viongozi kadhaa wa CDM zipo humu humu jukwaani.
 
Acha ubwege wewe hiyo pesa dola milion 5 kwa Serikali ni pesa ndogo mno,kwako wewe usiyejielewa utaiona kubwa , wenzako akina Zito wanatamani waongezewe, najua thamani ya hizo bilion kuliko wewe na kwa taarifa yako bila Zito kupewa pesa kama hizo wasingekubali Serikali ya mseto kamwe

Unaijuia na kuilewa dolla Milioni 1 US kwanza au unataja tu namba ? Ungeanza na kuilewa US Dola laki moja kwanza , Zitto Kabwe alipwe 5 million USD halafu aendelee kuganga njaa kwenye Siasa zisizo na mbele wala nyuma ? Unajua CHADEMA walikuwa wanalipwa ruzuku kiasi gani na Serikali kwa mwezi? Anzia hapo halafu labda utapata idea ya 5 million USD ni nini, labda kwa kukusaidiatu kama chadema walilipwa shilingi milioni 300/mwezi hiyo hiyo haifiki hata dola laki moja na nusu achilia mbali dola laki tano na wala sijagusia dola laki 7, 8, 9 mpaka 1 million USD, ...
 
Nimeshangazwa na majibu ya mkuu wa chama cha ACT Wazalendo ndugu Zitto Kabwe aliyoyatoa kwenye mtandao wa twitter.

Zitto alikuwa akimjibu mwananchi mmoja aliyekuwa akionyesha frustrations zake juu ya uamuzi wa chama cha ACT kujiunga na Serikali ya CCM huko Zanzibar katika kile kinachoitwa serikali ya umoja wa kitaifa. Mwananchi huyo anaonyesha kuwa kuingia kwa ACT katika hiyo serikali hakuwezi kusaidia wananchi kupata uhuru mpana waliokuwa wakitamani kuwa nao.

Katika hali isiyo ya kawaida, isiyo ya uungwana na isiyo ya kiuongozi mkuu wa chama cha ACT ndugu Zitto badala ya kutumia fursa hiyo kumuelewesha au atleast akae kimya wananchi watumie haki yao ya kutoa maoni, yeye anamjibu kwa ufedhuli na jeuri kuwa "Kama unaona tumekosea basi anzisha chama chako".

Kwa kweli sikutegemea kiongozi haswa wa upinzani kutoa majibu ya nyodo kama haya kwa wananchi wanapouliza maswali ya msingi juu ya mienendo ya kisiasa nchini.

Labda Zitto afahamu tu kuwa sababu mojawapo ya leo ACT kuwa hapa ni haohao wananchi ambao leo anawajibu kwa nyodo kuwa "anzisheni chama chenu"

Lakini pia Zitto akumbuke kuwa kuna watu wamekifia hicho chama, Wakati akijibu kwa majibu ya "Anzisheni chama chenu" Je amelifikiria hili kuwa kuna watu wame-pay ultimate price kwa hicho chama au kwa course yake waliyoinadi kwao na kwa hiyo ndugu, jamaa, marafiki na wananchi wana haki ya kuhoji ukinyongakinyonga wa misimamo iliyowafanya hapo awali wawe tayari kukipigania hicho chama?

Lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida, Viongozi wa ACT sasa hivi wameacha kujibu maswali magumu ya wananchi juu ya hatua yao ya kuingia kwenye SUK wakati waliitangazia dunia na nchi kiujumla kuwa uchaguzi uliopita ulikuwa haramu, Zitto mwenyewe akaweka saini tamko la pamoja la Upinzani kuwa hawautambui uchaguzi ule pamoja na natunda yake, Sasa leo wananchi wakihoji wanaambiwa jamani eeh kama hamtaki tulichokifanya basi nendeni CCM, au NCCR yaani ni majibu ya kifedhuli uliopitiliza!. Sasa wameacha kutoa majibu kwa wananchi, wameanza kublackmail wanachama wa ACT na kutoa kauli za nyodo kwa wananchi, kuwa "ACT ina wenyewe na nyie kaanzisheni chama chenu"

Sasa leo tunaona kwa macho yetu, watu tuliodhani ni wakomavu wa kisiasa, tuliodhani kuwa mashambulizi yao kwa CCM basi wao labda wana ngozi ngumu na kwamba labda wao wakipewa nchi basi watakuwa humble, watakuwa na humility, watajibu hoja kwa hoja kumbe hawa jamaa ni arrogant(wenye viburi), intolerant(wasio wavumilivu) na wanajiona wao ni wamiliki wa taasisi kwa kuwa walizianzisha na si wahudumu tu wa taasisi ambazo wao ni wanachama.

Hawa wapinzani hawana blank cheque ya kutuletea jeuri sisi wananchi, Kwa miaka mingi tumekuwa tukiishabumbulia CCM, lakini na wenyewe hawana impunity, tutawaekeza ukweli maana hivyo vyama kwa namba moja au nyingine vinanufaika kwa jasho la wananchi iwe kwa ruzuku au wanasiasa wao kulipwa kwa kodi za wananchi n.k

Zitto acha jeuri kwa wananchi, Jibu hoja na frustrations zao kwa hekima, utulivu, nidhamu na utu. Bila wananchi usingekuwa hapa kuwa na humility.

View attachment 1648516

Na mahali pengine anamjibu mwananchi hivi:

View attachment 1648775
Njaa bwana. Imewapasa wale nguruwe ili waishi. Ndiyo sababu ya hasira hizo.
 
Zitto yuko sahihi, anzisha chama chako maana ACT ni mali ya Zitto ndo maana yeye kajipa cheo cha Kiongozi Mkuu wa Chama maana yake ni kwamba hutosikia eti kuna uchaguzi wa Kiongozi Mkuu wa ACT
 
Zito na maalum seif wamepokea dola milion 5 ili kukubali kuunda Serikali ya mseto ni biashara haramu ya Siasa , ukitaka ukweli wote msake Le mutuz au kuna rafiki wa polepole anaitwa sele 0715132277 anazo siri zote juu ya biashara haramu za Siasa ya Tanzania

Vipi CCM hawajakutunuku bado ile nishani ya uzushi uliotukuka?
 
Kila mtu akiwa anachokitaka ndio hicho hicho chama kifanye basi itakuwa balaa, mimi naona jibu la Zitto ni la kiuhalisia kabisa. Ndio maana Chadema walikaa wenyewe huko wenye chama chao 2015 na kuamua kubadili gear, laiti wangetaka maoni ya watu wasingeweza kufanya hilo jambo.

Kwahiyo mi naona jibu la Zitto ndio uhalisia wenyewe.
 
Sjawahi kufahamu Kwa nini ukweli huwa unauma Sana!!!

Zitto kasema ukweli tupu, kama hulidhiki na maamuzi yao, Anzisha Chama chako
 
Wanaoumia na SUK ni CDM, cha kushangaza CDM waliamua kununa huku hawana leverage yoyote dhidi ya serikali, walikuwa wanategemea leverage ya ACT Zanzibar. CDM waendelee kununa tu hadi 2030 hakuna kitakachopungua wala kuongezeka.
Sawa umepataia ila ipo siku tutapata tume huru
 
Mkuu,
This is democracy, maamuzi ya MTU au ya chama cha sisa should be respected. Looks like chadema kimewauma sana hiki kitendo.
They will never get peace kwa kusaliti big course

Yaani hawa jamaa wameiondolea serikali ya CCM pressure kubwa ya ndani ya nchi na hata ya nje ambayo ingewaminya wafanye reforms fulanifulani za msingi.

Yaani ACT wamewazawadia CCM zawadi ya uaminifu kwa mchakato haramu na feki wa uchaguzi na kwa kufanya hivyo wameihakikishia CCM kuwa hakuna consequences zozote watakazozipata hata wakirudia michezo yao hiyo kwenye chaguzi zijazo!. Kwa kweli hakuna usaliti mbaya kama huu kwa future ya demokrasia ya nchi hii!.

Yaani kacheo kisicho na kichwa wala miguu cha Maalim na pengine "behind the scene deals ikiwemo hongo" vimesababisha hawa watu wasaliti movement nzima ya kuiminya CCM ifanye reforms za maana kwenye tume ya uchaguzi

Inasikitisha sana.
 
Mkuu,
This is democracy, maamuzi ya MTU au ya chama cha sisa should be respected. Looks like chadema kimewauma sana hiki kitendo.

Mkuu wapi unapounukuu msimamo wa CHADEMA?

CHADEMA ni taasisi kubwa jombi.
 
Siyo Zitto alitaka maandamano aliyetaka maandamano hajanunuliwa na CCM, pia ukumbuke maandamano yalipangwa tarehe 2 lakini tarehe 1 siku moja kabla Polisiccm kwa Amri ya CCM wakawakamata viongozi wa chadema, maandamano yalikuwepo lakini Polisiccm wakayazuia kwa uoga wao tu.
Tatizo makamanda mna kumbukumbu hafifu sana, mara hii mmeshasahau hata aliewataka muingie barabarani! Kwa mwendo huu kweli mnaelewa mlikuwa mnaombwa kuingia barabarani kwa sababu gani?
Screenshot_20201213-143908.png
Screenshot_20201213-143749.png
 
Unaijuia na kuilewa dolla Milioni 1 US kwanza au unataja tu namba ? Ungeanza na kuilewa US Dola laki moja kwanza , Zito kabwe alipwe 5 million USD halafu aendelee kuganga njaa kwenye Siasa zisizo na mbele wala nyuma ? Unajua chadema walikuwa wanalipwa ruzuku kiasi gani na Serikali kwa mwezi ? Anzia hapo halafu labda utapata idea ya 5 million USD ni nini, labda kwa kukusaidiatu kama chadema walilipwa shilingi milioni 300/mwezi hiyo hiyo haifiki hata dola laki moja na nusu achilia mbali dola laki tano na wala sijagusia dola laki 7, 8, 9 mpaka 1 million USD, ...
We jamaa mbona fala sana hzo US 5 milions dollar haizdi hata tsh billion 12 hafu unatupigia kelele zionekane nying kwamba serikali haiwez kuzitoa kuzitoa..
 
We jamaa mbona fala sana hzo US 5 milions dollar haizdi hata tsh billion 12 hafu unatupigia kelele zionekane nying kwamba serikali haiwez kuzitoa kuzitoa..

Hata wewe haulewi maana ya dola milion 5 USD unataja tu namba, laiti ungeelewa usingeamini kirahisi hivyo kwamba Serikali inaweza kumpa Zito Kabwe hela zote hizo, for what ?
 
Sasa Ndugu yangu Wewe wa kumfundisha Siasa Maalim Seif Sharif Hamad hasa hasa siasa za Upinzani Tanzania?

Seif katumia options zote mnazomshauri na bado hazijazaa matunda

1. 1980s Seif katumia uongo na uzushi na fitna kutaka kumchomoa Sheilkh Jumbe kwa kumchonganisha na Nyerere , akafanikiwa kumkosesha Urais Jumbe lakin hakufanikiwa kupata Urais wa Znz

2.1985-1990 Seif Katumia Siasa za kumchonganisha Idrisa Abdul wakeel na Wananchi Unguja 1985-1990 akafanikisha kumstaafisha Urais Hayati Mzee Wakeel lakin hakuupata Urais
3. 1995 Seif akafanikiwa kuichonganisha Znz na Jumuiya ya Kimataifa hadi ikawekewa vikwazo lakin haikumfanya kupata Urais
4.2000 Seif akafanikiwa kuitisha Maandamano ya vurugu watu wakauawa lakin hakufanikisha azma yake ya Urais

5. 2010 akaridhia maridhiano ili apate fursa ya kuwa ndani ya Serikal akidhan ni shortcut ya kumfanya kupata Urais lakin hakufanikiwa
6.2016 Akasusia Uchaguzi, uchaguzi ukafanyika lakin hakuna alicho gain

So Options zote za Kisiasa kuanzia Fitna za kuchonganisha Watu ndan ya Serikal, kufungwa, kuhama vyama, kuitisha maandamano hadi watu kufa, kususa, kuchongea jumuia ya kimataifa hadi kuwekwa vikwazo, kote huko kamaliza

So only option iliyopo ni kushirikiana na Walinzi wa Mapinduzi matukufu ya 1964
Hao viongozi kadhaa wa cdm walioenda kwenye sherehe za uhuru huko Mwanza kutaka maridhiano, sisi wafuasi wao tuliwapinga waziwazi na tuliwapa ukweli wao. Kimsingi walijikuta wenyewe bila support yetu sisi washabiki wao. Haya tunayomwambia Zito leo, hata viongozi wa cdm walioenda kutaka maridhiano uchwara tuliwananga, na post za kupinga ule upuuzi wa viongozi kadhaa wa cdm zipo humu humu jukwaani.
 
Back
Top Bottom