Zawadi Ngoda
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 4,175
- 2,294
Imenichukua takriban wiki moja kusoma malalamiko ya wote dhidi ya maamuzi ya ACT kujiunga SUK.They will never get peace kwa kusaliti big course
Yaani hawa jamaa wameiondolea serikali ya CCM pressure kubwa ya ndani ya nchi na hata ya nje ambayo ingewaminya wafanye reforms fulanifulani za msingi.
Yaani ACT wamewazawadia CCM zawadi ya uaminifu kwa mchakato haramu na feki wa uchaguzi na kwa kufanya hivyo wameihakikishia CCM kuwa hakuna consequences zozote watakazozipata hata wakirudia michezo yao hiyo kwenye chaguzi zijazo!. Kwa kweli hakuna usaliti mbaya kama huu kwa future ya demokrasia ya nchi hii!.
Yaani kacheo kisicho na kichwa wala miguu cha Maalim na pengine "behind the scene deals ikiwemo hongo" vimesababisha hawa watu wasaliti movement nzima ya kuiminya CCM ifanye reforms za maana kwenye tume ya uchaguzi
Inasikitisha sana.
Nilichokuwa nasubiri ni kuona hao watu wanakuja na solution/mapendekezo juu ya nini ACT wazalendo wangekifanya baada ya hapo kama wasingejiunga na SUK! Well kuna baadhi ya wanachadema wamekimbia nchi- Sijui kama hilo ndio jibu! Lakini ni hatua mojawapo, muda utatuonyesha. Kuna covid-19 ikaamua kuapishwa na spika- nayo ni hatua mojawapo ambayo kikundi fulani kimeona ni dawa ya kubadili mtazamo wa CCM. Mimi naamini kuwa yote haya yanafanyika kwa nia njema sana ya kubadili mbinu za CCM mbele ya wapinzani.
Ni ukweli usiofichika kuwa mbinu ya kuwaingiza wananchi barabarani ilishindikana, kwa vile watawala walitumia nguvu za ziada za kukabiliana na wananchi. Swali linabaki pale pale, tunafanya nini katika hatua ijayo. Sijasikia lolote toka kwa CHADEMA zaidi ya kudeal na covid-19 na waliokimbia nchi.
Binafsi sikilaumu chama chochote kile kwani yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi ni mshtuko mkubwa kwa kila chama. Hakuna aliyejua watawala wangeenda mbali namna hii bila aibu mbele ya macho ya waangalizi wa nje na ndani. Hakukuwa na haiba kabisa, ni ubabe wa aina yake.
Katika wakati kama huu, ili kuwaunganisha wanachama wa kila chama kunahitajika kurudi nyuma kwanza hatua kadhaa ili kujipanga upya. Ni strategy muhimu sana hii katika uwanja wa vita, vinginevyo mtamalizwa wote na msiwe na askari hata wa kupiga kelele. Hivyo kwangu alichokifanya ACT ni kurudi nyuma na kujipanga upya. Tunasubiri move ya CHADEMA, kwani sijaisikia!
Hata hivyo nyie mnaolaumu bado mna nafasi ya kueleza ACT wangefanya nini? Tiririkeni!