Zitto aja na hoja nzito
na Mwandishi Wetu, Dodoma
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), ameitaka serikali kuondoa mara moja balozi wake nchini Zimbabwe, na Bunge lisitishe shughuli zake na kuijadili hali ya mambo nchini humo.
Hayo yamo katika hoja ya jambo la dharura, ambayo mbunge huyo aliiwasilisha jana kwa Spika Samuel Sitta, chini ya kanuni ya 47 na 48.
Mara baada ya kipindi cha maswali na majibu, wakati Sitta alipomuomba Katibu wa Bunge kueleza jambo linalofuata katika ratiba ya shughuli za Bunge, Zitto alisimama na kuomba nafasi ya kuzungumza.
Alipopewa nafasi hiyo, alieleza kuwa kama alivyofanya asubuhi kwa kumpatia Spika jambo hilo la dharura, aliliomba Bunge kusitisha shughuli zake, ili lijadili hali ya mambo nchini Zimbabwe.
Spika alifahamisha Bunge kuwa alikuwa amepokea hoja hiyo kutoka kwa mbunge huyo asubuhi na baada ya kuisoma alikubaliana kuwa hoja hiyo ni nzito.
Mheshimiwa Zitto amewasilisha kwangu hoja ya dharura akitaka Bunge lisitishe shughuli nyingine ili lijadili kuhusu Zimbabwe. Baada ya kuipitia nimeona kweli ni hoja nzito, alisema Sitta.
Hata hivyo, Sitta alisema haiwezekani kuijadili hoja hiyo moja kwa moja bungeni, hivyo ameikabidhi kwa Kamati ya Mambo ya Nje, ili iipitie na kuwasilisha maoni yake katika ofisi yake, kabla hajatoa uamuzi kuhusu hoja hiyo.
Sitta alisema ameona busara kuikabidhi hoja hiyo kwa kamati ili kujiepusha na kuharibu zaidi kuliko kutengeneza kwa kuamua kuijadili hoja hiyo moja kwa moja.
Ingawa Zitto hakupewa nafasi ya kuelezea hoja yake, lakini gazeti hili lilifanikiwa kupata nakala ya hoja hiyo, ambayo mbunge huyo anaeleza kuwa mambo yanayotokea Zimbabwe hivi sasa yanahatarisha amani na kulifedhehesha bara la Afrika.
Anasema mara baada ya viongozi wa SADC kukutana na kujadili hali tete ya Zimbabwe, na mara baada ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kusema kwamba uchaguzi wa Zimbabwe hautakuwa huru na wa haki, nchi hiyo imechukua hatua ya kumwondoa balozi wake nchini.
Katika shughuli za kidiplomasia, hali ya nchi kumwondoa balozi wake kufuatia matamko ya nchi mwenyeji, ni sawa na kutangaza mgogoro wa kidiplomasia, anasema Zitto katika hoja hiyo ya kurasa mbili.
Anasema mpaka sasa, Serikali ya Tanzania bado haijachukua hatua yoyote kuhusu balozi wake aliyepo Harare na kubainisha kuwa Mtanzania huyo, ambaye ametumwa kumwakilisha rais na nchi nchini humo, anaweza kuwa katika hali ya hatari.
Anasema kuwa Zimbabwe ni rafiki wa siku nyingi wa Tanzania na Tanzania imesaidia sana katika harakati za ukombozi wa nchi hiyo, lakini hali ya sasa nchini humo haivumiliki, na ni aibu kwa bara la Afrika.
Anabainisha kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Wilson Masilingi na Anna Abdallah, wameshalizungumzia suala hilo bungeni na kuunga mkono kauli ya serikali iliyotolewa na Membe. Anaongeza kuwa, Chama cha Upinzani cha MDC cha Zimbabwe chini ya kiongozi wake, Morgan Tsvangirai, wamejitoa katika uchaguzi huo na hivyo kusababisha hali kuzidi kuwa tete. Zitto anashangaa katika hoja yake hiyo kuwa, kama Robert Mugabe na chama chake cha ZANU-PF hawawezi kuachia madaraka hata kama wakishindwa uchaguzi, na kwamba wapo tayari kuingia vitani, ni kwa nini waliitisha uchaguzi? Viongozi kama akina Mugabe ambao walikuwa na heshima kubwa na mfano wa kuigwa kwa viongozi bora wa Afrika, wanapofanya vitendo kama anavyofanya sasa, wanatutia aibu na kulichafua bara la Afrika, anasema Zitto katika hoja yake.
juu

Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 30 yameshatolewa. (
Nawe toa maoni yako!)
Hawa mawaziri na maraisi wa Africa watakao kuiunganisha Africa kuwa nchi moja lazima wakae chini kujua Jambo hili kwanza.Zimbabwe ni mfano wa hasara za kuungana . Matatizo ya ndani bado kutatuliwa watu wanadakia umoja wa Africa!!!Tanzania imechelewa sana kuichukulia hatua Zimbabwe Zimbabwe makabila ya mashona na ndebele hayaivi kabisaa na ndiyo kwanza yananyimana haki za binadamu . Halafu huu pia ni ubovu wa serikali za majimbo kuna majmbo ambayo yanaona kinyaa kumuona mtu wa majimbo mengine akitawala.
na dtto likingezuma - 24.06.08 @ 09:50 | #18342
Zito ,maswala ya kuingilia Wazimbabwe yanakutoka wapi?Nilifikiria wewe unaweza kutafakari kuwa, nini chi za magharibi zinahitaji ,ndani ya Zimbabwe,Unatakiwa kujua hali ya nchi hiyo kwanza.Mgabe hana tatizo lolote,Tatizo la Mgabe ni kukaa madarakani kwa mda mrefu.Hili ndilo la kuzungumza.Mgabe hayupo pale madarakanikwa matakwa yake.Wapo wapiganaji wanaomuunga mkono arudishe mali zote na aridhi yote iliyochukuliwa na wazungu,Wazungu wamepandikiza watu wa kurudisha aridhi iliyochukuliwa na Mgabe kuwapa wazawa mali na aridhi.Hili ndilo tatizo kubwa la wazungu kuanzisha vurugu ndani ya Zimbabwe.Sasa mheshimiwa Zito ,Hapa tatizo ninini la kumrudisha balozi.Au kwa vile ulikuwa Marekani wamekupa maneno ya kukulainisha uweze kumwona aliyekomboa Zimbabwe ni mbaya.Elewa wakati anafariki Joshua Nkomo alimwambia Mgabe,Ninakuachia nchi hii uwarudishie aridhi wananchi .Ileahadi ndiyo inayoleta matatizo.Wazungu hawakupenda .Imewashushia hadhi.Zito zungumza ya mafisadi Epa na mikataba mibovu .Swala la Mgabe achieni watu wa maghalibi wanaotaka kuabudiwa.Africa unite
na mtzmweyeuchungu, tz, - 24.06.08 @ 10:52 | #18376
No NO NO Zitto,usiingilie masuala ya ndani ya Zimbabwe.Tuna mambo mengi ya kujadiuli nchini kwetu.Kwani sisi uchaguzi wetu ndiyo uko fair.Pigana kupata tume huru ya Uchaguzi Tanzania achana na wazimbabwe.NO NO to Zitto's Comments.Asante sana Mtz mwenye uchungu.
na David Villa, Tanzania, - 24.06.08 @ 08:06 | #18378
Achaaaaaa!kabisa Zito mambo ya Zimbabwe kwani Mugabe nimtu makini anajua anchokifanya na siyo mtoto.Morgan T wa MDC yuko nyuma ya Wamarekani&Waingereza so sio busara kumwacha atawale pale Zimbabwe litakuwa kosa kubwa.Na haya matatizo yote yameletwa na hao wazungu kwani Wameshaharibu bara letu kwa kuwaweka watu kama wakina Morgan T(MDC)
na fredrick laizer, Tumaini University-Iringa, - 24.06.08 @ 08:20 | #18384
hii ni distraction ambayo hatuihitaji wakati huu. Tumeikaba koo ccm na rais wake watatue matatizo chungu zima yanayotunyima usingizi sasa ukianza kuzungumzia ya zimbabwe utaipa serikali mwanya wa kebuni 'maelezo' mengine. mjuavyo, africa union na UN ni toothless bulldogs. Wanaitisha vikao kulaani kwa maneno ukiukwaji wa haki za binadamu full stop. uwezo wanao wa kuwaondoa viongozi wasiofaa lakini hata kwenye level hii kuna kukingiana kifua. Hizi ni club za mafisadi wa siasa. wakikutana kuna vicheko, back slapping na kunywa champagne. Kwao, maisha ya wananchi na mateso yao si kitu. Baada ya wao ni wao (after me is me-change in leadership is taboo).
na Gabriel - 24.06.08 @ 08:52 | #18396
Mimi kwa kweli sasa naona umuhimu wa kuwa na wabunge wengi vijana katika Bunge letu tukufu. Yaani nilikuwa nangoja mtu wa kuwa sensitive kama wewe. Hali ya Zimbabwe inalitia aibu bara letu. Hawa wazungu wana haki ya kutudharau kwa kweli. Matamshi ya Mugabe yalinisikitisha kwa sababu niliona alipoikandamiza democrasia kwa kiwango cha juu saana. Na kuna haja ya kumrudisha balozi wetu nyumbani ili Mgabe ajue kuwa hatukubaliani na matamushi yake hata kidogo. Kwa nini sasa akaitisha uchaguzi???
na Leonard, Tanzania, - 24.06.08 @ 09:04 | #18399
Tunataka wabunge kama Zitto ambao sio wanafiki. Wachangiaji hapo juu mtzmwenyeuchungu, david na frederick ni wanafiki wenye jazba na pia uelewa wenu ni mdogo. Umoja wa mataifa umetoa tamko leo kumlaani Mugabe na inaonekana sio mwisho maana wanaoumia ni wananchi na UN haiwezi kukaa kimya.Un ni dunia nzima, waafrika na wazungu na walimwengu wote. Swali NI kwa nini Mugabe ameitisha uchaguzi kama hayuko tayari kukubali matokeo? Hakuna mwenye akili ambae atakubaliana na hoja za Mugabe kwamba Tsavingirai ni kibaraka wa wazungu. Ndugu zangu ni vizuri hoja inapotolewa tuijadili na sio kuangalia nani kaitoa. Suala la ardhi lilishakwisha siku nyingi ndio maana Mugabe alishinda uchaguzi uliopita na sasa hana sera nyingine zaidi ya kuwa 'Mungu amenipa nchi hii'.Zimbabwe ni sehemu ya Dunia hivyo kinachotokea pale kwa namna moja au nyingine kitatuathiri ndio maana naunga mkono hoja ya Mh.Zito kuwa Bunge lijadili hali ya mambo na kutoa msimamo. Jambo hilo ni muhimu ili kuwa na kauli moja kama nchi, na bungeni ndio mahali pake maana lile ni wananchi ndio wameongea, mambo ya kusubiri mpaka kwanza waziri au rais azungumze ni kurudisha enzi za zidumu fikra za mwenyekiti. Kuna aibu kidogo tulipata wakati wa vurugu zilizotokea nchini Kenya mwezi Januari. Kuna wakimbizi walikuja Tanzania na walipofika walizuiwa na maafisa uhamiaji eti hawana habari kama Kenya kuna machafuko, na jambo hili sio waziri wala rais aliyewaomba msamaha wakenya wale. Tukubali au tukatae ile ni aibu. Tatizo letu ni kuwa watumishi hawako huru kufanya hata
maamuzi madogo. Tutatakiwa kuachana na dhana mbaya zilizojengeka muda mrefu katika bara hili za rais wa maisha na mshindi wa uchaguzi kudharau wapinzani wake. Mambo haya yatatokomezwa tuu mabunge ya nchi zetu za kiafrika yatakaposhikia bango na kutoa matamko kulaani matukio kama haya ya Zimbabwe.
na Mfuatiliaji, tz, dsm., - 24.06.08 @ 09:13 | #18401
Wee Zitto, acha kurukia mambo mbona kura za CUF zinapoibiwa haujawataka mabalozi wa nchi za nje waondoke nchini.
Acha Mugabe apambane na vibaraka wa Uingereza na Marekani. Kama kweli Waingireza wanataka haki na demokrasia, iweje asilimia 92% ya ardhi yenye rutuba ikaliwe naz walowezi 200????????????????????
Zitoo waabie Walowezi kwanza waachie ardhi ndipo uoji uchaguzi huru.
Uchumi wa Zimbabwe umeharibiwa na Nchi za Magharibi zinazotaka walowezi wasibanwe kuachia ardhi
Wazimbabwe wanapigia kura MDC siyo kwakukipenda bali wanadhani hali mbaya ya uchumi itatengamaa kwa vile Vibaraka ndo kipenzi cha wakoloni wa zamani wa Zimbabwe!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
na bill - 24.06.08 @ 09:40 | #18408
NAFIKIRI NA NINAHUHAKIKA KWAMBA ZITTO YUKO SAWA, WATU MNAO SEMA MAMBO YA ZIMBAWE HAYATUHUSU NI WATU WENYE MAWAZO FINYU.KWA KUWA LINAOTOKEA SASA ZIMBABWE VIONGOZI WENGINE WA AFRIKA WENYE UCHU WA MADARAKA WANAANGALIA TU WAONE JUMMUIYA YA KIAFRIKA NA MATAIFA MENGINE WATAFANYA NINI? WAKIONA HAKUNA CHOCHOTE KINAFANYIKA KESHO WATAFANYA KATIKA NCHI ZAO INAWEZEKANA KABISA YAKATOKEA TANZANIA.SASA TUWE WAKWELI KUAMBIZANA MAMBO YA MSINGI. MIMI NIPO HAPA AFRIKA YA KUSINI, NINA MARAFIKI WAZIMBABWE WAKATI WALIKIZO NIMEPATA BAHATI YA KUTEMELEA HUKO, ASIKUMBIA MTU HALI NI MBAYA SANA, MAISHA NI MAGUMU.SASA YOYOTE WMENYE UWEZO WA KUTOA MSAADA KUREKEBISHA HALI YA MAMBO AFANYANYE HIVI.ZITTO HUKO SAHIHI KABISA
na Saluvatory, South Africa, - 24.06.08 @ 09:54 | #18415
Haitaji elimu kubwa kufahamu kuwa Zitto ni mbunge mwenye ufahamu mkubwa, wakipatikana 10 kama yeye tutapata mabadiliko makubwa tz afrika pia.Wakati Mwl Nyerere anahangaika na uhuru wa nchi za kusini wma afrika, je TZ haikuwa na mambo ya kufanya?
Wote mnaopingana na Zitto upeo wenu ni mdogo na inawezekana ndio mnaochangia kurudisha taifa nyuma kwa kuchangua viongozi wakiwemo wabunge ambao si makini.
Wakati umefika Mugabe aachie ngazi.
na Noni Yaza, Shinyanga Tanzania, - 24.06.08 @ 10:01 | #18417
wewe mdau wa mtzmweyeuchungu, tz, - 24.06.08 @ 10:52 | #18376
jaribu kuona hali iliyopo nchini zimbabwe,wananchi wanakufa(karibu watu 70)wanateswa na milioni 4 wamekimbia nchi!
mugabe ameapa kutokabidhi nchi akishindwa na ataingia msituni!
duru ya kwanza ya uchaguzi mugabe ameshindwa vibaya!
msioelewa mnazilaumu nchi za magharibi wakati matatizo yote haya yanasababishwa na udikteta,uchu wa madaraka na uongozi mbovu wa mugabe!
kisingizio ni kuwa anataka kurejesha ardhi kwa wazawa kwa miaka 27 ametawala watu na agenda ni kurejesha ardhi kwa wazawa!
tanzaimewekamsimamo wake kuwa uchaguzi wa zimbabwe hautakuwa huru na wa haki zimbabwe imemwita nyumbani balozi wake nchini nini maana yake kama si kuvunja uhusinao wa kidiplomasia?kisa tazani kusema ukweli!
na huu ni mfano wa jinsi mugabe alivyo dikteta mmbaya!
wakati umefika mugabe aondoke kwa hiari yake au ang'olewe kama kanali bakari!
ongera mhe.zitto kwa upeo mkubwa na kuona mbali ni mfano wa wabunge nchi inaowahitaji
na jingo - 24.06.08 @ 10:08 | #18422
Mheshimiwa Zitto Tanzania haina tume huru ya uchaguzi ni vyema sana kama tutamsaidia kwa hali na mali mch Mtikila kwenye kesi anayotaka kuifungua hili na sisi tuwe na tume huru ya uchaguzi[wakaazi wa Arusha mjini wanakumbuka hata mbunge wa sasa hatukumchagua].Tanzania tangu enzi za mwl Nyerere imekuwa na desturi ya kusahau kushughulikia mambo yake ya ndani na kukumbilia mambo ya nchi nyingine.Tulipigana kuzikomboa nchi za Msumbiji,Zimbabwe,Zambia na South Afrika,leo hii watanzania waliokuwa wanaishi South Afrika wametimuliwa hawatakiwi kabisa kuonekana huko wamesahau kuwa tulimwaga damu kwaajili ya uhuru wao.Mheshimiwa Zitto Tanzania ina mambo mengi ya kujadili kama EPA,Richmond na nk,jamaa wa CCM wamefurahi kweli kwamba mambo muhimu yanayowasibu watanzania yatasitishwa kujadiliwa kwa muda na kurukia mambo ya Zimbabwe.Mambo ya Zimbabwe tuwaachie South Afrika kwasababu ndiyo itakayo athirika kwa kupokea wakimbizi.
na G KABONDE, ARUSHA,TANZANIA, - 24.06.08 @ 10:16 | #18430
mhe.zitto yupo sahihi kabisa kuliona tatizo la zimbabwe na kuomba bunge lijadili,watu wanomkosoa kwa hili upeo wao wa kufikiri ni mdogo sana kwani hawajui kuwa matatizo ya zimbabwe ni matatizo ya afrika,nyerere,kwame nkurumah waliliona hili,ongera zitto kwa muono wako wa mbali!
zimbabwe ikilipuka vita tanzania hawezi kuwa salama,itapata matatioz tele ikiwamo kupokea wakimbizi nk,pia tanzania-raisi wetu ni mwenyekiti wa AU hivyo mhe.kabwe ni kama amemkumbusha mhe.mwenyekiti atoe tamko na kuweka msimamo wa nchi wazi na mapema!
na watz - 24.06.08 @ 10:17 | #18431