Elections 2010 ZITTO: CHADEMA isipoangalia itakosa mbunge kigoma 2015

Elections 2010 ZITTO: CHADEMA isipoangalia itakosa mbunge kigoma 2015

Zitto anaweza kuja na kukanusha hayo unayoyaandika na source huna!
 
Zitto anasema kweli na kweli tupu! Kwa nini wale wanne wa NCCR waliondoka Chadema? Jibu: wameona ni chama kinachoendeshwa Kidikteta na Kidini, kama ni muIslam huna thamani Chadema, kama yanayomkuta Zitto sasa hivi na karibuni tutasukia Arfi nae hayo hayo.

hakuna ukweli, kama mtu wenzako wamekuona huna thamani si unajiondokea zako tu? unangoja nini?,
 
Kwani Chadema ikikosa mbunge Kigoma (Tanganyika) kuna shida gani?

Tushawajua wabunge wa wakigoma vigeugeu
 
..Chadema walili-mishandle suala la Kafulila na wenzake.

..waache kuhangaika na majimbo yaliyochukuliwa na NCCR.

..wanachopaswa kufanya sasa hivi ni kujaribu kupokonya yale majimbo yaliyochukuliwa na CCM.
 
Zitto hana mpango wowote. Achukue chake mapema achape mwendo. Si mpinzani hata kidogo. dogo ana njaa tu na pesa ndo maana anakuwa msaliti




Chadema itakuwepo tu bila Zitto , Kwanza anaendelea kuushusha upinzani hadhi.


Go Zitto, it was not nice to be with you
 
Kwana haya kayaona baada ya kufika kigoma kwenye huo mkutano? Kwenye kamati yao ya viongozi wa cdm alishindwa ku-present hayo?
 
huyu bwana zito naamini kabisa kuwa kalewa sifa, na kujiona yeye ndio yeye bila yeye mambo hayaendi, kama ni kweli kauli yake hiyo ina maana kwamba nae anataka kuhama CDM, awe muwazi au anatumiwa na awa mabwana wakubwa wanaodhani nchi hii ni ya kwao peke yao? wanaokula nyama bila hata kubakiza mifupa na wakibakiza wanaitupa mbali ili wale wasio na uwezo wanuse hata harufu ya nyama?

Zito ni wa ukweli, chamsingi tumulikeni kwa mwenyekiti wa chama kwanini always anakuwa against na wale wanaokuwa na uwezo wa juu ndani ya chama kama chacha wangwe na hata zito pia?
 
Aende tu huko NCCR kama katibu anasema hayo unafikiri hamaanishi?
 
Zitto bana anazidi kuwakasirisha cdm, sijui ana mpango gani kichwani mwake
ana mpango wa kuhama chama ndo maana anadhan cdm itakosa kiti hata kimoja, ngoma ikilia sana ujue inakaribia kupasuka_umaarufu wa mtu unatokana na watu_watu wakikuelewa na kukudharau ujue mwisho wako unakuwa umefika_ndugu yangu wa kigoma mwenzangu mwisho wake umefika
 
kama kweli zitto kayasema hayo maneno basi anahitaji kupepewa, ana mapepe(po)
 
Jana naibu katibu mkuu wa CDM Zitto kabwe amefanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya kawawa mjini kigoma na kueleza haja ya kufanya tathnimini ndani ya chama juu ya uchaguzi uliopiita

Alisema katiak majimbo nane ya mkoa wa Kigoma CDM imepata kiti kimoja, NCCR mageuzi vinne na vilivyobaki vimekwenda kwa CCM

amesema jambo la kujiuliza kuwa kati ya wbaunge wanne wa NCCR mageuzi, watatu wametoka CDM na hadi mwaka jana walikuwa huko

amesema CDM ifanye tathimini kwani itacfika wakati hasa 2015 inaweza ikakos ambunge katika mkoa wa Kigoma

kwa hayo maneno yake inaonesha yuko mboni kuhama chama...na inawezekana akamfata rafiki yake Kafulila...
 
Kwanza kabisa siamini kama Zitto alisema hivyo. Hata hivyo Zitto siku hizi haaminiki sana maana ana tabia ya kutoa matamshi yanayotiliwa mashaka. Kama kweli ametamka hivyo, yeye ndiye anayetakiwa kutoa majibu sababu ya hilo kutokea.

Kama Zitto hakutoa matamshi hayo basi ni mbinu zile zile za kutaka kukivuruga Chadema na mwanya wameuona kuwa unapatikana kwa kupitia Zitto. Wakati mwingine tunaweza kuamini kuwayeye amekubali kutumika kuhujumu Chadema.

Kuhusu kauli ya Zitto kuwa wabunge 4 wa NCCR kutoka mkoa wa Kigoma ambao wametokea Chadema na hivyo mwaka 2015 kunaweza kukawa na uwezekano wa kutokuwa na mbunge wa Chadema ninaona yafuatayo:
1. Inaaminika kuwa Zitto mwenyewe ndiye aliyewasaidia watu kama kina Mh. Kafulila katika kupata ubunge kupitia NCCR. Ni yeye Zitto aliyeahidi kuwa atamsaidia Kafulila katika kampeni. Hili liliwafanya watu kujiuliza itakuwaje pale Chadema itakapomsimamisha mgombea ubunge katika Jimbo hilo hilo ambalo Kafulila anagombea kupitia NCCR? Ni wazi naibu katibu mkuu wa Chama anapotoa matamshi ya kumsaidia mbunge wa chama kingine hata kama ni cha upinzani bila sababu zinazoeleweka tafsiri yake ni kukihujumu chama. Ikumbukwe kuwa Kafulila kabla ya kuondoka Chadema aliwahi kumpigia debe Zitto wakati anawania Uenyekiti wa Chadema. Hivyo Zitto alikuwa sababu ya hao wabunge wa NCCR kuondoka toka Chadema.

2. Kuna mwenekano wa haraka ambao unaweza kutafsiriwa kuwa Zitto ana lengo la kuendelea kuleta chokochoko ndani ya Chadema ili awe na sababu ama ya kuondolewa( kitu ambacho ni kigumu) au kujiondoa mwenyewe. Baada ya kuondoka Chadema atakuwa amejiandilia mahali pa kutua. Hapo anaandaa mazingira.

3. Zitto anaonekana kujaribu kila mbinu ambayo inawezeka kufanya kazi katika kufikia malengo yake binafsi aliyonayo. Kila mara anataka watu wasahau kitu kimoja pale anapoleta kitu kipya. Bado mashaka yetu yataendelea kuwepo kuhusu mambo ambayo Zitto anayafanya na malengo yake katika Chadema.

Zitto usijihangaishe sana, kama una mapenzi ya kweli kwa Chadema tutayajua tu lakini mpaka sasa huaminiki. Hili wala lisihusianishwe na dini ya Zitto maana suala la udini limeonekana kama mtaji wa kuvuruga Watanzania na hasa pale Chadema ilipohusishwa na Ukristu. Kutokuaminika kwako kunaonekana katika baadhi ya matendo na maneno yako. Mifano michache ikiwa: moja, kukubali kuwa kwenye kamati ya rais ya madini. Tulihoji kama unaweza kuleta matunda yoyote kwani kamati hizi zilieleweka kama mbinu ya kuwapumbaza Watanzania. Hadi leo matunda ya kamati hiyo hatujayaona. Pili, ukasema Dowans inunuliwe. Wewe kama mpinzani na unaelewa kuwa Dowans ni dada yake Richmond. Iweje tuikatae Richmond lakini tuipokee Dowans? Hoja hiyo ilipingwa na baadhi ya wabunge wa CCM, huoni ulikuwa kioja? Hiyo Dowans hatuwafahamu wamiliki wake ingawaje wengine wanasema ni dili ya mafisadi watatu.Tatu, juzi juzi mlipiga kura kuhusu uamuzi wa kutoka bungeni JK atakapoingia na wewe ukapingana na uamuzi wa kikao cha kidemokrasia. Baada ya hapo ukaendelea kuropoka kwenye vyombo vya habari kwamba wewe unamheshimu JK ndiyo maana hukukubali uamuzi wa Chama chako. Jk na Chadema nani unamheshimu zaidi?
 
hahahahahah I love Tanzania Politics.....Namfananisha Zitto kama Mrema enzi zile na NCCR mageuzi alivyoanza kulumbana na akina Mabere Malando.....Matokeo yake chama kikasaramabatika ndiyo itakavyotokea Chadema....watch!...
 
Lazima Tukubali Yote Haya Waamuzi ni Wananchi wa Kigoma. Zitto Ndio Kawa Haribia Uwakilishi Bungeni na Miaka Hii Mitano Wananchi wa Kigoma Hawata Kuwa na Mwakilishi. Zitto Amekufa Kisiasa na Kilichobaki Aamie CCM Kama Lamwai Alivyofanya, Ukishajulikana Wewe Ni Dude Bovu Ndani ya Chadema Sijui Unasubiri Nini. Wanachama Wote Wanajua Huna Mchango Wowote Ila Ushushushu, Hana Kazi. Zitto Bye Bye Chadema...Kikubwa ni Kwamba Kazi ya CCM Kuuwa Upinzani Umefeli Tena, Wakati Huu Chadema na Wananchi Wanajua Tactics za CCM. Ni Aibu Sana kwa CCM Kutumia Fedha za Wananchi Kununua Influence Katika Vyama Vingine.

"CCM Tumieni Nafasi Hii Kuondoka Madarakani kwa Amani Kabla Wananchi Hawajawaondoa kwa Viboko. Hatuwataki Tena"
 
nimemsikia zito akisema haondoki chadema. na kuwa ameaga alikotoka. hivyo wale wanaoona choyo naye walie tu.
 
Watu wa kigoma wote uraia wao una utata na ndio maana watata...kazi ubishi tuu na kujiona wanajua kila kitu,kajitu kafupi,kichwa kibaya...aagh...taabu kwelikweli
 
Zitto anasema kweli na kweli tupu! Kwa nini wale wanne wa NCCR waliondoka Chadema? Jibu: wameona ni chama kinachoendeshwa Kidikteta na Kidini, kama ni muIslam huna thamani Chadema, kama yanayomkuta Zitto sasa hivi na karibuni tutasukia Arfi nae hayo hayo.

Acha upuuzi wewe, kwani hao waliotuimkia NCCR na kushinda Ubunge Kigoma ni Waislamu? Usiwe na akili kama za kuku; udini na ukabila vimekujaa kiasi kwamba unashindwa kufanya hata uchambuzi mdogo kama huo? Nakupa orodha ya Wabunge wa NCCR Kigoma- Felix Mkosamali- Muhambwe, David Kafulila- Kigoma Kusini, Agripina Zaituni Buyogela- Kasulu Vijijini. Haya, hao wote n Waislamu na Wachaga?
 
mapenzi ni kitu kibaya sana.mtu akiamua kutoa fikra na maono yake watu wengine wanamuona msaliti. wanataaka akubali tu kila lisemwalo na mboye na silahA!!!
 
Back
Top Bottom