Hivi mnaposoma hoja za mtu huwa mnasoma na kuzielewa ama?..nachosema mimi ni kwamba ugonvi wetu huko Bavicha hakuna sababu ya kumwingiza Kitila ktk mgogoro huu wala kumtaja Dr.Slaa aliamua vipi wakati hukuwepo kichwani kwake..Tunajua hamumpendi Zitto kabisa hata angekuwa na miaka 50.Mkandara bwana!!
Mleta mada hajamuingiza Kitila BAVICHA, nyinyi ndo mnamuingiza!! Mkuu sio vizuri kushadadia mambo ili kuleta mgongano! Mada inaeleweka vizuri msiingize mambo yenu!
Nimeamua kuwa msomaji maana naona Tuntemeke (from TUNduma toTEMEKE) lafikio kajitahidi kuja na ID mbili zikaumbuliwa kaanzisha ya tatu!! Wewe nae unapiga ndogondogo akija na M. Mwanakijiji, Ritz nae akachombeza lengo lazima litimie!!
Mmh!! Mi yangu macho Bwana Mkandara!! Nawaombea CDM kwa Mola busara na uvumilivu zaidi!!
Mada inaeleweka vizuri kwa mtazamo wako wewe lakini kwangu miye haya ni matusi ya nguoni.. Kiongozi hutakiwi kuwa chini kiasi hiki..Kuna mambo ya chama mnayaacha chamani, kuna msemo usemao What Happens in stays in Vegas sijui kama mnaelewa maana yake.. Mnachotuonyesha hapa ni jinsi gani msivyokuwa na hekima wala busara kutokana na makundi yenu ya ufitini..