Uchaguzi 2020 Zitto: Ilani ya ACT Wazalendo na utekelezaji wake


Mawazo mazuri sana haya big up mkuu ila hiyo hoja yako unayosuggest ya mtoto kuwekewa vizingiti kupata mkopo wa elimu ya juu kwa sababu eti baba yake huko zamani naye alikopa kwa ajili ya elimu yake lakini akashindwa kulipa deni imekaa kiuonevu, sikuungi mkono!. Kwa nini umuadhibu mtoto kwa deni ambalo si lake?

Pia sijaona popote kwenye bandiko la Zitto akisema kuwa elimu ya juu itakuwa bure, bali ameelezea utaratibu tofauti wa ulipiaji hiyo elimu.

Uzuri wa plan ya ACT ni kuwa watu wengi watakuwa covered kwenye kunufaika na elimu ya juu, na hili ni jambo chanya sana kwa Taifa.

Kuna correlation kati ya umasikini na kukosa elimu, kwa hiyo kama ACT watawekeza katika elimu kwa nguvu, si tu kwamba wataupiga vita ujinga bali wataupiga vita umasikini kwa kiwango kikubwa sana.

Pia kumbuka ACT ni Social democrats, wanaamini katika dhana ya umma kubeba jukumu la kujinusuru na kunusuru members wake collectively, Wewe umetoa wazo la Kibepari, yaani individualism. Hiyo sera yako inakifaa zaidi chama cha Kibepari kama Chadema lakini siyo vyama vyenye mirengo ya kijamaa
 
Sela ya Lisu na chadema:

Nlipigwa risasi 16
Magufuli kanunua jogoo kwa laki 1
 
Zitto akiacha papara chama chake kinaweza kuja kutawala!

Maana ni act pekee inaonesha ipo bara na zanzibar kama ilivyo ccm
 

Matarajio yenye kuvutia yasiyo na uchambuzi yakinifu na mlinganisho. Kwa mfano gharama za mwanafunzi mmoja wa chuo x idadi ya wanafunzi ikilinganishwa na kiasi kitakachopatikana kutokana na Tozo ya kuongeza ujuzi (Skills Development Levy - SDL)

Ni ahadi hewa hizo kwa kuwa viongozi wa ACT Mzalendo hawana ushahidi wa kutimiza ahadi zao.
 
Mie sipigi Kura...ujinga tu..kila nikikumbuka la lowasa nahis napata uchizi .. upinzani wanapisema wawe kitu kimoja wanaamanisha nn...maana lisu juzi nimemskia anasema hivyo mku5wa Act
Lisu Alisema chadema wamesimamisha wagombea nchi nzima, baadae akajishtukia kwamba kumbe yuko kwenye mkutano wa ACT ndio akasema itabidi tukae tuongee jinsi ya kuachiana ili tusigombane
 
Lisu Alisema chadema wamesimamisha wagombea nchi nzima, baadae akajishtukia kwamba kumbe yuko kwenye mkutano wa ACT ndio akasema itabidi tukae tuongee jinsi ya kuachiana ili tusigombane
Arghh
 
Hapo kwenye kufuta madeni ya Elim ya juu naona ni kutaka kufurahisha voters tu..
Hii nchi bila massive taxation maendeleo mtaendelea kuyaongea tu..
Wale ambao wameshalipa utawa refund?
Kwenye kurefund, hapo umenena sahihi, wengine walishamaliza kulipa, watakuwa refunded? Be as it may kufuta mikopo Ni Jambo la msingi Sana.
 
Sio kweli masmuzi ya halmashauri hufanywa na baraza la madiwani na meya wao .Ujiji iko chini ya ACT wazalendo walitakiwa waeleze walichoweka kwenye Ilani iliyopita walikitekelezaje kwenye halmashauri Yao ambako wao ndio waamuzi
Tuwe na kumbukumbu jamani. Umesahau JIWE alicentralise mapato yote kwenda kwake. Sasa hizo fedha za halmashauri ya ujiji, hata Kama wanakusanya, wangezichukuaje? Kumbuka hii ilikuwa kudhoofisha halmashauri zote zilizotwaaliwa na upinzani.
 
Zitto ndugu yangu hapo kwenye kutoza SDL hadi sector za umma sidhani itaiongezea mapato serikali ili muweze kufuta mikopo ya elimu ya juu.

SDL inalipwa na muajiri means kama itabidi sector ya umma ilipe maana yake ni serikali inalipa. Hapa hesabu hazipo sawa, ni kutoa mfuko huu na kurudisha mwingine. Mbaya zaidi serikali itabeba mzigo mkubwa kwa kufuta mikopo huku ilipe 2% SDL na hapo sector binafsi kulipa 2% badala ya 4% ni mapato kushuka kwa 2% zaidi.

Hapo fanyieni kazi hakuna uhalisia labda utoe ufafanuzi hiyo incremental benefit itatoka wapi. Ni kuzidi kuitwisha serikali mzigo huku pia kupunguza mapato kutoka private sector.
 
Pia mh Zitto ningependa kujua, mkishika madaraka mtaendelea na mipango ya miradi ya Strigler na SGR? Vipi ndege ambazo zipo kwenye mnyororo wa kuja kwaajili ya ATCL? Sheria ya madini mtaendelea na hii mpya au utarejesha ya zamani? Ningependa kujua chama chako kimejiandaa vipi kuanzia hapa tulipo hasa kwa miradi iliyo on progress.
 
Majuzi tu hapa serikali ilikuja na viwango vipya vya non taxable income kima chini ilikuwa laki mbili kutoka laki moja na nusu. Na mapunguzo mengine kwenye vyima vya juu.

Zitto akaja humu na uchambuzi wake (si ajabu kesha sahau kwa kusoma hii post yake) alidai hilo punguzo la serikali ni dogo wao watafuta kodi kima cha chini kabisa cha non taxable income kitakuwa laki tano na blah blah zingine na watapandisha watu mishahara pamoja madaraja kazini.

Leo tena ajaelezea hiyo hela ya kuongeza mishahara ataitoa wapi, keshakimbilia kuwaongezea kodi wafanyakazi kwa sababu ya funding za malipo ya wanafunzi. The irony ni kwamba watu ambao umedai wanapunjwa unafikiria tena kwenda kuwaongezea kodi ya 2% katika mapato hayo hayo ambayo unadai ni kiduchu.

Vitu vingine ata kuviongelea shida yaani anaongea kama kukopa 10 trillion ni jambo rahisi sana, wajameni kazi ya kupanga na kuchagua nchi maskini sio rahisi kama Zitto anavyopenda kuaminisha; yeye mwenyewe keshasahau juzi tu alikuwa anasema nini.
 
Yote hayo yanafanyika kwa sasa, wanachosema ACT WANANCHI kwenye Ilani yao hiyo ni uboreshaji tu wa kile kinachofanyika ndani ya Serikali hii ya Awamu ya Tano. Tatizo letu Watanzania ni kutokusoma na kufuatilia yanayofanyika sasa kwenye sekta au sehemu zote hizo na pesa ipo ndio maana yote yanafanyika. Uboreshaji kama sehemu ya mwendelezo wa yanayofanyika sasa hivi mtayaona kwenye kipindi cha 2020/2025 baada ya ushindi wa kishindo hapo Oktoba 2020.
 
Hanaga uhalisia kwenye lolote yeye kinachomjiaga kichwani ndio anachoandikaga.

Juzi tu alisema mishahara ya public workers ni kidogo; leo anafikiria icho kidogo kukipiga kodi ya 2% ku find project zingine wewe unaona huyo mtu anakumbuka ata miezi mawili nyuma alisema nini.
 
Uchambuzi mzuri na wakina.

Tatizo ni utekelezaji wale, na imani vyama vyote mwaka huu wataleta ilani nzuri changamoto ni utekelezaji wake na ni kwa namna gani wananchi tunaweza kuwabana ikiwa hamtotekeleza ikiwa mkishika dola.

Mwaka 2015 ilani ya CCM ilisema itapeleka milion 50 kila kijiji ila hadi leo hawajapeleka na hawana mpango huo. Wanajua fika hatuna cha kuwafanya.
 
mh Zitto vipi kuna matumaini yoyote/ mmefikia wapi kuhusu makubaliano kati yenu na cdm juu ya uchaguzi huu!? mana mkibugi kukubaliana uchaguzi huu mtaishia kugawana kura and concequently ccm itatoboa tuu.
 
Kila la kheri katika hili. ....Muhimu kama upinzani msigawane kura among yourselves fanyeni namna mufikie muafaka.
Hivi Lisu alivyo mbishi mtashirikiana vipi??
 
Ndugu .
Kiongozi wa Chama Pendwa cha Wananchi, ACT -Wazaleno Tanzania.
Kwanza Hongera kwa mafanikio ya kiuongozi na Usimamizi wa ujenzi wa chama Imara.
Nakumbushia tuu katika Ilani ya Chama musilisahau suala la wananchi kulipwa fidia kwa wote waliovunjiwa Majumba yao ili kupisha upanuzi wa Barabara. Kwa Dar es salaam ni Kimara hadi Kibaha, bila ya kuwasahau wale wa Jangwani. Na takriban kila mkoa Tanzania nzima wapo waathirika wanaofikia Milioni Moja na nusu au zidi.
Naomba Serikali ya ACT Wazalendo iwape faraja watu wale japo kwa kuwagawia angalau Viwanja na kuwalipa japo 1/3 ya hasara waliyoipata kwa kuvunjiwa makaazi yao. Hili litaiongezea Baraka Serikali ya ACT 2020-2025 na kupendwa sana na wananchi wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…