Wangari Maathai
JF-Expert Member
- Aug 13, 2018
- 34,962
- 70,576
Kuwa serious mkuu>>CCM B na CCM A wanaenda kugawana kura alafu nyinyi wapinzani mnashinda uchaguzi kilaini,sasa sijui hofu yako ni nini? Wewe shangalia tu ushindi upo karibu yenu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuwa serious mkuu>>CCM B na CCM A wanaenda kugawana kura alafu nyinyi wapinzani mnashinda uchaguzi kilaini,sasa sijui hofu yako ni nini? Wewe shangalia tu ushindi upo karibu yenu.
Ndugu yangu na kaka yangu Zitto Kabwe
Ilani yenu ni nzuri na naamni kabisa inaakisi mahitaji ya Wananchi wengi kwa sasa.Natamani nipate nakala kamili ya ilani yenu kabla sijaweka uchambuzi wangu kamili hapa ilakwa sababu umeweka kitu kidgo basi naweza kutoa maoni kwa kuzingatia hiki kidgo ulichoweka.
Mikopo ya ELimu ya Juu
Ilani yenu imezungumzi kutoa elimu ya Juu bure swali ni kwa nini muitoe bure?kwa sababu tuna uwezo wa kulipa,sababu wananchi hawawezi kulipa au ni sababu gani?Dhana ya maendeleo lazima iwe shirikishi kutoa ahadi ya kutoa elimu bure nafikir ni wazo zuri ila wakati wake bado.Binafsi nafikiri zaidi kwamba kwa rasilimali tulizo nazo lazima tupange na tuchague kwa umakini.Sikubaliana na hoja ya kufuta madeni ya nyuma ya mkopo ingawa najua yanaweza kuvutia kisiasa.Katika eneo hilo la Mikopo mnaweza kuweka utaratibu kwa wale wahitimu ambao kweli hawana uwezo wa kulipia au wana kipato kidogo sana Mfano Mhitimu wa Chuo kikuu atalipa mkopo wake pale tu anapokuwa na PATO la TZS Milion 1.5 and above ila chini ya hapo hatalazimika kulipa ingawa anaweza kuamua kuchangua kwa kiwango ambacho hakitakuwa katika asilimia kwa hiyari yake.
Deni lake halitafutwa,litaendelea kuwepo active kwa kipindi cha miaka 15.Na iwapo mhitimu huyu ambaye hajalipa deni atakuwa na mtoto wake ambaye anahitaji mkopo basi credit rating ya baba yake itaathiri kiwango cha mkopo atakachopewa mwanae kwa kuzingatia uwezo wa mzazi kwa wakti huo na performance ya mtoto.Hu ni mtazamo na uhauri wangu kwenye swala hili.
Jambo la muhimu zaidi ni kuongeza financing katika mfumo wa elimu za ufundi stadi ni ikiwezekana mikopo itolewe katika ngazi hii ya elimu kwani tukiwa na mafundi stadi wenye ujuzi wanaweza kuzalisha ajira na bidhaa kuliko wahitimu ambao wengi wanahitaji white collar jobs ambazo ni very limited.
BIMA YA AFYA NA HIFADHI YA JAMII
Kwenye swala la Bima ya afya naona una nia nzuri ila hapo napendekeza zaidi uangalie kuhusu ukweli kwamba swala BIMA ya AFYA ni swala la kiutamaduni zaidi kuliko swala fedha.Kuunganisha bima ya afya na other aspect za social security ni hatari hasa ukizingatia kwamba zote hizo ni very sensitive and resource demanding sectors.
Binafsi naamini kwamba suala la Universal Health coverage linahitaji kuwezesha mtu mtu kupata BIMA kwa bei nafuu.Kwa mfano,Katika Mfumo wa TAX assessment katika Biashara uwekwe utaratibu kwamba Ukishapewa TIN number na kulipa kodi unakuwa entitle kupewa BIMA ya afya at percent ya TAX estimates zako kwa kuzingatia mapato yako.Mfano Kama mtu amekadiria kwamba kodi yake kwa mwaka ni TZS 500,000 basi atachangia kiasi sawa na mafanyakazi anayelipwa mshahara wa kiwango hicho with discount kidogo.na pia atachangia kwenye social security kiwango kidogo.Lengo ni kutengeneza MFumo wa BIMA ya AFYA na HIFADHI YA JAMII AMBAO ni inclusive.
SWALA LA MAJI SAFI NA SALAMA
Katika Swala hili PPP ndio solution,Serikali itoe incentive kwa watu binafsi kuwekeza katika kuchimba na kusambaza maji katika maeneo mbalimbali.Watu Binafis wataweka mitaji yao humo huku wakijua watapata mapato.Halihitaji Rocket Sayansi hili linahitaji NIA thabiti tu na ujasiri na uzalendo.Tukifanya hivyo watu watabeba maji ya chumvi kutoka Dar na kuyapeleka DODOMA.
Hii barabara ya KOROSHO sitaki kusema chochote ila embu anza kufikiri in terms of RAILWAY TRANSPORT nafikir tunahitaji nchi nzima iunganishwe na Mtandao wa Reli.
KUHUSU MAPINDUZI YA KILIMO
Hili lina mipango mingi lakini cha muhimu zaidi katika kilimo chetu ni masoko.Mfumo mzuri wa masoko ukiwepo watu watalima maana wanayo mitaji ila tatizo ni masoko bado serikali inmeshidwa kuweka mfumo mzuri wa kuhamasisha masoko ya nje.Mfano Rahisi ni swala la Commodity Exchange Market ambayo ilianza na kubaki kuwa exclusive na bureaucratic
Iwapo ungependa zaidi niitazame ilani yenu tena na kuitolea maoni zaidi tafadhali nimekutumia Messeji PM,Sasa usije kuwa kama ile aina ya iongozi ambao wakitumiwe messeji hawarudi kwa sababu wanafikiri kwamba wao ni wakubwa zaidi,wana elewa zaidi,wana akili zaidi,wanaweza zaidi,Be humble and GOD will show you the WAY
Ubarikiwe sana
Mbunge wa Wananchi
Kimbiji Kigamboni
Ahadi za ACT Wazalendo Jamhuri ya Muungano ZITATEKELEZWAJE?
1. Elimu ya Juu: Kufuta mikopo yote ya miaka ya nyuma iliyotolewa kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu na kuanza kutekeleza Mfumo mpya wa kugharamia Elimu ya Juu.
FEDHA ZA KUTEKELEZA ZITATOKA WAPI?
- Gharama za Elimu Ufundi na Elimu ya Juu zitatokana na Mapato ya Tozo ya kuongeza ujuzi ( Skills Development Levy - SDL ). ..
Kitengo cha Kampeni ACT Wazalendo
Agosti 7, 2020
Lisu Alisema chadema wamesimamisha wagombea nchi nzima, baadae akajishtukia kwamba kumbe yuko kwenye mkutano wa ACT ndio akasema itabidi tukae tuongee jinsi ya kuachiana ili tusigombaneMie sipigi Kura...ujinga tu..kila nikikumbuka la lowasa nahis napata uchizi .. upinzani wanapisema wawe kitu kimoja wanaamanisha nn...maana lisu juzi nimemskia anasema hivyo mku5wa Act
ArghhLisu Alisema chadema wamesimamisha wagombea nchi nzima, baadae akajishtukia kwamba kumbe yuko kwenye mkutano wa ACT ndio akasema itabidi tukae tuongee jinsi ya kuachiana ili tusigombane
Kwenye kurefund, hapo umenena sahihi, wengine walishamaliza kulipa, watakuwa refunded? Be as it may kufuta mikopo Ni Jambo la msingi Sana.Hapo kwenye kufuta madeni ya Elim ya juu naona ni kutaka kufurahisha voters tu..
Hii nchi bila massive taxation maendeleo mtaendelea kuyaongea tu..
Wale ambao wameshalipa utawa refund?
Tuwe na kumbukumbu jamani. Umesahau JIWE alicentralise mapato yote kwenda kwake. Sasa hizo fedha za halmashauri ya ujiji, hata Kama wanakusanya, wangezichukuaje? Kumbuka hii ilikuwa kudhoofisha halmashauri zote zilizotwaaliwa na upinzani.Sio kweli masmuzi ya halmashauri hufanywa na baraza la madiwani na meya wao .Ujiji iko chini ya ACT wazalendo walitakiwa waeleze walichoweka kwenye Ilani iliyopita walikitekelezaje kwenye halmashauri Yao ambako wao ndio waamuzi
Kuwa serious mkuu>>
Yote hayo yanafanyika kwa sasa, wanachosema ACT WANANCHI kwenye Ilani yao hiyo ni uboreshaji tu wa kile kinachofanyika ndani ya Serikali hii ya Awamu ya Tano. Tatizo letu Watanzania ni kutokusoma na kufuatilia yanayofanyika sasa kwenye sekta au sehemu zote hizo na pesa ipo ndio maana yote yanafanyika. Uboreshaji kama sehemu ya mwendelezo wa yanayofanyika sasa hivi mtayaona kwenye kipindi cha 2020/2025 baada ya ushindi wa kishindo hapo Oktoba 2020.Ahadi za ACT Wazalendo Jamhuri ya Muungano ZITATEKELEZWAJE?
1. Elimu ya Juu: Kufuta mikopo yote ya miaka ya nyuma iliyotolewa kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu na kuanza kutekeleza Mfumo mpya wa kugharamia Elimu ya Juu. Serikali italipia Ada ya Masomo (Tuition Fee), Fedha za Vitabu (Stationeries), na gharama za Mafunzo kwa Vitendo (Field Studies/Internship) kwa kila mwanafunzi anayedahiliwa kwenye Chuo Kikuu. Wanafunzi watachukua mikopo, Kwa wanaotaka, Kwa ajili ya gharama za maisha tu ( Meals and Accommodation ). Mfumo mpya utaanza Mwaka wa Masomo 2021/2022.
FEDHA ZA KUTEKELEZA ZITATOKA WAPI?
- Gharama za Elimu Ufundi na Elimu ya Juu zitatokana na Mapato ya Tozo ya kuongeza ujuzi ( Skills Development Levy - SDL ). Tozo hii itatozwa kutoka Waajiri wa sekta binafsi na sekta ya Umma Kwa kiwango cha 2% ya gharama za mishahara. Sasa hivi tozo hii inatozwa kwa sekta binafsi peke yake Kwa kiwango cha 4% ya gharama zote kwa Wafanyakazi walioajiriwa na kampuni husika ( SDL is charged based on the gross pay of all payments made by the employer to the employees employed by such employer ). Baada ya marekebisho ya kupanua wigo wa walipaji, Serikali itakuwa na uwezo wa kukusanya shilingi Bilioni 470 kila Mwaka. Mapato haya yataongezeka kulingana na kuongezeka kwa shughuli za Uchumi Nchi na Ajira nyingi zaidi kutengenezwa.
2. Bima ya Afya kwa Wote: Kuboresha mfuko wa Bima ya Afya kwa kuunganisha na mifumo ya Hifadhi ya Jamii, ili kila Mtanzania anapochangia hifadhi ya jamii awe anapata huduma ya Afya moja kwa moja. Kwa mfumo huu, mfuko wa Bima ya Afya utaweza pia kupata fedha kwa wakati na kulipa watoa huduma kwa wakati. Bima ya Afya ni haki ya kila Mtanzania. Itaisimamia kikamilifu haki ya kila Mtanzania kuwa na Bima ya Afya yenye kumpa kinga ya matibabu bila kujali hali yake ya kiafya (wakati wa kujiunga na bima).
FEDHA ZA KUTEKELEZA ZITATOKA WAPI?
- Kupitia vyama vya Ushirika na vikundi vya uzalishaji vya Wananchi haswa Wakulima, Wafugaji na Wavuvi Serikali itaanzisha Mfumo wa kuchangia wananchi wanaochangia Skimu ya Hifadhi ya Jamii. Serikali itatenga Fedha kutoka kwenye Bajeti kila Mwaka kuchangia michango ya Wananchi kwenye Hifadhi ya Jamii ( matching scheme). Kwa mfano katika mchango wa Shs 30,000 kwa Mwezi, Serikali itamchangia Mwananchi Shs 10,000. Kwa njia hii kila Mtanzania atakuwa na Bima ya Afya Kama Fao katika Skimu ya Hifadhi ya Jamii. Skimu hii itawezesha Taifa kuwa na Akiba kubwa kwa uwiano wa Pato la Taifa (savings - GDP ratio) na hivyo kuwezesha uwekezaji mkubwa na wa muda mrefu kufanyika. Kwa Makadirio ya Watu Milioni 6 watakaojiunga na Skimu ya Hifadhi ya Jamii, Mfuko utakuwa makusanyo ya Shilingi Trilioni 2.2 kwa Mwaka, katika hizo Shilingi Bilioni 648 zitachangiwa na Serikali kutoka kwenye Bajeti.
3. Maji safi na salama kwa kila Mtanzania: Kuwekeza kiasi cha shilingi Trilioni 10 ndani ya miaka mitano, wastani wa Shilingi Trilioni 2 kwa kila mwaka, kwenye kumaliza kabisa tatizo la maji safi na salama kwa Wananchi. Hii ni pamoja na kujenga na kupanua miundombinu ya maji safi na maji taka.
FEDHA ZA KUTEKELEZA ZITATOKA WAPI?
- Gharama za Ujenzi wa Miradi ya Maji zitagharamiwa na Tozo Maalumu ya Matumizi ya Mafuta ya Petroli. Serikali itachukua Mkopo nafuu wa Muda mrefu wa Shilingi Trilioni 10 kutoka Benki za Maendeleo ili kutekeleza mradi kwa mara moja na Mapato ya ‘fuel levy’ yatahudumia mkopo huo mpaka utakapomalizika kulipwa. Tozo ya shilingi 200 kwa kila lita ya Mafuta itazalisha Jumla ya shilingi Bilioni 700 kila Mwaka zinazoweza kutumika kulipa mkopo wa muda mrefu wa miaka 15.
4. Barabara ya Korosho: Kuwezesha Ujenzi wa barabara ya korosho (cashew ring road) – Nangurukuru – Liwale – Nachingwea – Masasi – Newala – Tandahimba – Mtwara – Lindi - Nangurukuru kutoka mapato ya ushuru wa korosho kwa kutumia mfumo wa “development finance” ili kufungua wilaya zinazolima korosho. Vile vile kufungua Wilaya ya Liwale kwa kufungua barabara za Songea-Liwale na Liwale-Morogoro
FEDHA ZA KUTEKELEZA ZITATOKA WAPI?
- Gharama za Ujenzi wa Barabara ya Korosho (Cashew Ring Road) zitalipiwa na 50% ya Mapato ya Ushuru wa Korosho (exports levy) ambapo Serikali itachukua mkopo nafuu wa muda wa kati ili kupata fedha za ujenzi wa barabara hiyo mara moja na mapato ya exports levy yatahudumia mkopo huo mpaka utakapomalizika kulipwa. Ushuru wa Korosho unakadiriwa kuingiza mapato ya zaidi ya shilingi Bilioni 245 kila Mwaka ambazo nusu yake inaweza kulipa mkopo wa barabara hiyo na barabara za Songea-Liwale na Liwale-Morogoro kwa muda wa miaka 10.
5. Kilimo cha kimapinduzi: Kusimamia Ujenzi wa mabwawa makubwa 5 ya kuzuia mafuriko na kujenga skimu kubwa za umwagiliaji zenye jumla ya hekta 1,000,000 zitakazowezesha Kilimo cha kimapinduzi, mamilioni ya ajira, uzalishaji wa mazao ya mafuta ya kula, sukari na chakula hivyo kuokoa fedha za kigeni zinazotumika kuagiza sukari na mafuta ya kula kutoka nje, na kuongeza Mapato ya Fedha za Kigeni.
FEDHA ZA KUTEKELEZA ZITATOKA WAPI?
- Gharama za Miradi mikubwa ya Umwagiliaji zitalipiwa kutoka uwekezaji wa skimu ya Hifadhi ya Jamii kwa Wakulima kama uwekezaji wa Skimu wa muda mrefu. Jumla ya Shilingi Trilioni 2.5 zitawekezwa kwenye miradi hii ya uwekezaji kutoka Skimu ya Hifadhi ya Jamii kama Uwekezaji wa kuongeza shughuli za uchumi Kwa kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo na Viwanda vya kuongeza mazao ya Kilimo.
Kitengo cha Kampeni ACT Wazalendo
Agosti 7, 2020
Hanaga uhalisia kwenye lolote yeye kinachomjiaga kichwani ndio anachoandikaga.Zitto ndugu yangu hapo kwenye kutoza SDL hadi sector za umma sidhani itaiongezea mapato serikali ili muweze kufuta mikopo ya elimu ya juu.
SDL inalipwa na muajiri means kama itabidi sector ya umma ilipe maana yake ni serikali inalipa. Hapa hesabu hazipo sawa, ni kutoa mfuko huu na kurudisha mwingine. Mbaya zaidi serikali itabeba mzigo mkubwa kwa kufuta mikopo huku ilipe 2% SDL na hapo sector binafsi kulipa 2% badala ya 4% ni mapato kushuka kwa 2% zaidi.
Hapo fanyieni kazi hakuna uhalisia labda utoe ufafanuzi hiyo incremental benefit itatoka wapi. Ni kuzidi kuitwisha serikali mzigo huku pia kupunguza mapato kutoka private sector.
Hivi Lisu alivyo mbishi mtashirikiana vipi??Kila la kheri katika hili. ....Muhimu kama upinzani msigawane kura among yourselves fanyeni namna mufikie muafaka.
Ndugu .Ahadi za ACT Wazalendo Jamhuri ya Muungano ZITATEKELEZWAJE?